Kwanini serikali ya Uchina inawafurusha Maimam misikitini?

Chanzo cha picha, Getty Images
Takriban Maimam 630 na viongozi wengine wa dini ya kiislamu wamekamatwa nchini uchina tangu mwanzoni mwa operesheni ya kuwakamata iliyoanza katika jimbo la Xingiang mwaka 2014, a kulingana na utafiti uliofanyw ana kikundi cha haki za binadamu cha jamii ya Uighur.
Matokeo ya utafiti huo ambayo yameifikia BBC pia yamebaini ushahidi kwamba maimamu 18 walikufa muda mfupi baada ya kukamatwa.
Wengi wa viongozi wa dini ya kiislamu waliokamatwa walishitakiwa kwa makosa kama vile "kueneza itikadi kali'', "kuwakusanya watu pamoja kinyume na maagizo ya serikali ", na "uchochezi ".
Kulingana na walioshuhutia matukio ya kamatakamata ya maimamu, mashitaka dhidi yao yalitokana na shughuli za kawaida, mikutano ya kidini na kwa kuwa walikuwa ni Maimam.

Chanzo cha picha, Getty Images
Shirika la haki za binadamu la Uighur UHRP, linalohusika na utetezi wa haki za watu wote, liliweza kubaini hali ngumu ya ya maisha ya Maimam 1,046 wengi wao wakiwa ni wa asili ya Uyghur - kupitia nyaraka za mahakama, ushahidi wa familia na vyombo vya habari vya taifa na taarifa za vyombo vya habari.
Kati ya viongozi wa kidini wa kiislamu 630 waliokamatwa 304 walipelekwa gerezani kwa madai ya kuipinga serikali na hivyo kupelekwa katika kile kinachoitwa kambi ya "kuelimishwa upya" ambako mashirika ya kibinadamu yanasema serikali ya Uchina inawafungia waislamu wa Uighur.
Uchina imetetea hatua yake ya kuwakamata na kuwapeleka kambini maimam hao, ikisema ni ya muda tu ambako , "wanajifunza " mbinu za kuzuia vitendo vya ugaidi na itikadi kali za kidini.
Data kutoka mahakamani na kindi cha kufungwa kwao, zinaonesha kiwango cha ukosefu wa haki katika jimbo la Xinjiang province: 96% ya maimam na viongozi wa kidini walihukumiwa kwa takriban miaka mitano gerezani, 26% walihukumiwa kifungo cha miaka 20 au zaidi, na watu 14 walihukumiwa kifungo cha maisha jela.
Data zilizokusanywa na mtafiti Abduweli Ayup, mwanaharakati katika Uighur ambaye pia anatoka katika kikundi cha Wahanga wa Uighur katika jimbo la Xinjiang , ni tofauti na za wizara ya sheria ya Uighur- ambazo zinataja idadi ndogo sana ya idadi ya Maimam waliopo katika jimbo.
Lakini zinatoa mwangaza wa watu binafsi, viongozi wa kidini ambao wamekuwa wakiengwa , na kuonesha kuwa kuna tatizo kwamba serikai ya Uchina inajaribu kuangamiza utamaduni wa dini ya watu wa Uighur kuwaingiza katika utamaduni wa kawaida wa Uchina.
Serikali ya Uchina imekanusha madai haya dhidi yake, ikisema kuwa mpango unaoendelea katika Xinjiang unalenga tu "kuwaelimisha upya " watu na kumaliza fikra za itikadi kali miongoni mwa Wauighur na Waislamu wengine walio wachache .
Kuhusisha dini na itikadi kali

Uchina inaaminiwa kuwakamata zaidi ya watu milioni moja wa jamii ya Uighur na Waislamu wengine katika jimbo la Xinjiang , ambalo ni jimbo kubwa kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, na nyumbani kwa watu wa jamii ya tofauti ya Turkic.
Serikali imekuwa ikikosolewa kwa kutekeleza ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu katika jimbo hilo, ikiwa ni pamoja na kuwatumikisha watu kazi za lazim na ubakaji.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ni nadra sana kuona vituo vinavyofahamika vya mahabusu, na wala hakuna taarifa kuhusu kesi, lakini wale wanaoonekana wanaonesha ni kwa jinsi gani serikali ya Uchina imehusisha matendo ya kawaida ya dini ya Xinjiang na itikadi kali au upinzani wa kisiasa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuna ushahidi pia kwamba maelfu ya watu bado wako gereani. Harakati za kuwakamata katika jimbo la Xinjiang ziliongezeka katika miaka ya 2017 na 2018, kulingana na Makala ya gazeti la New York Times. Iliongeza kuwa watu wapatao 230,000 walikamatwa- idadi hiyo ikiwa ni 200,000 zaidi ya miaka ya nyuma.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wachambuzi katika Xinjiang wanasema misikiti 16,000 imekwisha haribiwa. Idadi hiyo ni sawa na theluthi moja ya misikiti yote ya Xinjiang.
Mwanaume mmoja kwa jina Memet, wa Uighur ambaye alitoroka kutoka Xinjiang, aliiambia BBC kwamba baba yake alikamatwa 2017 baada ya kuwa Imam kwa amani kwa miaka mingi, na anasema anafuatilia hali ya familia yake kwa njia ya simu maana yuko mbali na hawezi kuwaona.












