Coronavirus: Je kinga ya virusi vya corona itaziba pengo la chanjo kati ya nchi tajiri na maskini?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mtaalamu wa chembe za urithi Kate Broderick ni miongoni mwa timu ya wanasayansi ambao wanashughulika na moja kati ya majaribio 44 ya kutafuta tiba ya ugonjwa virusi vya corona (Covid-19) ambao kwa sasa ni janga kote duniani.
Ni miongoni mwa timu ya watafiti wa kampuni ya Inovio ya biotekinolojia ya Marekani ambayo inapanga kuwa na dozi milioni moja ya kinga ya Covid 19 kufikia mapema Desemba lakini je ni wapi na ni nani atakayewapokea?
Ni swali ambalo mara nyingi humjia Daktari Broderick. Mwanasayansi huyu wa Uskochi ana dada yake ambaye ni muuguzi katika Hospitali ya Taifa ya Uingereza.
"Dada yangu anakuwa na wakati mgumu kila siku kusaidia watu kukabiliana na ugonjwa huu. Na bila shaka nina wasiwasi kuhusu hali ya kila mmoja wetu," ameiambia BBC.
"Tunahitaji tiba hii kuwa tayari."
Je inawezekana chanjo ya Virusi vya Corona kupatikana kwa usawa?

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini tayari kuna wasiwasi kuhusu vile suluhisho la virusi vya corona kutoka kwa kampuni kama ya Inovio, inaweza ikawa inapatikana kwa nchi tajiri pekee.
Miongoni mwa wanaotoa onyo la kutokea kwa pengo katika utoaji wa chanjo ni mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza Seth Berkley.
Huyu ni mkurugenzi mtendaji wa shirika la kimataifa la chanjo- Gavi, katika mashirika ya sekta za kibinafsi na ya umma yaliyojitolea kuongeza upatikanaji wa chanjo kati nchi 73 maskini zaidi duniani.


Washirika wake ni pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO).
"Ni wakati wakuwa na mazungumzo kama haya, hata ingawa chanjo yenyewe bado haijapatikana," Berkley ameaimbia BBC.
"Changamoto itakuwa ni kuhakikisha kwamba kuna chanjo ya kutosha kwa watu anaohitaji kutoka nchi tajiri lakini pia kwa nchi maskini vilevile."
"Bila shaka nina wasiwasi. Kuna tabia zisizoridhisha zinazojitokeza kila kunapokuwa na bidhaa ambayo ni adimu sana kupatikana. Tunahitajika kufanya maamuzi sahihi kwa sasa ," Berkley ameongeza.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hofu yake haina kithibitisho: Upatikanaji wa chanjo kwa usawa kumekuwa jambo linalopewa angalizo siku za nyuma. Hivi karibuni, Gazeti la Ujerumani la Welt Am Sontag limenukuu maafisa waandamizi serikalini kuonesha kwamba Rais wa Marekani Donald Trump alijaribu na akashindwa kuhakikisha utoaji huduma sawa kwa raia wote wa Marekani ya chanjo inayobuniwa na kampuni moja ya biotekinolojia ya Ujerumani ya CureVac.
Pengo la utoaji wa chancho ya Hepatitis B
Mfano mzuri ni wa chanjo ya hepatitis B, virusi vinavyoongoza katika usababishaji wa saratani ya ini na ambayo maambukizi yake ni mara 50 zaidi ya virusi vya HIV, kulingana na WHO.
Inakadiriwa kuwa watu milioni 257 kote duniani waliishi na ugonjwa wa hepatitis B mwaka 2015.
Chanjo dhidi ya ugonjwa huu ilianza kupatikana kwa nchi tajiri mwaka 1982 lakini kufikia 2000 chini ya asilimia 10 ya nchi maskini duniani ndizo zilizokuwa zinaweza kupata chanjo hii.
Shirika ambalo liliundwa na Bill and Melinda Gates mwaka 2000 la Gavi, limesaidia pakubwa kupunguza pengo hili asante kwa makubaliano ya serikali na kampuni za utengenezaji wa dawa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo mwengine muhimu katika upatikanaji wa chanjo ni ni Muungano wa shirika la kukabiliana na majanga na ubinifu wa tiba lenye makao yake Norway lililoundwa 2017 kufadhili utafutaji wa chanjo kwa kutumia pesa kutoka kwa wa fadhili wa umma na kibinafsi.
Shirika hilo linapigia moja kwa moja linaunga mkono upatikanaji wa chanjo kwa usawa.
"Kama Covid 19 inavyoonesha, magonjwa ya kuambukiza mara nyingi hayatilii maanani mipaka," kampuni hiyo imesema kwenye taarifa.
"Hatuwezi kuzuia wala kusitisha tishio la maambukizi yanayosambaa kote duniani bila kuwepo na chanjo zinazotolewa kwa usawa."
Ukweli wa upatikanaji chanjo

