Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Namna ambavyo waasi wa Uganda walikuwa washirika wa IS nchini DRC
Uasi wa jihadi uliokuwa umeibuka unaweza kuongeza nguvu eneo la mashariki mwa DR Congo, ambalo limekuwa kituo cha shughuli za waasi kwa miongo mitatu iliyopita.
Vurugu katika eneo lenye utajiri wa madini zimesababisha sheria za kijeshi na tamko la hali ya kuzingirwa katika majimbo ya Ituri na Kivu Kaskazini.
Makundi mengi yanayohusika na mauaji ya maelfu ya raia na maelfu zaidi kuhama makazi yao yana asili katika nchi jirani za Rwanda, Burundi na Uganda.
Miongoni mwa makundi yenye vurugu zaidi ni kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Allied Democratic Forces (ADF) wa Uganda ambalo shughuli zao zinazidi kudaiwa chini ya lufanyika chini ya mwamvuli wa kundi la Islamic State (IS).
Shughuli za kundi hilo la jihadi zinazopamba moto nchini DR Congo ni sehemu ya mwelekeo mpana kuelekea Afrika kufuatia kuporomoka kwa kile kinachoitwa ukhalifa mnamo 2019.
Uasi huo unatishia kutokomeza juhudi za jeshi la DR Congo (FARDC) na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa (Monusco) kuleta utulivu katika eneo la mashariki na inaweza kusababisha mapigano ya kimadhehebu katika eneo hilo.
Msimamo mkali wa ADF
ADF hapo awali ilijulikana kama Kikosi cha Allied Democratic Forces-National Army for the Liberation of Uganda (ADF-NALU). Iliundwa kaskazini mwa Uganda miaka ya 1990 na maafisa wa zamani wa kijeshi watiifu kwa dikteta wa zamani Idi Amin na ina wanachama wengi wa Kiislamu.
ADF-NALU ilichukua silaha dhidi ya kiongozi wa muda mrefu wa Uganda, Yoweri Museveni. Ilishindwa na jeshi la Uganda na kuondoshwa kisha kukimbilia katika eneo la Beni, Jimbo la Kivu Kaskazini nchini DRC mnamo mwaka 2001.
Monusco inakadiria kuwa kunaweza kuwa na wapiganaji zaidi ya 1,000 wa ADF chini ya uongozi wa Musa Seka Baluku. Anatoka Mkoa wa Kasese huko Uganda na alishika uongozi wa kikundi hicho baada ya kiongozi wake mwanzilishi, Jamil Mukulu, kutiwa mbaroni nchini Tanzania mnamo 2015.
Mnamo mwaka 2016, Baluku aliripotiwa kuahidi utii kwa IS.
Hatahivyo, IS ilitambua mara ya kwanza shughuli zake huko DR Congo mnamo 18 Aprili 2019, wakati ilipodai kufanya shambulio dhidi ya maeneo ya jeshi kaskazini mashariki mwa nchi, karibu na mpaka wa Uganda.
Wakati kukiwa kuna dalili kwamba IS imechagua ADF, IS yenyewe bado haijatoa tangazo lolote juu ya ahadi ya uaminifu kutoka kwa kikundi au kiongozi wake. Kwa kweli, IS haijawahi kuitaja hadharani ADF kwa jina katika propaganda zake.
Mwezi Septemba mwaka 2020, Baluku alitangaza kwamba ADF "haipo tena"."Kwa sasa, sisi ni mkoa, Jimbo la Afrika ya Kati, ambalo ni moja ya majimbo mengi ambayo yanaunda Jimbo la Kiislamu, ambalo liko chini ya khalifa na kiongozi wa Waislamu wote ... Abu Ibrahim al-Hashimi al-Qurashi, " alisema.
ADF iliwekewa vikwazo na Hazina ya Marekani na kuwekwa kwenye orodha ya shirika la kigaidi na Wizara ya mambo ya nje ya Marekani mwezi Machi.
Mgongano kati ya malengo ya ADF na madai ya IS
Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR), ADF imewauwa raia wapatao 200 na kusababisha karibu wengine 40,000 kuhama makazi yao huko Beni tangu Januari mwaka 2021. Kundi hilo la waasi pia linalenga wanajeshi kutoka FARDC na Monusco.
Tangu IS ilipoibuka katika taifa la Afrika ya kati mnamo 2019, mashambulio yaliyodaiwa na kundi la jihadi na kuhusishwa na ADF kwenye vyombo vya habari vya ndani yameongezeka na kuwa mabaya zaidi.
Madai ya shambulio ya ISCAP yamefanyika sana katika eneo la Beni la Kivu kaskazini, ambalo ni ngome ya ADF, na mara kwa mara huingia katika Jimbo la Ituri ambalo shughuli za ADF zimeripotiwa pia.
Kwa mujibu wa data iliyokusanywa na BBC Monitoring kutoka kwa vyanzo vya vyombo vya habari vya IS, kikundi hicho kilidai mashambulio 113 kati ya Aprili 18 mwaka 2019 na Aprili 30 mwaka 2021, na 465 walijeruhiwa. Mwezi uliomwaga damu zaidi ilikuwa Desemba 2020, wakati IS ilidai kutekeleza mashambulizi 13 na majeruhi 70.
Machi 2020 ilishuhudia shambulio moja tu lakini ilikuwa moja ya mashambulio makubwa, na karibu askari 20 waliripotiwa kuuawa katika shambulio la mjini Beni.
Hadi wakati huo, IS ilikuwa ikidai karibu majeruhi 1.4 kwa kila shambulio nchini DR Congo. Katika miezi iliyofuata, takwimu hiyo iliongezeka hadi 4.5 kwa shambulio.
