Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Aliyekuwa Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo awekewa vikwazo na China
Mike Pompeo, Steve Bannon, Peter Navarro, au Alex Azar ni miongoni mwa maafisa wakuu katika utawala wa rais Trump ambao wamewekewa vikwazo na China wiki hii.
Taifa hilo la bara Asia linamshutumu waziri huyo wa masuala ya kigeni , aliyekuwa mshauri wa Ikulu ya White House na mpanga ratiba katika ofisi ya biashara na sera , na maafisa 24 wa zamani kwa kuchukua hatua zinazoingilia vibaya masuala ya ndani ya China.
Vikwazo vilivyowekwa vinashirikisha marufuku ya kuingia nchini humo ama kufanya biashara na China.
Kulingana na taarifa iliochapishwa katika gazeti la People Daily, msemaji wa chama cha kikomyunisti cha China , amesema kwamba ''maafisa hao walikiuka uhuru wa taifa hilo na kwamba ndio waliohusika na baadhi ya matatizo yanayoihusu China''.
Katika kipindi chote cha utawala wa rais Trump, Maafisa walijulikana kwa msimamo wao mkali dhidi ya China na wamekuwa wakishutumiwa na vyombo vya habari vya China.
Kulingana na taarifa , katika miaka ya hivi karibuni , ''baadhi ya wanasiasa wanaopinga utawala wa China walioshawishiwa na maslahi yao na chuki bila kufikiria kuhusu maslahi ya raia wa China na wale wa Marekani wamepanga , kukuza na kutekeleza hatua mbaya dhidi ya China''.
''Vitendo hivyo vimeathiri vibaya masuala ya ndani ya China , kukandamiza maslahi yake kukera raia wake na kuharibu vibaya uhusiano kati ya mataifa hayo mawili''.
Uhusiano huo umezorota haraka tangu mwezi Machi 2018 , wakati rais Trump alipoanzisha vita vya kibiashara dhidi ya China ambavyo vilipanuka na kuathiri sekta nyingine.
Makabiliano ya hivi karibuni yalitokea kabla tu ya uamuzi wa Wachina, wakati siku ya mwisho ya urais wa Trump, Waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo alisema kwamba serikali ya China imetekeleza "mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya Binadamu" katika kampeni yake ya ukandamizaji dhidi ya jamii ya Kiisilamu la Uighur katika mkoa wa Xinjiang, Magharibi mwa China.
Maneno hayo hayakupokewa vizuri huko Beijing, ambayo kwa muda mrefu imepokea ukosoaji kutoka kwa jamii ya kimataifa kuhusu namna inavyoitendea jamii hiyo ya wachache wa Uighur, ambayo imeandikwa sana na vyombo vya habari vya kimataifa, pamoja na BBC.
Uchunguzi wa BBC: kambi zilizofichwa za mafunzo ambapo Waislamu wamefungwa nchini China
Serikali ya China imekanusha kwa nguvu madai ya ukandamizaji na unyanyasaji huko Xinjiang.
Imewahakikishia watu waliofungwa katika kambi za "kutoa elimu" zilizojengwa katika eneo hilo hupokea "mafunzo ya ufundi", katika mfumo wa mapambano dhidi ya "ugaidi, msimamo mkali na kujitenga."
Matamshi ya Pompeo yalikuja wakati wa kuzorota vibaya kwa uhusiano kati ya serikali mbili kuu za ulimwengu na baada ya kampeni ya Biden mwenyewe kuelezea matukio huko Beijing huko Xinjiang kama "mauaji ya kimbari," waandishi wa habari wa Marekani walisema.
Rais mpya wa Marekani, Joe Biden, amewahi kumtaja Rais wa China Xi Jinping kuwa "muasi."
Wataalam wanasema kwamba sera mpya na China haitabadilisha msimamo wake.
Tofauti na Trump, Biden anatarajiwa kutafuta ushirikiano wa pande nyingi kuipiku China.