Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Bahati au Tamaa? Jinsi watu hawa walivyokosa kupewa kiasi kikubwa cha fedha na wengine wakaachwa na majuto
Kupata pesa nyingi ama utajiri wa haraka huwa matamanio ya watu wengi . Walakini kunao watu ambao kiasi kikubwa cha fedha nusura kiingie mifukoni mwao lakini hawakuzipata kwa kuzikataa wakitaka kupewa zaidi au bahati haikutengenea.
Hii hapa orodha yawatu ambao wamezinusia pesa hizo lakini hazikuwafikia .Aliyetukumbusha hili maajuzi ni raia wa Afrika Kusini Nkosana Makate ambaye alivumbua huduma ya 'please call me' iliyotumiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom .
Nkosana alidai mwaka wa 2016 kwamba uvumbuzi wake uliipa Vodacom dola bilioni 5 na yeye anataka asilimia 15 ya fedha hizo .
Nkosana Makate (Shilingi Milioni 354)
Nkosana Makate, mwanzilishi wa huduma ya simu, 'Tafadhali Nipigie simu' anadai jumla ya Sh75 bilioni kama fidia kutoka kwa kampuni ya Vodacom.
Kampuni ya Vodacom mwanzoni ilikuwa imekubali kulipa Makate Sh354 milioni ambayo alikataa. Mzozo wa kampuni hiyo na mvumbuzi Makate upo kortini .
Huduma ya 'Tafadhali Nipigie' ililetwa sokoni kwa mara ya kwanza mnamo 2001. Hii ni huduma ya sms ya bure ambayo inaruhusu wateja kutuma ujumbe kwa mtumiaji mwingine anayeomba apigiwe simu.
Mvutano kati ya Makate na Vodacom umekuwa ukifanyika kwa zaidi ya miaka 20 sasa .
Korti imetakiwa kutathini upya fidia aliyopewa kama ilivyohesabiwa na mtendaji mkuu wa Vodacom Shameel Joosub.
Hii ilifuata uamuzi wa Mahakama ya Katiba mnamo 2016 ambapo Vodacom iliamriwa kufanya mazungumzo na Makate ili kupata fidia ya haki.
Wakili Gilbert Marcus, ambaye alianza vita vya kisheria kwa niaba ya Makate, alisema hakutumia neno "usaliti" kwa wepesi , lakini hii ilikuwa hivyo kwa sababu mteja wake alisalitiwa . Alisema kuwa wakati Vodacom ilikuwa ikipata faida kubwa kutoka kwa uvumbuzi huo na "ilikuwa ikitabasamu hadi benki", hawakuacha tabasamu katika uso wa Makate ".
Andy Green-£1.7m
Mnamo mwaka wa 2020 mwanamme ambaye akaunti yake iliwekwa £1.7m aliwasilisha kesi kortini nchini Uingereza baada ya fedha hizo kuondolwa .
Andy Green, 53, kutoka Lincolnshire alifiriki kwamba ameshinda kitita kizito cha fedha mwaka wa 2018 baada ya kushiriki mchezo wa kubasiri mtandaoni .Lakini iliyompa fedha hizo Betfred ,ilimarifu kwamba kulikuwa na hitilifau ya kimtambo ambayo ilizihamisha fedha hizo kwa akaunti yake.
Lakini mawakili wa Bw Green wanasema hakupewa thibitisho la shida hiyo.
Baada ya usiku mrefu kucheza Betfred Frankie Dettori Magic Seven Blackjack mnamo Januari 2018, akaunti ya Green ilipewa $ 1,722,923.54 ambayo alijaribu kutoa - lakini ombi hilo lilikataliwa.
Baada ya kuweka dau zingine na ushindi wake alichukua picha ya skrini kudhibitisha kilichotokea.
Kama ishara ya "nia njema" kampuni hiyo ilikuwa tayari kumlipa pauni 30,000, lakini Bwana Green angelazimika kukubali kutozungumza suala hilo tena.
Bwana Green alikataa na kampuni hiyo ikaongeza ofa yake hadi Pauni 60,000, ambayo pia alikataa.
Zaidi ya miaka miwili baadaye ameenda mahakamani kuishtaki Betfred na kampuni yake kuu , Petfre yenye makao yake Gibraltar kwa pauni milioni 2, pamoja na riba ambayo angepata kutoka kwa ushindi.
Pauline McKee (£27.6m)
Mnamo mwaka wa 2015 Mwanamke mwenye umri wa miaka 90 kutoka Illinois ambaye alidhani ameshinda $ 41.8m (£ 27.6m) kwa mashine ya video ya senti, alinyimwa bonasi hiyo baada ya kupoteza kesi kortini.
Bibi Pauline McKee alikuwa akicheza mchezo wa Miss Kitty kwenye kasino
Lakini ujumbe ulionekana kwenye skrini ukisema pia ameshinda bonasi yenye thamani ya $ 41,797,550.16.
Kasino ilikataa kulipa, ikisema tuzo hiyo ilikuwa hitilafu ya kompyuta.
Bi McKee, ambaye ana wajukuu 13, alishtaki kasino lakini Mahakama Kuu ya Iowa mwishowe ilitupa kesi yake.
"Nilikuwa na mashaka yangu tangu mwanzo, kwa sababu hizo ni pesa nyingi kwa mashine ya senti," aliiambia Chicago Tribune.
Nilikuwa na matumaini ya kuwasaidia watoto wangu kifedha, lakini haikukusudiwa kuwa hivyo. "
'Hitilafu'
Kasino ilisema kwamba sheria za skrini zilionyesha wazi kwamba "hitilafu yoyote huondoa malipo yote na uchezaji".
Wakati wa mzozo, Tume ya Mashindano na Michezo ya Kubahatisha ya Iowa (IRGC) ililinda mashine hiyo na kufanya uchunguzi, ikipeleka vifaa na programu hiyo kwa maabara huru ya upimaji.
Wachunguzi waligundua kuwa programu hiyo ilikuwa imewekwa kuruhusu bonasi ya hadi $ 10,000, lakini hawakuweza kujua jinsi ujumbe wa ziada wa mamilioni ulivyotokea.
Mtengenezaji wa mashine hiyo, Aristocrat Technologies, alisema alikuwa anajua aina hii ya makosa kwenye onyesho na alipendekeza "uharibifu wa sehemu ya mashine kwa muda unaweza kuongeza uwezekano wa tukio hili adimu".
Iwapo hatima kama hiyo itamkumba mwafrika kusini Makate katika harakati zake za kulipwa kiasi kikubwa cha fedha ni jambo litakalotegemea uamuzi wa mahakama na muda .Wengi katika ambao wanazitamani pesa alizoahidiwa na Vodacom bila shaka wana uchu wa kumpa ushauri azikubali lakini kwa sababu yeye ndiye mvumbuzi wa huduma hiyo anaijua vyema thamani ya uvumbuzi wake .