Uingereza yaanza enzi mpya bila washirika wake wa Ulaya mwaka mpya

Enzi mpya imeanza Uingereza baada ya kujiweka huru na Ulaya

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Enzi mpya imeanza Uingereza baada ya kujiweka huru na Ulaya

Uingereza iliacha kufuata sheria ya EU saa 23:00 GMT, baada ya mpango mbadala wa usafiri , biashara, uhamiaji na ushirikiano wa kiusalama kuanza kutekelezwa.

Boris Johnson alisema Uingereza ina " uhuru mikononi mwake" na uwezo wa kufanya vitu "Tofauti na bora" na sasa muda uliokuwa ukisubiriwa umekwisha .

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema Uingereza itasalia kuwa "rafiki na mshirika".

Mawaziri wa Uingereza wameonya kutashuhudiwa changamoto katika siku na wiki chache zijazo, wakati sheria mpya zitakapoanza kutekelezwa na mashirika ya Uingereza yanayofanya biashara na bara Ulaya yatakapoanza kukumbana na mabadiliko hayo.

Maafisa wamesisitiza mifumo mipya ya mipakani ''iko tayari'' kuanza kazi licha ya hofu ya mizigo kukwama bandarini.

Uingereza ilijiondoa katika muungano huo wa kisiasa na kiuchumi uliyo na nchi wanachama 27 miaka mitatu na nusu iliyopita baada ya raia wa Uingereza kupiga kura ya maoni mwaka 2016, maarufu Brexit.

Lakini iliendelea kufuata sheria za kibiashara za EU katika kipindi cha miezi 11 wakati pande hizo miili zilipokuwa zikishauriana kuhusu ushirikiano wao wa kibiashara wa siku zijazo.

Baada ya mazungumzo hayo kukamilika, mkataba wa kihistoria uliafikiwa mkesha wa Krismasi. Ulikuwa sheria siku ya Jumatano baada ya kuidhinishwa na bunge.

Chini ya sheria hilo mpya, alioanza kutekelezwa 24:00 CET, Wafanyabiashara wa Uingereza watafikia masoko ya ndani ya EU bila kulipishwa kodi, kumaanisha bidhaa zinazosafirishwa kati ya Uingereza na Ulaya hazitatozwa kodi.

Lakini inamaanisha nyaraka zaidi kwa wafanyabiashara na watu wanaosafiri kwenda nchi za EU wakati bado kuna kutokuwa na uhakika juu ya nini kitatokea kwa benki na huduma, ambazo ni sehemu kuu ya uchumi wa Uingereza.

Uchambuzi

Ni hatua ambayo baadhi ya watu wameipokea kwa matumaini makubwa na wengine wakiwa na masikitiko.

Mkataba huo wa kihistoria umeafikiwa wakati, baadhi ya sekta zitanufaika zaidi ya zingine - kwa mfano, kunatarajiwa msongamano katika kituo cha Dover siku ya kwanza ya mwaka 2021 wakati uangalizi wa mpakani utaanza kutekelezwa.

Hata hivyo, kuna mabadiliko kidogo yatakayoshuhudiwa hapo - iwe ni katika masuala ya biashara, usafiri na uhamiaji.

Na huku janga la corona likiendelea- kufungia jamii- mabadiliko hayo huenda yakashuhuduwa zaidi miezi michache ijayo

Waziri Mkuu apongeza 'hatua ya ajabu'

Bw. Johnson - ambaye amekuwa kiungo muhimu katika kampeni ya Brexit katika kura ya maoni ya mwaka 2016 na kuiondoa Ungereza ndani ya EU mwezi Januari - miezi sita baada ya kuwa Waziri Mkuu- alisema ''ulikuwa wakati wa ajabu' kwa Uingereza.

Katika ujumbe wake wa mwaka mpya, Waziri Mkuu alisema Uingereza sasa iko ''huru kufanya vitu tofauti, na ikiwezekana vyema zaidi kuliko marafiki zetu wa EU.

"Uhuru wetu uko mikononi mwetu, tunaweza kuamua tutakacho," alisema.

Lord Frost, Mshauri mkuu wa Ungereza, aliandika kwenye Twitter kwamba Uingereza ''imekuwa huru tena'' huku mbunge mkongwe wa Conservative Sir Bill Cash akisema matokeo yalikuwa ''ushindi kwa demokrasia".

BBC haiwajibikii maudhui yao katika tovuti zingine

Waziri wa Mambo ya Nje Simon Coveney alisema sio "jambo la kusherehekea" na uhusiano wa Uingereza na Ireland utakuwa tofauti kuanzia sasa, lakini "nawatakia kila la heri".

Lakini wanaopinga Brexit wanashikilia kuwa nchi itafanya vibaya kuliko wakati ilipokuwa ndani ya EU.

Waziri wa kwanza wa Uskochi Nicola Sturgeon, ambaye alama yake ni kuiregesha Ushokochi EU, aliandika kwenye Twitter: " Uskochi itarejea hivi karibuni, Ulaya. Endelea kuangaza."

Mjini Brussels, kutakuwa na utulivu baada ya mchakato wa Brexit kukamilika, lakini kuna hali ya kutoridhika kutokana na hatua yenyewe ya Brexit .

Ukweli ni kwamba, Muungano wa Ulaya unafikiria Brexit umezifanya dhaifu - EU na Uingereza.

Nchi ya kwanza inayokujia akilini ukitaja mwaka mpya ilikuwa Australia. Maonyesho ya fataki ya Sydney yalifanywa kama kawaida lakini watu hawakuruhusiwa kukusanyika kujionea kama ilivyo ada .

"Hatutaki kuwa na hafla ambayo itasambaza virusi mkesha wa mwaka mpya," Waziri mkuu wa New South Wales Gladys Berejiklian alisema.

Wakazi Wendi wa Sydney walifuatilia onyesho hilo kwenye televisheni zao nyumbani, ambako watu watano tu waliruhusiwa kuwa pamoja.

Waziri Mkuu Boris Johnson alisema Uingereza ina " uhuru mikononi mwake"

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Waziri Mkuu Boris Johnson alisema Uingereza ina " uhuru mikononi mwake"

PICHA

China, tamasha la mwangaza linalofanyika kila mwaka katika mji mkuu wa Beijing kililifutiliwa mbali. Lakini katika mji wa Wuhan, ambao unadhaniwa kuwa chimbuko la janga la corona, maelfu ya watu walikusanyika kati kati ya mji huo kusherehekea huku vibofu vikiachiliwa angani.

Japan ilifuta sherehe za jadi za kukaribisha mwaka mpya ambayo Emperor Naruhito na familia yake ilikuwa iwasalimie watu.

Nchini India, Delhi na miji mingine kadhaa, amri ya kutotoka nje usiku na masharti mengine ya kuzuia mikusanyiko mikubwa ya watu wakati wa mwaka mpya iliwekwa

Hata hive nchini New Zealand,ambako amri kari ya kutotoka nje na kufungwa kwa mipaka kumesaidia kuangamiza ugonjwa wa corona, she/he za kuukaribisha mwaka maya ziliandaliwa kama kawaida.Nchi za Asia-Pasifiki zimeathiriwa vipi?