Kwanini 'jeans' zilizochanika magotini na mapajani zazuwa gumzo India

Bollywood actress Priyanka Chopra in a pair of ripped jeans

Chanzo cha picha, Gotham

Maelezo ya picha, Jeans zilizochanika ni maarufu sana kwa nyota wa Bollywood kama vile Priyanka Chopra Jonas
Muda wa kusoma: Dakika 2

Denimu - mavazi ya vitambaa vyenye nyuzi za asili kama vile jeans zilizochanika kwenye magoti na mapajani zimeanza tena kuwa gumzo la utovu wa nidhamu kwa vijana.

Wa hivi karibuni kabisa kukasirishwa na vazi hilo ni waziri Tirath Singh Rawat wa kaskazini mwa India jimbo la Uttarakhand aliyeteuliwa hivi karibuni.

Mapema wiki hii, waziri huyo alilaumu "jeans zilizochanika" kama moja ya kile kinachosumbua vijana.

Akizungumza katika warsha iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Kulinda Haki za Watoto, Bwana Rawat alimkosoa mwanamke ambaye hakutajwa aliyekutana naye ndani ya ndege.

Alisema, mwanamke huyo alikuwa akisafiri na watoto wake wawili na alikuwa amevaa viatu aina ya "boots, suruali ya jeans iliyochanika kwenye magoti na bangili kadhaa mkononi".

"Unaendesha shirika lisilokuwa la kiserikali, umevaa jeans iliyochanika kwenye magoti, unatembea na watoto, utawafunza maadili gani?" waziri alimuuliza.

Denim is the choice of clothing for many young Indians

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Fasheni ya denimu ni aina ya vazi linalovaliwa sana na vijana India

Waziri huyo alikaripia raia wa India kwa "kutembea uchi" na kudai kuwa "wakati watu nchini India wanavaa jeans zilizochanika, wale walio nje ya nchi wanafunika miili yao na kufanya yoga".

Matamshi ya Bwana Rawat yamesababisha shutuma kali nchini India.

Chama cha upinzani cha Congress party kilitoa taarifa na kumtaka "aombe msamaha kwa wanawake wote India" - au ajiuzulu.

Alhamisi, kiongozi mwandamizi Priyanka Gandhi Vadra alishirikisha wengine picha za Waziri Mkuu Modi na mmoja wa mawaziri wenzake "wakionesha magoti yao":

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Presentational white space

Mkuu wa tume ya Delhi kwa wanawake Swati Maliwal aliandika ujumbe kwenye Twitter akimshutumu Bwana Rawat kwa "kuendeleza chuki dhidi ya wanawake":

Presentational white space
Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Presentational white space

Katika ujumbe wake kwenye Twitter, Maliwal alisema kuna tatizo sio tu vile alivyosema Bwana Rawat - lakini pia alivyokubali "kudharau wanawake".

Matamshi yake yamewafanya maelfu ya wanawake wa India katika mtandao wa Twitter na baadhi ya wanaume kuweka picha zao wakiwa wamevaa jeans zilizochanika. Na hashtag za #RippedJeansTwitter na #RippedJeans zikisambaa mtandaoni kwa muda.

Presentational white space
Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 3

Presentational white space
Ruka X ujumbe, 4

Mwisho wa X ujumbe, 4

Presentational white space
Presentational white space
Ruka X ujumbe, 5

Mwisho wa X ujumbe, 5

Presentational white space

Ijumaa, Bwana Rawat aliomba msamaha kwa matamshi yake kwa aliowakera. Alisema nia haikuwa kuwadharau na kuwa kila mmoja yuko huru kuvaa anachotaka.

Presentational white space