Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Nigeria: Jinsi mpango ulioungwa mkono na Gordon Brown na Mashirika ya UN kuwalinda wanafunzi Nigeria ulivyofeli
Utekaji nyara wa mamia ya wasichana wa shule za Nigeria kutoka Chibok miaka saba iliyopita ulisababisha kuzinduliwa kwa mpango wa mamilioni ya dola, ulioungwa mkono na waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, ili kuimarisha usalama shuleni - lakini mpango huo umeshindwa kuzuia utekaji nyara na kuwalinda watoto.
Ngozi Okonjo-Iweala, waziri wa fedha wa Nigeria wakati huo na sasa mkuu wa Shirika la Biashara Ulimwenguni, alipokelewa na umati wa viongozi wa jamii na wazazi ambao binti zao walikuwa wametekwa nyara.
Alikuwa Chibok kuweka matofali ya kwanza katika mradi wa kukarabati Shule ya Sekondari ya Serikali ambayo iliharibiwa na wapiganaji wa Boko Haram usiku huo mbaya wa tarehe 14 Aprili 2014.
Kulikuwa na hotuba fupi, kisha akaweka matofali machache na simiti na kisha akaondoka kwa kishindo na kuwaachia vumbi waliokuwepoo hapo kama tu alivyoingia kwa njia hiyo kutumia helikopta .
Pamoja na kazi iliyofanyika kulikuwa na salamu kwa ajili ya picha kadhaa, kisha alikuwa amekwenda kwenye shughuli nyingine
kuwepo kwa Bi Okonjo-Iweala kulikuwa na sehemu ya jibu la kimataifa kufuatia kutekwa nyara kwa wasichana 276 na wapiganaji wa Kiislam huko Chibok mnamo 2014.
Maoni ya ulimwengu na msimamo wake yalipigwa jeki na hashtat ya twitter #BringBackOurGirls - na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Gordon Brown, aliongoza mpango wa $ 30m (karibu £ 22m) wa Safe Schools Initiative (SSI) - pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa , serikali ya Nigeria na viongozi wa kibiashara wa kampuni za kibinafsi
Shule mia tano zingelindwa: kungekuwa na madarasa mapya; kungekuwa na ua kuzizingira shule hizo ; kungekuwa na walinzi wenye silaha.
"Lengo la mpango huo ni kuhakikisha kuwa vijana hawawi salama tu wakienda shule lakini pia kutoa mazingira mazuri ya kusoma ,ukuaji na maendeleo bila hofu," Bwana Brown alisema mnamo Mei 2014.
Yote yalisikika kuwa mazuri sana, lakini miaka saba baadaye , shule 500 hazijalindwa na madarasa hayajajengwa.
Shule za Chibok bado zimefungwa
Kulikuwa na mafanikio kadhaa ikiwa ni pamoja na utoaji wa madarasa ya muda na vifaa vya kujifunzia kwa watoto katika kambi za watu walioachwa bila makao , lakini mpango huo ulikomeshwa chini ya miaka miwili baada ya uzinduzi wa kina katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja.
Matukio ya hivi karibuni ya utekaji nyara shuleni kaskazini na kaskazini magharibi mwa Nigeria yanaonyesha kushindwa kwa serikali kutunga sera ambazo zinaweza kuboresha usalama shuleni.
Wasichana 112 wa shule ya Chibok wlaiotekwa nyara bado hawajapatikana na shule yao, kati ya 30 zilizochaguliwa kwa awamu ya majaribio ya mifano salama ya shule, haijawahi kujengwa kikamilifu.
Ingawa kuna majengo ya muda yalioanzishwa baada ya ziara ya Bi Okonjo-Iweala, viongozi wa jamii wanasema kuwa hazikujengwa vizuri.
"lilijengwa kwa muundo duni, kila upepo uliovuma uliharibu sehemu ya jengo. Iiliendelea kuanguka mara kwa mara na hadi leo halijatumika," Allan Manase, msemaji wa jamii ya Chibok, aliambia BBC.
