Mkutano wa G7: Mpango ulioidhinishwa na mataifa tajiri dhidi ya Uchina uko vipi?

G7 leaders meeting in Carbis Bay, Cornwall (11 June)

Chanzo cha picha, Leon Neal/PA Media

Viongozi wa nchi zenye tajiri zaidi duniani G7 wanaotaka kukabiliana na Uchina ameidhinisha mpango wa kusaidia nchi zenye lkipato cha chini-na cha kati katika ujenzi wa miundo mbinu bora.

Rais Joe Biden alisema anataka mpango unaoungwa mkono na Marekani wa kujenga tena dunia bora (B3W) kuwa wa ubora wa hali ya juu ambao utakuwa badala ya mpango wa aina hiyo wa Uchina.

Mpango wa Uchinia wa Belt and Road Initiative (BRI) umesaidia kufadhili ujenzi wa miundo mbinu ya treni, barabara, na michezo katika nchi nyingi.

Lakini umekuwa ukikosolewa kwa baadhi yake kuambatana na madeni.

Katika taarifa yao kwenye kikao hicho katika kaunti ya Uingereza ya Cornwall, viongozi wa G7 walisema watatoa ushirikiano "wenye misngi ya maadili, kiwango cha juu na wa uwazi."

Hatahivyo, maelezo kuhusu ni vipi mpango wa G7 utakavyofadhiliwa bado hayajawa wazi. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa kikundi hicho bado hakijafikia kwenye hatua ya kutangaza ufadhili wake kwa ajilio ya mpango huo.

Marekani hasa imekuwa mkosoaji mkubwa wa kile kinachoitwa "diplomasia ya deni" ya Uchina.

Mpango wa Uchina wa kusaidia nchi masikini ujenzi wa miundo mbinu umekuwa ukikosolewa kwa baadhi yake kuambatana na madeni
Maelezo ya picha, Mpango wa Uchina wa kusaidia nchi masikini ujenzi wa miundo mbinu umekuwa ukikosolewa kwa baadhi yake kuambatana na madeni

G7, ambacho ni kikundi cha viongozi wa mataifa saba yenye utajiri zaidi duniani, pia wanatarajiwa kuweka ahadi zao kwenye mpango wa kuzuia majanga yajyayo.

Hatua hizo ni pamoja na kupunguza muda unaohitajika wa kutengeneza chanjo na tiba ya Covid-19 hadi chini ya siku 100.

Waziri Mkuu wa uingereza Boris Johnson ni mwenyeji wa kikao hicho cha siku tatu kinachofanyika katika hoteli iliyopo kwenye mwambao wa bahari ya Carbis Bay katika Cornwall.

Unaweza pia kusoma:

Hadi sasa ni nini ambacho nchi za magharibi zenye nguvu za mzimeifanyia uchina?

Mapema mwka huu, Marekani, Muungano wa Ulaya, Uingereza na Canada zilianzisha vikwazo vilivyoratibiwa dhidi ya Uchina.

Vikwazo hivyo vilikuwa ni pamoja na vya safari, kufuja mali, kuwalenga maafisa wa ngazi ya juu katika Xinjiang ambao wamekuwa wakishutumiwa kwa ukiukaji mkbwa wa haki za binadamu dhidi ya Waislam wa Uyghur.

Zaidi ya Wauyghur na jamii nyingine za walio wachache wanakadiriwa kuwa wamekuwa wakishikiliwa kwenye makambi yaliyoko katika jimbo la kaskazini-magharibi.

Serikali ya Uchina imekuwa ikishutumiwa kwa kuwafunga vizazi kwa nguvu wanawake wa Uyghur na kuwatenganisha watoto na familia zao.

Workers walk by the perimeter fence of what is officially known as a vocational skills education centre in Dabancheng in Xinjiang Uighur Autonomous Region, China September 4, 2018.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Uchina imebuni mtandao wa kambi za mahabusu kutoka jamii za walio wachache katika jimbo la Xinjiang

Uchunguzi wa BBC uliochapishwa mwezi Februari ulikuwa na ushahidi wa kuaminika wa ubakaji wa kupangwa, unyanyasaji wa kingono na mateso ya wafungwa.

Uchina ilijibu kwa vikwazo vyake dhidi ya maafisa wa Ulaya.