Virusi vya Corona: Muungano wa Afrika kupokea dozi milioni 300 za chanjo ya Urusi

Chanjo ya Urusi inatarajiwa kupatikana kwa kipindi cha miezi 12 kuazia mwezi Mei 2021,

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Chanjo ya Urusi inatarajiwa kupatikana kwa kipindi cha miezi 12 kuazia mwezi Mei 2021,

Kikosi kazi cha Muungano wa Afrika (AU) kimesema kuwa Urusi imetoa dozi milioni 300 za chanjo yake ya Sputnik V COVID-19 pamoja na msaada wa kifedha kwa nchi zinazotaka kupata chanjo hiyo.

Chanjo ya Urusi inatarajiwa kupatikana kwa kipindi cha miezi 12 kuazia mwezi Mei 2021, AU imesema katika taarifa yake.

Mfuko wa Urusi wa uwekezaji wa moja kwa moja (RDIF), ambao unahusika na utafutaji wa masoko ya nje, umesema usambaziji wa chanjo hiyo unaweza kuanza mwezi Mei, zaidi ni kuanzia mwezi Juni.

Nchi 55 wanachama wa Muungano wa Afrika zinatumai kushuhudia 60% ya wakazi wake bilioni 1.3 wanachanjwa kwa kipindi cha trakriban miaka mitatu ijayo.

Lakini wakati mataifa tajiri zaidi yakiendelea vyema na kampeni ya chanjo, ni nchi chache tu za Afrika ambazo zimeanza mipango ya utoaji wa chanjo kwa watu wake.

Sputnik V ndio chanjo inayoongoza katika udhibiti wa Covid-19 nchini Urusi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sputnik V ndio chanjo inayoongoza katika udhibiti wa Covid-19 nchini Urusi

"Tunashukuru tumepokea chanjo za Sputnik V kutoka Shirikisho la Urusi na tunajivunia saana kuzitoa ... kwa ajili ya nchi wanachama wetu," John Nkengasong, mkurugenzi wa taasisi ya udhibiti wa magonjwa la AU, alisema katika taarifa.

"Ushirikiano wa sekta binafsi wa aina hii ni muhimu katika juhudi za kumaliza janga la Covid-19," Nkengasong aliongeza.

Awali AU ilisema iliweza kupata dozi milioni 270 za AstraZeneca, Pfizer na Johnson & Johnson kwa ajili ya usambazaji mwaka huu.

Ijumaa kikosi kazi cha chanjo kimesama dozi zote milioni 270 "zimechukuliwa kwa ajili ya kukamilisha awamu ya kwanza ya chanjo".

Urusi imenadi chanjo yake ya Sputnik V kote duniani. Imeweza kusaini mikataba na makampuni ya utengenezaji wa chanjo hiyo na makampuni ya India, Korea Kusini na Brazil, na imeahidi kutoa mamilioni ya dozi kwa mataifa mengine ikiwa ni pamoja na Venezuela na Hungary.

Ikiwa msaada wa chanjo hiyo utatolewa yote kwa AU, utakuwa ni miongoni ni miongoni mwa mikataba mikubwa ya chanjo ya nje kusainiwa na Urusi.

Huku Moscow ikifanya mikataba ya aina hiyo kuonesha mchango wake katika kukabiliana na janga la corona, mauzo ya nje ya chanjo yameibua hofu ndani ya Urusi, ambako wanahangaika na mkakati wa kitaifa wa utoaji wa kote nchini humo.

Ramaphosa

Chanzo cha picha, AFP

Katika Afrika, Algeria tayari imeanza kutoa chanjo ya Sputnik V , na makumi kadhaa wamekwisha kupata chanjo, huku Guinea kwa sasa inafanya mazungumzo ili kupata takriban dozi 400,000, alisema afisa wa afya Alhamisi

Waziri wa afya wa Afrika Kusini alisema wiki hii kuwa watengenezaji wa chanjo ya Sputnik V waliwasilisha nyaraka kwa wadhibiti wa madawa kwa ajili ya usajili.

Taarifa zaidi kuhusu corona: