Virusi vya corona: Ukipata maambukizi ya corona utakuwa na kinga kwa miezi kadhaa

Chanzo cha picha, Reuters
Watu wengi ambao wamewahi kupata ugonjwa wa virusi vya corona miili yao imejikinga yenyewe na hawawezi kupata tena ugonjwa huo kwa karibu miezi mitano, utafiti ulioongozwa na wizara ya Afya nchini Uingereza imeonesha.
Kama mwili uliwahi kupata maambukizi, asilimia ya kupata maambukizi hayo yanapungua kwa 83 ikilinganishwa na wale ambao hawajawahi kupata maambukizi hayo, wanasayani wamebaini.
Lakini wataalamu wameonya kuwa baadhi ya watu wanapata maambukizi ya virusi vya corona tena na pia wanaweza kuambukiza wengine.
Maafisa wanasisitiza kuwa watu wanastahili kufuata sheria za kubaki nyumbani - ama wawe wamewahi kupata maambukizi au la.
'Kuokoa maisha'
Profesa Susan Hopkins, aliyeongoza utafiti huo alisema matokeo hayo yanatia moyo kuwa kinga ilichukuwa muda mrefu lakini hilo halikuwa na uhakika.
Pia kulikuwa na wasiwasi kwamba baadhi ya waliopata tena mambukizi wana kiwango cha juu cha virusi - hata kama hawana maambukizi - na walikuwa katika hatari ya kusambaza kwa wengine, alisema.
"Hio ilimaanisha kuwa hata kama umepata maambukizi hayo na unakinga, unaweza kuwa na uhakika kwamba ni vigumu kupata maambukizi makali lakini bado kuna hatari unaweza kuambukiza wengine," aliongeza.
"Kuliko wakati mwingine wowote, ni muhimu sana ikiwa watu wabaki nyumbani kulinda afya zao na maisha yao."
Kuanzia Juni hadi Novemba 2020, ikiwa ni karibu wafanyakazi wa afya 21,000 kote Uingereza walikuwa wanapimwa mara kwa mara kfuatilia ikiwa wana virusi vya corona au walikuwa navyo wakapona.
Kwa wale ambao hawakuwa na kinga ya virusi hivyo huenda hawajawahi kupata maambukizi hayo, huku 318 wakionesha uwezekano wa kupata maambukizi mapya ndani ya kipindi hicho.
Lakini miongoni mwa watu 6,614 waliokuwa na kinga, 44 walikuwa na uwezekano wa kupata maambukizi mapya.
Watafiti wamepokea ushahidi kadhaa unaoonesha kuwa watu hawa walikuwa wamepata tena maambukizi ikiwemo dalili mpya zaidi ya siku 90 baada maambukizi yao ya kwanza, na kupimwa tena.
Baadhi ya vipimo bado vinaendelezwa na watafiti wanasema matokeo yao yatawekwa wazi baada ya kutoka.
'Uwezekano wa kinga kuimarika'
Wanasayansi wataendelea kufuatilia wahudumu wa afya kwa miezi 12 kuangalia kinga yao itadumu kwa muda gani.
Pia watafuatilia kwa karibu maambukizi ya virusi vipya ambayo hayakuwa yameanza kusambaa sana wakati utafiti huu wa kinga kwa waliopata chanjo unafanyika.
Dkt. Julian Tang, mtaalamu wa magonjwa ya virusi kutoka chuo kikuu cha Leicester, alisema matokeo yanatia moyo kwa wahudumu wa afya.
"Kupata kinga baada ya kupona maambukizi ya virusi vya corona sio tatizo... na huenda kukaimarisha kinga ya asili," aliongeza.
"Hili huwa linatokea hata wakati wa msimu wa chanjo ya mafua.
"Ni matumaini yangu kuwa matokeo ya utafiti huu yatapunguza wasiwasi kwa wahudumu wa afya juu ya kupata maambukizi ya virusi vya corona mara mbili."
Mengine yaliyotokea:
- Mwanasayansi mwandamizi amesema maambukizi ya virusi vya corona yanapungua Uingereza na idadi ya maambukizi hayo yameanza kupungua katika baadhi ya maeneo. Lakini Profesa Neil Ferguson ameonya kuwa jumala ya idadi ya vifo huenda ikazidi 100,000
- Baadhi ya maduka ya kuuza dawa Uingereza yataanza kutoa chanjo kwa makundi ya watu waliopewa kipaumbele kuanzia Alhamisi, huku 200 wakipata chanjo hiyo katika kipindi cha wiki mbili zijazo.
- Sheria za kujipima virusi vya corona Uingereza kwa wageni zimesongezwa mbele kwa siku kadhaa ili wasafiri wapate muda wa kujitayarisha, serikali imesema.













