Naftali Bennett, Mfahamu mshirika wa karibu wa Benjamin Netanyahu aliyebadilika na kuwa mpinzani wake mkuu Israel

Naftali Bennett amekuwa akiwania nafasi ya kuwa waziri mkuu wa Israel kwa muda mrefu sasa, lakini uteuzi wake umewashangaza wengi katika chama chake, Yamina, alishinda viti vichache tu katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana pekee.

Licha ya kujiunga kwa pamoja kwa mara ya tano wakiwa na viti saba, bwana Bennett ameapishwa kuwa waziri mkuu akiwa na msaada muhimu dhidi ya pande mbili zilizokuwa zikishindania kuunda serikali ya mpito.

Alipewa wadhifa wa kuwa kiongozi na wote walio madarakani, Benjamin Netanyahu, na kiongozi wa upinzani Yair Lapid. Hivyo mwisho wa siku kumuunga mkono bwana Bennett licha ya kutofautiana sana kiitikadi.

Naftali Bennett, 49, aliwahi kuwa mshirika wake bwana Netanyahu, kwa kuwa mkuu wa wafanyakazi tangu mwaka 2006 mpaka 2008, wakati wawili hao walipokosana.

Aliondoka chama cha bwana Netanyahu cha Likud party na kujiunga na mrengo wa pili katika chama cha taifa cha dini ya kiyahudi, na kuweza kuijngia bungeni baada ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2013.

Ameendelea kuwa waziri katika serikali zote za muungano mpaka mwaka 2019, wakati ambao chama chake kiliposhindwa kupata ushindi kwa mwaka huo.

Lakini miezi kumi na moja baadae , bwana Bennett alifanikiwa kurejea bungeni kama kiongozi wa Yamina (waebrania wa mrengo wa kulia).

Mara nyingi alionekana kuwa mzalendo, alikuwa anajitambulisha kama mtu wa mrengo wa kulia zaidi ya bwana Netanyahu), Naftali Bennett amekuwa anaongea waziwazi kuwa mtetezi wa Israel kama taifa la kiyahudi na katika historia ya Uyahudi na madai ya kidini katika kingo za magharibi, Mashariki mwa Yerusalemu na upande wa eneo la Syria -lililochukuliwa na Israeli tangu mwaka 1967 wakati wa vita vya mashariki ya kati.

Kwa muda mrefu ametetea haki ya makazi ya Wayahudi katika Ukingo wa Magharibi (aliwahi kuwa kiongozi wa baraza la Yesha, mwakilishi wa kundi la wakazi wa kiyahudi), ingawa alisema Israel haina madai yoyote dhidi ya Gaza (ambapo Israel ilipeleka majeshi yake kuwaondoa walowezi wa mwaka 2005). Zaidi ya wayahudi 600,000 wanaishi katika eneo la ukingo wa magharibi na mashariki ya Yerusalemu, ambapo karibu jumuiya yote ya kimataifa inadai kuwa wapo hapo kinyume na sheria , licha ya Israel kupinga madai hayo.

Hatima ya nani ana haki ya kuishi hapo inaendelea kuleta mgogoro mkubwa kati ya Israel na Palestina, ambapo wanataka kuwaondoa na kuufanya ukingo wa magharibi na Gaza kuwa huru na mashariki ya Yerusalemu kuwa mji mkuu.

Kuingilia kati, achilia mbali kusitisha, shughuli za makazi ni jambo linalopingwa vikali na Bwana Bennett, ambaye alimchukulia Netanyahu kutotoa kipaumbele juu ya suala hilo.

Bwana Bennett ni mzungumzaji mzuri wa kiingereza, na anaonekana mara kwa mara katika TV za kigeni, akiwa anatetea hatua ya Israel.

Aliwahi kupinga vikali, katika mjadala wa kituo cha runinga ya nyumbani aliwahi kumuonya mbunge wa Kiarabu wa Israeli kwa kusema Wayahudi hawana haki ya kukaa katika Ukingo wa Magharibi, akimwambia::

"Wakati mkiwa bado mnabembea kwenye miti, sisi tulikuwa na jimbo la wayahudi hapa."

Bwana Bennett alikataa suala la kuanzisha jimbo la pamoja la Palestina na Israel -jambo ambalo liliitwa kuwa suluhisho la mzozo wa serikali mbili kati ya Israeli na Palestina (suala ambalo amelihusisha katika kusitisha mapigano ) lilihamasishwa na jumuiya za kimataifa akiwemo rais wa Marekani, Joe Biden.

"Nikiwa bado nina nguvu ya udhibiti wa jambo hili, siwezi kuiachia ardhi ya Israel," alisema hivyo katika mahojiano mwezi Februari 2021. Aidha bwana Bennett anahamasisha kuimarisha Israel kuendelea kushikilia ukingo wa magharibi - eneo ambalo wananukuu katika biblia kwa jina la Judea na Samaria - kuwa ni lao.

Bwana Bennett amechukua hatua kali katika kutoa vitisho dhidi ya wanajeshi wa Palestina ( ambapo alisema kuwa anaunga mkono adhabu ya kifo. Suala hili halijawahi kufanyika nchini Israel ukiachilia mbali kesi ya Adolf Eichmann, kiongozi wa mauji ya halaiki katika eneo la Yerusalemu mwaka 1961 na alinyongwa mwaka uliofuata).

Alipinga makubaliano ya watawala wa Gaza wa Hamas ambao walimaliza mapigano mnamo 2018 na kulishutumu kundi hilo kwa kuua kwa ufanisi raia wake wengi waliouawa katika mashambulio ya angani ya Israeli yaliyotekelezwa kufuatia kurushwa kwa roketi kutoka Gaza katika mapigano mapya mnamo Mei 2021.

Mada ya majivuno ya Wayahudi na kujiamini kwa taifa hilo ni miongoni mwa mambo ambayo bwana Bennett, ambaye hujifunika kichwa kama waumini wa kiyahudi aliweka sahihi yake.

Katika kampeni za chama mwaka 2014 ,alilitaarifu gazeti la New York Times la mrengo wa kushoto la Israeli la Haaretz kwa kukosoa vitendo vya Israel katika mitandao ya kijamii, kwa kuonesha video inayojirudia kusema samahani kabla ya kujitambulisha mwenyewe na kutangaza kuwa kuanzia sasa wataanza kuacha kuomba radhi.

Kuongezeka kwa mvutano wa kisiasa kwa Bennett kumepelekea kuonesha tofauti mapema kati ya jeshi na biashara.

Alikuwa anawahudumia katika makundi mawili muhimu ya jeshi la Israeli wakati wa huduma yake katika vita kabla hajaanzisha makampuni ya teknolojia ya kiwango cha juu, hivyo kumfanya kuwa milionea kutokana na shughuli zake.

Akizungumzia suala la utajiri katika mahojiano ya mwaka 2014, alisema: "sili nyama vipande 17 na sina ndege binafsi au meli yangu mwenyewe.

Hii inanifanya kuniletea uhuru wa kufanya ninachotaka."