Mzozo kati ya Israel na Palestina: Kwanini mji wa Jerusalem ni mji mtakatifu kwa Waislamu, Wakristo na Wayahudi

Aliyekuwa rais wa Marekani Donald alitangaza kwamba Marekani inatambua rasmi mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Punde tu baada ya tangazo hilo , kumekuwa na madai kwamba huenda hatua hiyo ya Marekani ndio 'busu la mwisho' la mchakato wa amani katika eneo hilo.

Tamko hilo liliifanya Marekani kuwa taifa la kwanza kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel tangu kuzaliwa kwa taifa la Israel 1948.

Wakati huohuo rais Trump aliagiza kuhamishwa kwa ubalozi wake kutoka mjini Tel Aviv hadi Jerusalem na kusisitiza kwamba uamuzi wake haumaanishi kujiondoa katika suluhu ya kudumu ya amani katika Israel na Wapalestina.

Baadhi ya maeneo matakatifu ya kidini duniani yapo katika mji wa zamani wa Jerusalem : Dome of the Rock, Msikiti wa Al Aqsa, hekalu la Mlimani na Ukuta wa magharibi wa dini ya wayahudi na kaburi takatifu wa dini ya Wakristo.

Na pia unatambulika kuwa mji mtakatifu zaidi wa Wayahudi na Wakristo na ni mji mkuu mtakatifu wa Waislamu.

Historia yenye mgogoro

Ukijulikana kiHebrew kama Yerushalayim na kiarabu kama Al Quds, ni mmoja wa miji ya zamani zaidi duniani.

Umetekwa, kuharibiwa na kujengwa kwa mara nyengine ,na kila safu ya dunia kipande tofauti cha historia yake hubainika.

Ijapokuwa mji huo umezongwa na hadithi za tofauti na mizozo kati ya watu wa dini tofauti, huunganishwa na heshima ya mji huo mtakatifu.

Katikati yake ni mji wa zamani , uliosheheni historia unaoelezea majirani zake wane : Wakristo, Waislamu Wayahudi na Warmenia.

Mji huo umezungukwa na ukuta wenye mawe na ni nyumbani kwa baadhi ya maeneo takatifu zaidi duniani.

Kila eneo jirani linawakilisha idadi yake ya watu. Wakristo wana maeneo mawili, kwasababu Warmenia pia ni Wakristo na ujirani wao ukiwa mdogo zaidi kati ya maeneo hayo manne, ni moja ya kituo cha zamani zaidi cha Armenia duniani. Ni wa aina yake kwasababu jamii hiyo imehifadhi utamaduni wake ndani ya hekalu.

1- Kanisa

Ndani yam ji huo wa zamani ni kanisa la mtakatifu Sepulcher, mojawapo ya maeneo takatifu ya Wakristo duniani. Lipo katika eneo ambalo historia yake inamuhusisha Yesu Krsito , kifo chake , kusulubiwa kwake na kufufuka kwake.

Kulingana na tamaduni za Wakristo, Yesu alisul hapo katika Eneo la Gogotha ama Mlima Calvary, na kaburi lake lipo hapo na ndipo eneo alilofufuka.

Kanisa hilo linasimamiwa na wawakilishi wa makanisa tofauti ya Kikristo , hususan Kanisa la Orthodox la Ugiriki, kanisa la Katholiki la Franciscan Friars na kanisa la Armenia Patriarch.

Lakini kanisa la Ethiopia la Coptic na kanisa la Syria pia yanahusishwa.

Ni eneo moja linalotembelewa sana na mamilioni ya mahujaji Wakristo kote duniani ambao hutembelea kaburi ya Yesu na kuomba katika eneo hilo.

2- Msikiti

Msikiti wa Al Aqsa ndio mkubwa kati ya maeneo matakatifu yaliopo katika mji huo katika eneo linalojulikana kama Haram al Sharif.

Msikiti huo ndio eneo la tatu takatifu kwa ukubwa na husimamiwa na ufadjhili wa fedha unaojulikana kama Wakfu.

Waislamu wanaamini kwamba mtume Muhammad alisafiri kuelekea eneo hilo kutoka Mecca wakati wa safari ya usiku na kuombea roho za mitume yote.

Hatua chache kidogo, The Dome of The Rock linamiliki jiwe ambalo mtume Muhammad alienda mbinguni.

Waislamu hutembelea eneo hilo takatifu kila mwaka , lakini kila Ijumaa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramdhan, mamia ya maelfu ya Waislamu huenda katika eneo hilo kufanya ibada.

3- Ukuta

Eneo hilo linamiliki Kotel- ama ukuta unaolia, mojawapo ya milima iliosalia ya mlima Moria.

Ndani ya hekalu hilo ni eneo takatifu la matakatifu ya Wayahudi.

Wayahudi wanaamini kwamba eneo hilo ndio eneo la jiwe la msingi ambapo dunia iliundwa na ni eneo ambalo mtume Abraham alitaka kumchinja mwanawe Isaac.

Wayahudi wengi wanaamini kwamba The Dome of The Rock ndio eneo la maeneo yote matakatifu.

Hii leo ukuta huo unaolia ndio ulio karibu zaidi kwa Wayahudi kufanya ibada.

Unaongozwa na Rabbi na mamilioni ya wageni hutembelea eneo hilo kila mwaka.