Mapinduzi ya Myanmar: Suu Kyi akabiliwa na shtaka jipya

Protesters are demanding the release of Aung San Suu Kyi after the elected leader was detained in a coup

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Waandamanaji wataka Aung San Suu Kyi kuachiwa huru

Kiongozi wa Myanmar ambaye yupo kizuizuni bi, Aung San Suu Kyi, ameongezewa shtaka la pili la jinai mahakamani alipofika kusikiliza kesi inayomkabili.

Bi Suu Kyi, ambaye hapo awali alishtakiwa kwa kumiliki kifaa cha mawasiliano aina ya redio sasa anadaiwa pia kukiuka Sheria ya Maafa ya Asili nchini humo.

Hata hivyo Jeshi la Myanmar hapo awali lilisema kuwa litatekeleza ahadi yake ya kufanya uchaguzi mpya na kuachia madaraka walioitwaa.

Huku hayo yakiendelea, waandamanaji wanaopinga mapinduzi hayo ya kijeshi wanadai kuachiliwa kwa viongozi wao waliowachagua kidemokrasia.

Katika mkutano wa kwanza wa wanahabari tangu kuangushwa kwa serikali, msemaji wa jeshi Brigedia Generali Zaw Min Tun amesema vikosi vya jeshi havitabaki madarakani kwa muda mrefu, na akaahidi "kurudisha nguvu kwa chama kilichoshinda" kufuatia uchaguzi uliopangwa.

Hata hivyo tarehe ya uchaguzi mpya bado haijatajwa.

Akizungumza katika mji mkuu Nay Pyi Taw , Zaw Min Tun pia alirudia madai hayo - bila kutoa ushahidi - wa ulaghai katika uchaguzi wa Novemba uliopita.

Chama cha Bi Suu Kyi cha National League for Democracy (NLD) kilipata ushindi mkubwa katika kura hiyo. Jeshi limedai udanganyifu kama haki ya mapinduzi yake.

Uingereza na Marekani kwa pamoja wamekosoa madai hayo.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema "walizushwa" na "ukiukaji wazi wa haki zake za binadamu", wakati msemaji wa idara ya serikali ya Marekani akiwaita kuwa ni watu wasumbufu.

People with placards take part in a protest against the military coup outside the US embassy in Yangon, Myanmar, 16 February 2021

Chanzo cha picha, Reuters

Bi Suu Kyi alijitokeza kwa muda mfupi katika mahakama iliyopo mji mkuu Nay Pyi Taw.

Inasemekana alijibu maswali juu ya mipango ya kisheria na uwakilishi.

Amepangiwa kufikishwa tena mahakamani Machi 1 mwaka huu.

Waandamanaji wameendelea kupambana na maafisa wa usalama na kumekuwa na ripoti za hivi karibuni za polisi kutumia mabomu ya machozi na risasi za mpira ili kuwatawanya.

Protesters opposed to the military coup block the railway between Yangon and the southern city of Mawlamyine, Myanmar February 16, 2021 i

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wapinzani wapinga mapinduzi ya jeshi

Maandamano yakoje katika taifa hilo?

Waandamanaji wamekuwa wakipambana na maafisa wa usalama na hivi karibuni kumekuwa na ripoti kuwa polisi wanatumia mabomu ya machozi kutawanyisha waandamanaji hao.

Muandamanaji mmoja ambaye yuko kwenye hali mbaya alipigwa risasi Februari 9.

Huku waandamanaji wengine 19, wakiwa wamejeruhiwa vibaya .

Zaw Min Tun amesema hatua zinachukuliwa kukabiliana na mkusanyiko wa watu wanaowarushia mawe polisi.

Myanmar -

  • Myanmar, inajulikana pia kama Burma, ilikuwa chini ya utawala wa kijeshi kuanzia mwaka 1962 mpaka 2011
  • Harakati za ukombozi zilianza mwaka 2010, na kulifanya taifa hilo kuwa na uchaguzi huru mwaka 2015 na mwaka uliofuata serikali ya taifa hilo kuanza kuongozwa na kiongozi nguli wa upinzani Aung San Suu Kyi
  • Mwaka 2017, mgogoro mkubwa uliibuliwa na jeshi la Myanmar katika eneo la waislamu wa Rohingya ambapo mamilioni ya watu walikimbilia mpakani mwa Bangladesh, jambo ambalo baadaye Umoja wa Mataifa UN iliita kuwa "mfano wa kitabu cha utakaso wa ukabila"
  • Aung San Suu Kyi na serikali yake ilipinduliwa na jeshi Februari 1 February kufuatia matokeo ya uchaguzi wa Novemba.