Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wasichana wa Chibok walibadilishwa na makamanda
Mtandao wa habari wa Sahara ambao ulikuwa wa kwanza kuripoti kuhusu kuachiliwa kwa wasichana wa Chibok umechapisha ujumbe katika mtandao wake wa Twitter kuhusu ubadilishanaji wa wafungwa uliosababisha kuachiliwa kwao.
Maelezo bado hayajathibitishwa ,lakini mtandao huo unasema kuwa wasichana 18 wana watoto na kwamba walibadilishwa na makamanda wanne wa Boko haram .
Pia mtandao huo umeripoti kwamba wasichana hao wanaelekea mji mkuu wa Abuja.