Chanzo cha picha, Getty Images
Mfano mzuri ni Gardasil, chanjo iliyobuniwa 2007 na maabara ya Marekani inayomilikiwa na kampuni ya Merck kukabiliana na virusi vya Human Papilloma Virus (HPV) iliorodheshwa na mamlaka ya Marekani mwaka 2014.
HPV ndio chanzo kikuu cha virusi vingi vya saratani ya mlango wa tumbo la uzazi kote duniani lakini hadi mwaka 2019 chanjo hiyo ilikuwa inapatikana kwa nchini 13 tu maskini.
Wanaotaabika? Upungufu duniani unaosababishwa na uhitaji unaoongezeka

Chanzo cha picha, Getty Images
Asilimia 85 ya vifo kote duniani vya saratani ya mlango wa kizazi vinavyotokea katika nchi maskini.
Ili kuelewa zaidi kwanini upungufu huu unatokea pia tunahtajika kuangazia biashara ya chanjo.
Faida kidogo kutokana na uvumbuzi wa chanjo
Chanjo siyo tu biashara inayotegemewa na maduka ya kuuza dawa wakati ambapo soko la duniani likiwa na thamani ya dola trilioni 1.2 mwaka 2018 na kufikia karibia dola bilioni 40 katika kipindi sawa na hicho.
Tofauti kama hizo zinaakisi vile biashara ya kutengeneza chanjo ni hatari zaidi kuliko biashara ya utengenezaji dawa.
Chanjo inahitaji utafiti wa hali ya juu na gharama yake ni ya juu na pia kanuni na sheria ni ngumu upande wa majaribio.
Pia mashirika ya afya ya umma, wateja wake wakuu wananunua dozi kwa gharama ya chini zaidi ikilinganishwa na wateja wa sekta ya kibinafsi.

Chanzo cha picha, AFP Contributor
Kwa ujumla hilo linafanya biashara ya chanjo kuwa isiyo na faida ikilinganishwa na ile ya utengenezaji wa dawa hasa chanjo ambazo zinatolewa mara moja katika maisha ya mwanadamu.
Marekani, idadi ya kampuni za kutengeneza chanjo ilipungua kutoka 26 mwaka 1967 hadi 5 kufikia 2004, kwasababu makampuni yalianza kuangazia zaidi katika tiba badala ya kuzuia.
Hata hivyo, mambo yamebadilika. Afueni imepatikana kutoka kwa taasisi na watu kama vile Bill and Melinda Gates, ambao wametoa ufadhili wa mabilioni ya madola kuhakikisha chanjo inafikia wengi katika miaka ya hivi karibuni, ambapo uhitaji wa kinga umekuwa ukiongezeka.
Chanjo iliyopata mafanikio makubwa
Chancho kama vile ya Prevenar, kinga kwa watoto na watu wenye umri mkubwa dhidi ya viini vinavyosababisha pneumonia zimekuwa na mafanikio makubwa.
Mwaka 2019, chanjo ya Prevenar ilikuwa moja ya dawa 10 zenye kununuliwa kwa wingi duniani ikitengeneza mapato ya dola bilioni 5.8, kulingana na Jarida la Kisayansi la Nature.
Chanjo iliyotengenezwa na kampuni ya Pfizer, kinga iliyokuwa na mauzo ya juu hata kuliko zile zinazosemekana kuwa bidhaa maarufu za kimataifa kama vile: Viagra.

