Kundi la watu DRC lakichoma moto chuma cha ajabu

Chanzo cha picha, Reuters
Chuma cha ajabu kilichoonekana katika eneo la makutano ya barabara jijini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kimeteketezwa na moto kwa kuhofia uasili wa chuma hicho.
Watu mjini Kinshasa, wamekipiga mawe na kukichoma chuma hicho cha ajabu cha kung'aa chenye futi 12 ambacho kinafanana na vyuma kadhaa ambavyo vimekuwa vikionekana duniani kote miezi ya hivi karibuni, cha kwanza kilionekana Utah nchini Marekani mwezi Novemba mwaka jana.
Wengi walipokiona walianza kwa kukipiga picha na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.
Hata hivyo, wengi walihofia imani za nguvu za giza.
"Tumeamka tu na kuona chuma hiki cha ajabu cha pembe nne... Tulishangazwa kwasababu ni chuma ambacho huwa tunakiona kwenye makala kuhusu freemasons au illuminati," mkazi mmoja wa eneo hilo Serge Ifulu aliiambia Reuters.
Uvumi kuhusu chuma hicho ambacho ulianza kusambaa katika mji wa Bandal mwishoni mwa wiki iliyopita lakini Jumatano wakaanza kukiteteza.

Chanzo cha picha, Reuters
Walioshuhudia tukio hilo wanasema watu walitaka kujua kuna nini ndani ya chuma hicho baada ya kukichoma walikuta kuna vyuma tu.
Meya wa eneo hilo Bayllon Gaibene ameliambia shirika la BBC kuwa wametuma sehemu ya chuma hicho kwa wanasayansi ili kijulikane kilipotokea.
Na alikanusha madai yanayomshutumu Gavana wa Kinshasa Gentiny Ngobila kuhusika na kutokea kwa chuma hicho cha ajabu.

Chanzo cha picha, Reuters
Msemaji wa Ngobila anasema meya anataka kuleta gumzo tu.
Kwanza sio chuma cha kwanza cha aina hiyo kuonekana duniani na kuzua taharuki za kiimani na haswa za kisayansi .
Watalii walikimbilia kukiona chuma cha ajabu kilichoanguka Utah nchini Marekani Novemba mwaka jana.
Na kikauzwa kwa dola 45,000 (£34,000).
Vyuma vingine vya aina hiyo vilionekana Uingereza kikiwemo kile cha Isle of Wight kilichotokea mwezi Desemba.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe

Kuna kingine kilionekana nchini Uturuki mwezi huu , na wao wakataka kukiweka katika hifadhi ya vivutio vya dunia.













