China imeshutumiwa kuwalazimisha wanawake wa kiislamu wa jamii ya Uighur kufunga kizazi

Chanzo cha picha, AFP
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Dominic Raab ameishutumu china kwa vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya jamii ndogo ya kiislamu ya Uighur na kusema kuwa vikwazo dhidi ya waliohusika hivitaondolewa.
Ripoti za kulazimisha jamii hiyo kufunga kizazi pia kuteswa kwa jamii hiyo ya kiislamu ilikwa ''kumbukumbu ambayo ilikuwa haionekani kwa muda mrefu'', aliiambia BBC.
Uingereza itafanya kazi na washirika wake kuchukua hatua madhubuti, alisisitiza.
Balozi wa China nchini Uingereza amesema kuwa madai hayo ni ''uongo''.
Liu Xiaoming amemwambia Andrew Marr wa BBC kuwa jamii ya Uighur wanatendewa sawa kwa mujibu wa sheria kama ilivyo kwa makundi mengine ya kikabila nchini mwake.
Picha zilizochukuliwa na ndege isiyo na rubani ilionesha watu wa kabila la Uighur wakiwa wamefunikwa macho na kuongozwa kwenye treni, picha zilizooneshwa na vikosi vya usalama vya Australia, alisema ''hafahamu'' video hizo zilikuwa zikionesha nini na '' wakati mwingine unasafirisha wafungwa kuelekea nchi yoyote''.
''Kuna shutuma nyingi za uongo dhidi ya China.'' na hakuna kambi zinazowashikilia''.
Inaaminika kuwa kuna watu wa jamii ya Uighur na wengine hasa wa jamii ya kiislamu wanaoshikiliwa nchini China, kambi ambazo sinaelezwa kuwa kama ''kambi za kutoa elimu ya kubadili imani yao.
Awali China ilikataa uwepo wa makambi hayo, kabla ya kutetea kuwa ni hatua muhimu dhidi ya ugaidi, baada ya kutokea machafuko katika mji wa Xinjiang.
Mamlaka hivi karibuni zimeshutumiwa kuwashinikiza wanawake kufunga kizazi au kutumia njia za uzazi wa mpango ili kudhibiti idadi yao, hali iliyosababisha wito kutolewa kwa Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi.

Chanzo cha picha, AFP
Wito umekuwa ukizidi kutolewa kwa Uingereza kuweka vikwazo, kama vile kuzuia mali na marufuku ya kuingia Uingereza dhidi ya maafisa wa China kwa kuwatesa watu wa jamii ya Uighur.
Hivi karibuni Uingereza ilichukua hatua dhidi ya majenerali wa juu nchini Myanmar ambao waliongoza kampeni ya unyanyasaji dhidi ya jamii ya Rohingya na pia nchini Korea Kasikazini.
Wabunge wa Conservative pia wameshinikiza hatua zichukuliwe dhidi ya maafisa wa juu katika serikali ya Hong Kong kutokana na kuwekwa sheria ya usalama ambayo Uingereza inakiuka makubaliano ya kimataifa ya kulinda uhuru.
Je Uighur ni nani?
Watu wa kabila la Uighur ni Waislamu asilimia 45 ya watu wanaoishi katika jimbo la Xinjiang ; 40% ni watu wa kabila Han Chinese.
China ilichukua udhibti wa eneo hilo 1949 baada ya kuliangamiza jimbo la Mashariki mwa Turkestan.
Tangu wakati huo kumekuwa na uhamiaji mkubwa wa watu wa kabila la Han Chinese na watu wa kabila la Uighur wanahofia mmomonyoko wa utamaduni wao
Xinjiang ni jimbo huru ndani ya China, kama Tibet iliopo kusini mwake.