Hata hivyo madarasa katika shule hiyo hivi sasa yanakarabatiwa na jeshi la Nigeria, lililofadhiliwa na serikali ya jimbo la Borno baada ya Gavana Babagana Zulum kuzuru shule hiyo mnamo Novemba na kushtushwa na kile alichokiona.
Usalama ni jambo la kina zaidi ya mapambo ya nje
Muundo wa shule salama , uliyoundwa na iliyokuwa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (Dfid), ililenga kutoa mpango wa kulinda shule, kuzuia mashambulizi, na kuendelea na masomo kwa wanafunzi katika Jimbo ambalo limeharibiwa na shughuli za Boko Haram.
Lakini hakuna shule kati ya 30 zilizochaguliwa kwa awamu ya majaribio iliyoboreshwa miundombinu, BBC iligundua.
Kulikuwa pia na maswali juu iwapo uwa la waya na milango inaweza kutoa kinga yoyote dhidi ya vikundi kama Boko Haram, ambao wapiganaji wao wana silaha kama roketi na magari maalum ya kijeshi. Shule ya Chibok ilikuwa na ua wakati iliposhambuliwa.
"Ua lingeweza kuzuia mashambulio kwa shule, lakini hakuna uhakika wa hilo," anasema mtaalam wa usalama Aminu Bala.
"Usalama wa shule ni jambo zaidi ya muundo wa mapambo, ikiwa kuna ukosefu wa usalama kwa ujumla basi ni vigumu kulinda kila mahali, haswa maeneo yaliyo na udhaifu kama shule zilizo na maelfu ya ua hizo za kuta ," anasema.
Ofisi ya Mambo ya nje ya Uingereza, Jumuiya ya Madola na Maendeleo (FCDO), ambayo imejumuisha Dfid, iliiambia BBC kwamba jukumu lake lilikuwa kutoa "ushauri wa wataalam juu ya njia za kuimairisha usalama shuleni ", pamoja na "maendeleo ya miongozo ya shule salama".
Lakini iliongeza kuwa haikuwajibika moja kwa moja kutekeleza miradi kwani hii ilikuwa chini ya kikosi cha uhandisi cha jeshi la Nigeria.
Jeshi la Nigeria halikujibu maswali ya BBC kuhusu jinsi mradi huo ulivyoshughulikiwa
Ucheleweshaji wa Serikali
Ofisi ya Bw Brown, ambaye bado ni mjumbe maalum wa UN kuhusu elimu, iliiambia BBC katika taarifa kwamba "kufuatia utekaji nyara wa hivi karibuni katika mwaka uliopita, [alifanya] mkutano na waziri wa fedha wa Nigeria mnamo 2020 kusaidia kuhimiza Mpango mpya wa Shule Salama'
Ofisi yake haikujibu maswali kuhusu jinsi $ 30m za awali zilivyotumika , ikisema kwamba "fedha zote zilielekezwa kupitia na kusimamiwa na serikali ya Nigeria".
Mradi wa SSI uliporomoka mnamo 2016, mwaka mmoja baada ya mabadiliko ya serikali nchini Nigeria.
Goodluck Jonathan ambaye aikuwa uongozini wakati wasichana hao walipotekwa nyara na SSI kuzinduliwa ,alishindwa katika uchaguzi mikuu na rais wa Muhammadu Buhari.
Mashirika ya UN na wafadhili wa kimataifa walisema mikutano ya mara kwa mara na mabadiliko ya sera za Bw Buhari yalikwamisha shughuli za mpango huo na kusababisha kuondoka kwao.
Katika ripoti yake, ofisi ya kigeni ya Uingereza ililaumu serikali ya Buhari kwa ucheleweshaji wa kutekeleza SSI, na maamuzi yakiahirishwa kwa sababu ya mikutano ya mara kwa mara ya kamati za uongozi.