Ni kiasi gani cha chumvi kinachopendekezwa kwa siku

Eliminate the salt shaker from your table, if you are looking to reduce salt consumption.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ondoa chupa ya chumvi mezani ikiwa unapanga kupunguza kiwango cha chumvi unayotumia

Msimu wa siku kuu unapobisha hodi, baadhi ya watu huwa makini kuhusu kile wanachokula ili wasiongeze uzani wa mwili, kwa sababu wanahisi wataongeza kilo kadhaa kutokana na mililo tofauti inayoandaliwa msimu wa sherehe.

Mara nyingi watu huwa waangalifu kuhusu kiwango cha vyakula vilivyo na wanga, sukari na mafuta. Lakini ni nadra kuangazia chumvi, madini ambayo haiwafanyi watu kunenepa lakini inaweza kuwa na athari kwa afya ikitumiwa kupita kiasi.

Kwa mujibu wa Shirika La Afya Duniani (WHO), mtu mzima anatakiwa kutumia kiwango cha chumvi kisichozidi gramu tano kwa siku ili kupunguza shinikizo la damu na hatari ya kupata magonjwa ya moyo.

Kupunguza kiwango cha chumvi kwenye chakula sio vigumu kama inavyodhaniwa , lakini kabla ya kufanya hivyo wacha tuchambue baadhi ya dhana zinazoenezwa kuhusu bidhaa hii inayotumiwa zaidi katika vyakula vya ulimwengu.

1. Ukitokwa na jasho jingiunahitaji kuongeza chumvi zaidi katika chakula

Japo ni kweli kwamba kutokwa jasho jingi kunapunguza madini aina ya sodium chloride, kiwango kinachopotea kupitia jasho ni kidogo sana kiasi cha kumfanya mtu ahitaji kuongeza chumvi kwenye chakula.

Ikiwa jua kali limekufanya utokwe na jasho kuliko kawaida, ni vyema kunywa maji mengi.

Chakula kilicho na madini muhimu na lishe murua inatosha kufidia kiwango cha chumvi ulichopoteza mwilini.

Chipsi

Chanzo cha picha, Getty Images

Ikiwa umetokwa na jasho jingi kutokana na mazoezi , hali ni tofauti kidogo lakini inategemea umefanya mazoezi kiasi gani.

Kwa mujibu wa Taaasisi ya matibabu katika chuo kikuu cha Harvard, nchini Marekani, ikiwa unafanya kazi inayokufanya kutumia nguvu kwa kati ya saa 8 na 12, huenda ukapoteza kiwango kikubwa cha madini ya sodium kwa siku kutokana na jasho na huenda ukatumia chumvi nyingi kuliko kiwango kinachopendekezwa.

Lakini ukiwa unafanya mazoezi ya karibu dakika 30 kwa siku , na unafuata mpango maalum wa lishe, kuna uwezekano huenda unatumia chumvi nyingi kwa hivyo hakuna haja ya kuongeza chumvi katika chakula chako.

2. Chakula kisichokuwa na chumvi hakina ladha

Hii ni kweli kwa kiwango fulani ikiwa umezoea kutumia chakula kilicho na chumvi nyingi, kwa sababu mdomo umezoea.

Lakini ukizoea kula chakula kilicho na chumvi kidogo, huenda ukafurahia chakula chako kadri unavyogundua ladha tofauti ambayo hukuwa umezoea kutokana na matumizi ya chumvi kupita kiasi.

Kupika kwa kutumia chumvi kiasi (au bila chumvi) pia ni mwenendo mzuri utakaokupatia nafasi ya kujaribu viungo ambayo hujazoea.

Viungo vbay kupikia
Maelezo ya picha, Jifunze kupika kwa viungo kuipatia milo yako ladha nyingine

3. Vyakula vilivyo na viwango vya juu vya chumvi vina chumvi nyingi.

Bila shaka.

Vyakula vingi vilivyo na kiwango cha juu cha chumvi huenda visiwe na chumvi kwako kwa sababu huenda vimechanganywa na viungo vingine kama vile sukari kupunguza kiwango cha chumvi

Njia nzuri ya kubaini kiwango cha chumvi ndani ya chakula ni kusoma kiwango cha madini ya sodium kwenye pakiti ya bidhaa.

Pia unatakiwa kujua kwamba kuna vyakula ambavyo vinachangia kiwango cha juu cha chumvi kwenye chakula chako , lakini sio kwa sababu vina chumvi nyingi. Wataalamu wanasema kwamba vyakula vya aina hiyo huongezea kiwango cha chumvi mwilini mwako kwasababu umekula vingi, kwa mfano mkate au nafaka kwa kiamsha kinywa.

4. Ni wazee tu wanafaa kuwa waangalifu wanapotumia chumvi

Hii sio kweli.

Chumvi

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa mujibu wa WHO, utumizi wa chumvi kupita kiasi unaweza kumsababishia mtu shinikizo la damu akiwa umri wowote.

Kuna vyakula ina tano ambavyo vina kiwango cha juu cha chumvi kuliko ulivyodhania.

Lakini tunaweza kuwafundisha watoto kutokuwa na mazoea ya kula chumvi nyingi ili kuwaepusha na hali ya kupenda chumvi.

5. Kupunguza chumvi ni hatari kwa afya yako

Madini ya Sodium ambayo inapatikana kwa chumvi ni muhimu kwa mwili kwanai inasaidia mwili kufanya kazi vyema.

Lakini ukweli ni kwamba, kihistoria, idadi kubwa ya watu wanatumia chumvi nyingi kuliko ilivyopendekezwa.

Kupunguza chumvi katika chakula chako hakuwezi kuathiri vibaya afya yako kwa sababu, ni vigumu sana kula chumvi kidogo: vyakula vingi tunavyokula kila siku vina chumvi.

6. Kutumia chini ya gramu 5 ya chumvi kama ilivyopendekezwa na WHO ni vigumu

Walea ambao wanaweka chumvi katika kila chakula wanashtuka wakisikia kwamba kwa siku wanatakiwa kutumia nusu ya kijiko cha chai kwa siku.

Lakini ukiamua kupunguza chumvi katika chakula chako inawezekana, kuna vitu vingi unavyoweza kuzingatia kufikia lengo hilo.

Vidokezo muhimu ambavyo huenda vikakusaidia:

Usitumie kiholela sosi, hususan mchuzi wa soya, ambao una kiwango cha juu cha chumvi. Michuzi ya nyanya huwa na chumvi kidogo kuliko ile ambayo ni pamoja na jibini, mizeituni,

  • Jiepusha kula vyakula vya nafaka, vibanzi, na vyakula vingine vilivyo na hcumvi nyingi. Badala yake tumia vyakula visivyo na chumvi nyingi.
  • Usiweke chumvi kwenye chakula wakati unapopika badala yake tumia viungo vingine kuongezea ladha chakula chako.
  • Usiongeze chumvi kwenye chakula kabla hujaonja kwanza.
  • Ondoa chupa ya chumvi mezani ikiwa unapanga kupunguza kiwango cha chumvi unayotumia(wakati mwingine uvivu wa kwenda kuchukua chumvi kunakusaidia).
  • Ikiwa utatumia bidhaa zilizosindikwa, linganisha lebo kabla ya kununua na uchague zile zilizo na kiwango cha chini kabisa cha sodiamu.