Mashambulio mengi (98) ni ya vikosi vya jeshi na vikosi kadhaa vya UN. Lakini mashambulizi mabaya zaidi hutokea wakati raia wa Kikristo wanalengwa. Kiwango cha wastani cha majeruhi kwa mashambulizi haya ni 9.7.
Mnamo mwezi Mei tarehe 17, 2020, IS ilidai kuwajeruhi watu karibu 30 katika mashambulio kwenye vijiji vitatu vya Beni. Shambulio kama hilo katika eneo la karibu mnamo Oktoba 28 lilisemekana kuua watu 19.
Hatahivyo, shambulio muhimu zaidi la IS hadi sasa linaonekana kuwa kuvunja jela mwezi Oktoba 2020 huko Beni ambalo lilisababisha kutoroka kwa wafungwa zaidi ya 1,000. Vyombo vya habari nchini DR Congo viliripoti tukio hilo na kuhusishwa na ADF.
Pia ni muhimu kuzingatia kwamba takwimu hizi za majeruhi zinategemea madai ya ISCAP mwenyewe, na vikundi vya jihadi vinajulikana wakati mwingine vinashawishi athari za mashambulio yao.
Propaganda za IS zinachochea mvutano wa kikabila
Mzozo mashariki mwa DRC umegusa mara nyingi mvutano wa kikabila. Hatahivyo, mashambulizi ya ADF na propaganda za IS zinaweza mizozo ya kidini zaidi.
Kuna idadi kubwa ya madhehebu ya Kikatoliki DRC, na kanisa ni kiungo muhimu cha kijamii na kisiasa nchini humo. Waislamu wanajumuisha karibu 10% ya idadi ya watu wote.
Beni, ambapo ADF inafanya operesheni zake zaidi, ina idadi ya watu karibu 200,000. Jamii ya Waislamu wa eneo hilo imekuwa ikikemea sana shughuli za kundi la waasi, ambalo linashutumu kuchafua dini. Mwezi Mei, maulamaa wawili mashuhuri wa Kiislamu wanaojulikana kuwa wanalikosoa kundi la ADF waliuawa kwa kupigwa risasi huko mjini Beni.
Kundi la waasi pia limehusishwa na mashambulio dhidi ya Wakatoliki. Mwezi Oktoba mwaka 2012, iliwateka nyara mapadre watatu Wakatoliki kutoka katika nyumba ya watawa katika eneo la Beni huko Mbau. Mpaka sasa hawajulikani walipo
Katika propaganda zake, IS imekuwa ikiwachagua Wakristo na kukejeli serikali ya Congo kwa "kutofaulu" kwao kuwalinda kutokana na mashambulio yake.
Uchochezi kama huo ni tabia ya IS, ambayo mara nyingi inatafuta kuzidisha mivutano ili kuimarisha sifa zao kama mtetezi wa Waislamu wa kawaida dhidi ya "dhuluma". Kihistoria ADF ilidai kuteswa kwa Waislamu nchini Uganda.
Shughuli zinazohusishwa na ADF na vikundi vingine vya waasi zinaripotiwa sana na vyombo vya habari vya ndani vilivyo katika mji wa Goma Kivu Kaskazini na kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii yaliyo katika mji mkuu wa DR Congo, Kinshasa na nje ya nchi hiyo. Majukwaa haya yanatoa ripoti za kweli ambazo zina shuhuda za mashahidi, vikundi vya kijamii na maafisa wa serikali.
ADF haijaonekana kuendesha vyombo vya habari au kudai kuhusika na mashambulio.
Hatahivyo, IS inatoa madai na propaganda kwa DR Congo kupitia vyombo vyake vya habari haswa kwenye Telegram ya programu ya ujumbe, na kwenye jukwaa la RocketChat.
ISCAP hadi sasa imetoa video moja tu ya kipropaganda iliyoonesha wanamgambo wake huko DR Congo. Video ya Julai 2019 ilionesha mwanamgambo aliyejificha akiwahutubia wengine zaidi ya dazeni, pamoja na watoto, kwa Kiswahili, katika eneo lisilojulikana la misitu.
Mwezi Machi, ISCAP ilitoa picha zinazodaiwa kuwaonesha wanamgambo wake wakizurura katika mitaa ya kijiji katika Mkoa wa Ituri kufuatia shambulio dhidi ya jeshi. Lakini picha kama hizo ni nadra na zinaonesha kwamba IS bado imekuwa nguvu kubwa nchini DR Congo.
Mnamo Mei 13, IS ilitoa picha za wanamgambo wake nchini DR Congo wakisherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr inayoashiria kumalizika kwa Ramadhani. Picha hizo zilionesha kikundi cha wanaume wakifanya maombi ya Eid katika eneo la msitu.
Picha nyingine ziliwaonesha wakitayarisha chakula, kula na kukumbatiana. Baadhi ya wanamgambo hao walikuwa wamefunikwa nyuso zao , wakati nyuso za wengine zilikuwa zikionekana. Watoto na wasichana pia walioneshwa katika baadhi ya picha.
Ghasia za waasi mashariki mwa Congo zimekua kwa kiasi kikubwa kutokana na ukosefu wa taasisi za serikali zenye nguvu na Jeshi kutoaminika.
ISCAP itatumia vurugu ili kupanua shughuli zao katika nchi jirani. Ndani ya mwaka mmoja wa kuundwa kwake, ISCAP ilionekana kuingia kusini mwa Tanzania karibu na mpaka na Msumbiji.
Mnamo Oktoba 2020, IS ilidai shambulio lake la kwanza katika Mkoa wa Mtwara nchini Tanzania ambapo inadaiwa iliwaua wanajeshi 20 wa Tanzania.
ADF, kwa upande wake, inaweza kutumia ushirika wae na IS kwa kuongezea zaidi na kuongeza nguvu.