Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vyama vya Upinzani Israel vyakubaliana kuunda serikali ya muungano
Vyama vya upinzani vya Israeli vimefikia makubaliano ya kuunda serikali mpya ambayo itamaliza miaka 12 ya utawala wa Benjamin Netanyahu kama waziri mkuu.
Yair Lapid, kiongozi wa chama cha mrengo wa kati cha Yesh Atid, alitangaza muungano kwamba muungano wa vyama vinane ulikuwa umeafiakiwa
Chini ya utaratibu wa kupokezana mamlaka , mkuu wa chama cha mrengo wa kulia Yamina, Naftali Bennett, atahudumu kama waziri mkuu kwanza kabla ya kumkabidhi Bw Lapid.
Bado kuna haja ya kuwa na kura ya bunge kabla ya serikali kuapishwa.
Katika taarifa, Bw Lapid alisema amemfahamisha Rais Reuven Rivlin juu ya makubaliano hayo, na kuongeza: "Ninaahidi kuwa serikali hii itafanya kazi katika kuhudumia raia wote wa Israeli, wale waliopigia kura na wale ambao hawakufanya hivyo.
"Itaheshimu wapinzani wake na kufanya kila kitu kwa uwezo wake kuunganisha sehemu zote za jamii ya Israeli."
Picha iliyochapishwa na vyombo vya habari vya Israeli ilionyesha Bwana Lapid, Bwana Bennett na kiongozi wa chama cha Waislamu cha Raam, Mansour Abbas, wakitia saini makubaliano hayo, makubaliano ambayo wengi walidhani hayangewezekana
Bwana Abbas aliwaambia waandishi wa habari: "Uamuzi huo ulikuwa mgumu na kulikuwa na mizozo kadhaa lakini ilikuwa muhimu kufikia makubaliano." Alisema kuwa kulikuwa na "mambo mengi katika makubaliano haya kwa faida ya jamii ya Kiarabu".
Katika barua yake kwa rais, Bw Lapid alisema ataongoza serikali pamoja na Bwana Bennett na atachukua nafasi ya waziri mkuu mnamo 27 Agosti 2023.
Bwana Rivlin ametoa wito kwa bunge kukutana haraka iwezekanavyo ili kupiga kura ya kuidhinisha serikali mpya
Ikiwa muungano utakosa kuungwa mkono na wengi katika bunge la Knesset lenye viti 120, kuna hatari ya nchi hiyo kulazimika kwenda kwenye uchaguzi kwa mara ya tano katika miaka miwili.
Wanachama wa muungano huo ni kutoka vyama vyote vya siasa za Israeli. Vyama hivyo havikaribiana katika sera za kisiasa ila uchu wavyo wa kumtoa bwana Netanyahu uongozini
Vingozi hao ni :
- Yesh Atid (Mrengo wa kati ) - kinachoongozwa na Yair Lapid ( viti 17)
- Kahol Lavan (Blue and White) (mrengo wa kati t) - kiongozi yBenny Gantz (viti 8)
- Israel Beiteinu (mrengo wa kati hadi wa kulia ) - kiongozi Avigdor Lieberman (viti 7 )
- Labor (Demokrasia ya kisosholisti ) - kiongozi ni Merav Michaeli (viti 7 )
- Yamina (mrengo wa kulia - kiongozi ni Naftali Bennett (viti 7)
- New Hope (mrengo wa kulia kati hadi wa kulia)- kiongozi ni Gideon Sa'ar (viti 6 )
- Meretz (mrengo wa kushoto left-wing, Demokrasia ya kisosholisti) - kiongozi ni Nitzan Horowitz (viti 6)
- Raam (Waarabu waislamu) - kiongozi ni Mansour Abbas (viti 4)
Vikundi vyote nane vilihitajika kupitisha idadi ya kura 61 .
Mazungumzo ya muda mrefu siku ya Jumatano yalifanyika katika hoteli karibu na Tel Aviv, na idadi kubwa ya maswala - kutoka kuhalalisha bangi hadi faini kwa ujenzi haramu hadi kubadilishana nafasi za kamati za uteuzi wa mahakama - yote yakiwa kwenye ajenda.
Vyombo vya habari vya Israeli vilisema kuwa sio vitu vyote vilikamilishwa, na hii bado inaweza kusababisha mashaka juu ya ikiwa muungano utashinda kura yake ya imani
Chama cha Likud cha Bw Netanyahu cha mrengo wa kulia kilishinda viti vingi katika kura ambayo haikutamatishwa ya Machi, lakini hakuweza kuunda muungano wa kuunda serikali .
Bwana Netanyahu alikuwa ameiita serikali mpya inayopendekezwa kuwa "Ulaghai wa karne", akisema inahatarisha serikali na watu wa Israeli.
Mhariri wa BBC wa Mashariki ya Kati, Jeremy Bowen, anasema kwamba kushindwa kwa Bwana Netanyahu kulisababishwa sio na wapinzani wa mrengo wa kushoto lakini na wenzake wa mrengo wa kulia ambao alikuwa amewafanya kuwa maadui na mbinu zake za kukabiliana nao vikali .
Hakuna mtu anayepaswa kutarajia mipango mikubwa, mipya kutoka kwa muungano huu mpya mwandishi wetu anasema, akiongeza kuwa kazi kubwa kwao itakuwa kushirikiana tu ili kuendelea kukabiliana na Bwana Netanyahu