Fahamu kwanini ni vigumu kumsamehe mpenzi wako wa zamani?

Chanzo cha picha, NURPHOTO
Mara kwa mara ni vigumu kwa watu wawili waliopendana kuvunja penzi lao, lakini kwa nini watu hupigania kurudiana huku wengine wakilipuuzilia mbali na kuendelea na Maisha yao?
Lengo la kuuwasha mshumaa ambao ulikuwa umezima linatokana na masuala kadhaa moyoni na akilini.
Yannes alikuwa na machozi machoni mwake wakati alipomwambia mpenzi wake George kwamba uhusiano wao hauwezi kuendelea.
Ilikuwa mara ya tatu wapenzi hao walikuwa wamuvunja uhusiano wao katika kipindi cha miezi miwili.
Wakati huu Yaness anasema kwamba kulikuwa hakuna fursa ya wao kurudiana tena.
Kila wakati alipokuwa akikumbuka yaliojiri alikuwa amezidiwa na kumbukumbu hizo ."Namuwaza sana na akili yangu imekuwa ikikumbuka siku na wakati mzuri tuliokuwa pamoja hivyobasi nilimfuata mara kadhaa'', alisema Yannes.
Lakini tunavyofikiria ni tofauti na kwamba hali haibadiliki. Nilifuta picha zake zote katika akaunti zangu za mitandao ya kijami na najua huo ndio ulikuwa wakati wa mwisho tukiwa pamoja.
Karibia thuluthi mbili za wanafunzi vyuoni hufufua tena mahusiano yao ya kimapenzi mara kadhaa na nusu yao hujamiana baada ya mahusiano yao kuvunjika.

Chanzo cha picha, Getty Images/AVIER HIRISCHFELD
Vijana wadogo ndio wanaopona kwa haraka baada ya mahusiano yao kuvunjika .
Mahuasiano hufufuliwa mara mbili huku kila mmoja akiapa kurudiana na mpenzi wake wa zamani.
Wanandoa wengi ambao wamepeana talaka hurudiana .
Hisia hizi hushirikisha nyimbo zisizohesabika , filamu, vipindi vya runinga na kadhalika .
Kuvunja mahusiano na baadaye kuomba msamaha ni suala lililopo akilini mwetu.
Lakini kwanini tunajaribu kuunda tena penzi ambalo tayari limekufa?

Chanzo cha picha, JAVIER HIRISCHFELD / GETTY IMAGES
Watu ambao huogopa kusalia peke yao hujaribu kurudiana na wapenzi wao wa zamani.
Wakati wanandoa wanapoachana , Wengine uhisi kile ambacho Hellen Fisher , mwansaikolojia anakiita awamu ya pingamizi, ambapo mtu anayechukiwa hawezi kuhimili hadi pale atakapokutana na mtu aliyekuwa naye katika mahusiano hayo.
Fisher na kundi la wanasayansi wamechunguza ubongo wa watu 15 ambao walivunja mahusiano yao . wakati wa utafiti huo , picha za wapenzi wao zilioneshwa , na watalaam wa sayansi walichunguza bongo za watu waliovunja uhusiano na kwamba akili zao zilikuwa zinawapendelea wapenzi wao wa zamani.

Chanzo cha picha, JAVIER HIRSCHFELD / GETTY IMAGES
''Pia kumekuwa na tabia ya kuvunja uhusiano ama kuharibu uhusiano. Wakati mtu unayempenda anapoondoka , huwachi kumpemda mtu huyo na kwamba mapenzi yako kwa mtu huyo huongezeka'', alisema Fisher.
Pia kuna kipande cha ubongo kinachokabiliana na mambo fulani, na kwamba watu waliokataliwa kwasababu ya kimapenzi hawaachi kuwatafuta wapenzi wao wa zamani mara kwa mara.
Wanasayansi wanahisi kwamba hii ndio sababu mtu hawezi kupiga hatua bila mpenzi wake wa zamani.
Suala la masuala ambayo hayajatatuliwa katika talaka ni mojawapo ya masuala ambayo huwafanya watu kujaribu kuwasha moto penzi lao kulingana na mtafiti Rene Dailey , profesa katika chuo cha Texas ambaye hufanyia utafiti chanzo cha mapenzi kuvunjika na watu kurudiana.

Chanzo cha picha, JAVIER HIRSCHFELD / ALAMY
Inaweza kukusadia kukaa mbali na mpenzi wako wa zamani hata iwapo unataka kurudi.
''Ni rahisi kwa wapenzi kupigana baada ya uhusiano wao kuvunjika, lakini bado wanahisi mapenzi'', anasema Dailey.
Kama anavyosema Yannes, upweke, furaha mawazo ya nyakati za furaha huchangia pakubwa kwa wapendanao kurudiana, kulingaa na Kristen Mark , profesa wa masuala ya afya ya ngono.
Mitandao ya kijamii kama vile Facebook , pia huchangia pakubwa katika kuwaunganisha tena wanandoa , kwasabahu huona picha zilizochapishwa.
Lillian msichana mwengne kutoka mji wa Hong Kong, aliye katika umri wa miaka 20 na mmoja ya wanandoa anayehangaika katika mitandao ya kijamii.

Chanzo cha picha, JAVIER HIRSCHFELD / GETTY IMAGES
Mojawapo ya vidokezo vinavyotolewa na watu wanaowasaidia wanandoa waliotalakiana ni kwamba yule anayetaka kurudisha uhusiano huo ni sharti kujipamba hali ya kwamba anaweza kumvutia yule aliyetalakiana naye.
Siku kadhaa baada ya talaka hiyo alitafuta katika intaneti kwa njia za kurudiana na mpenzi wake wa zamani.
Ameona picha zilizochapishwa na mtu anayewasaidia watu kama hao kutatua masuala hayo.
Lilian anasema kwamba mtu huyo alimpatia ushauri ikiwemo ule wa kuzuia kurudiana na mpenzi wako wa zamani.
Lakini mapendekezo hayo hayakufua dafu. Wataalam wanapendekeza kwamba katika kipindi cha kati ya siku 30 hadi 60 , mtu huzuia kuwasiliana na mpenzi wake walieachana naye na wakati huo hujaribu kujiweka katika awamu mpya.