Chanzo cha picha, Getty Images
Huku shirika la kimataifa la chanjo la Gavi likiwa linashirikisha hata nchi maskini, dozi moja ya chanjo ya Prevenar ni chini ya dola 3 kwasababu ya makubaliano ya kibiashara ( ya kununua chanjo hiyo kwa kiwango cha juu na kupunguza gharama ya dozi moja) bei ambayo Marekani imepanda hadi dola 180.
Uingereza, dozi bili ya chanjo ya HPV ambayo inatolewa bure kwa wasichana na wavulana kati ya umri wa miaka 12 na 13, itafanya gharama hiyo kuwa dola 351.
Kwa shirika la kimataifa la chanjo la Gavi ni chini ya dola 5 kwa dozi moja.
Wasiwasi wa soko huru
Kwahiyo kwa nchi tajiri, faida ni ya juu kama namna ya kwanza ya kufidia gharama ya utafiti na utengenezaji wa chanjo.
Chama cha Dawa cha Uingereza kinakadiria kwamba ubunifu wa chanjo mpya kunaweza kugharimu hadi dola bilioni 1.8.
"Iwapo maamuzi yataachiwa soko huru, watu kutoka nchi tajiri pekee ndio watakaoweza kupata chanjo ya ugonjwa wa Covid 19," Mark Jit, Profesa wa chuo kikuu cha London na magonjwa ya nchi za Kitropiki, ameelezea BBC.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Hili tumelishuhudia katika chanjo nyingi za nyuma lakini wakati huu tutashuhudia maafa zaidi iwapo hilo litatokea tena."
Pia, licha ya faida ndogo, kampuni kubwa za dawa kama vile Pfizer na Merck zinasimamia asilimia 80 ya mauzo ya chanjo duniani, kulingana na takwimu za WHO.
Kwa hiyo kuna uwezekano kwamba kampuni kubwa za kuuza dawa hatimaye zitakuwa na jukumu muhimu katika chanjo ya Coronavirus.
"Huenda wazo la awali lisiwe lao lakini wao ndio wenye uwezo wa kifedha wa kuhakikisha chanjo inapatikana," Ana Nicholls, mchambuzi wa kiwanda cha dawa cha Economist Intelligence ameiambia BBC.
Makubaliano
Kampuni ya Inovio, kwa mfano, itashirikiana na kampuni ya dawa kuongeza uzalishaji hadi kiwango cha mamia ya mamilioni ya dozi kadhaa iwapo chanjo ya Covid 19 itakuwa na mafinikio.
Kampuni kubwa kubwa zimeahidi kuhakikisha kila mmoja anapata chanjo katika miaka ya hivi karibuni.
Kampuni ya Uingereza ya GlaxoSmithKline (GSK), moja ya kampuni kubwa za dawa kote duniani inashirikiana na wengine kutafuta chanjo ya Covid 19.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Kupata tiba ya Covid 19 kunahitaji ushirikiano kutoka kwa kila mmoja katika sekta ya afya," amesema mkurugenzi Emma Walmsley katika taarifa.
"Tunaamini pakubwa kwamba ushirikiano kati ya wanasayansi, viwanda, wadhibiti, serikali na wahudumu wa afya kutasaidia pakubwa kulinda watu na kutoa suluhisho kote duniani kukabiliana na janga hili."
Seth Berkley kutoka Shirika la kimataifa la chanjo - Gavi anaamini kwamba makubaliano hayo yatakuwa muhimu iwapo tunataka kupunguza pengo la chanjo baina ya nchi.
"Bila shaka upatikanaji wa chanjo kwa wote ni jambo ambalo haliwezi kufikiwa mara moja"
"Lakini hili haliwezi kufikiwa kwa kuzingatia upatikanaji wa chanjo kwa misingi ya uwezo wa nchi kulipia gharama," ameongeza.
"Iwapo tutashindwa kutoa chanjo hii kwa nchi zenye uhitaji zaidi, ni wazi kuwa janga hili litaendelea."












