Mzozo wa Tigray: Wanajeshi wa Ethiopia walaumiwa kwa kufunga mpaka wa Sudan

Refugees who have fled Ethiopia's northern Tigray region amid fierce fighting
    • Author, Na Anne Soy
    • Nafasi, BBC Afrika

Idadi ya wakimbizi wanaotoroka jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia - ambako vikosi vya kitaifa vinakabiliana na wapiganaji wa jimbo hilo - imepungua baada ya wanajeshi wa kupelekwa katika mpaka wa nchi hiyo na Sudan.

BBC iliwaona wanajeshi hao mara ya kwanza siku ya Jumatano, katika kituo cha mpakani cha Hamdayet, na imekuwa ikipata ushuhuda kutoka kwa wakimbizi wanaosema jamaa zao wamezuiliwa kutoka nchini Ethiopia.

"Niliwasili jana asubuhi lakini nataka kurudi nyumbani kuchukua familia yangu," alisema mmoja wa wakimbizi hao ambaye hakutaja jina lake kutambulishwa.Akizungumza na BBC katika kingo za mto Sittet mjini Hamdayet, alisema ameshindwa kurudi Tigray kuchukua familia yake kwasababu "kuna wanajeshi waliofika mpakani kabla yangu na wameniambia nisirudi huko".

Serikali ya Ethiopia haijaitikia ombi la BBC la mara kadhaa kutaka itoe maelezo kuhusu madai hayo.

Upande wa pili wa mto ambao uko kati ya nchi hizo mbili, makumi ya wanajeshi wanashika zamu kwa kupokezana juu ya mlima kuelekea upande Tigray. Maboti yameegeshwa pande zote mbili katika kivuko hicho kilicho na shughuli nyingi.

Wanajeshi wa Ethiopia wamepelekwa katika eneo la mpaka wa nchi hiyo na Sudan
Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Ethiopia wamepelekwa katika eneo la mpaka wa nchi hiyo na Sudan

Makumi ya wakimbizi wamekusanyika katika eneo jimpya mpaka wa Ethiopia ambako wanajeshi wanashika doria. Wengine - wakimbizi wameungana na wakimbizi wenzao wa Sudan - na wamekuwa wakiteka maji au kufua nguo pamoja. Kundi la watoto limekuwa likiogelea na kuchezea maji.

Lakini cha kushangaza ukivuka mto huo upande wapili hakuna mawasiliano- kumaanisha wale waliotenganishwa na jamaa zao katika jimbo la Tigray hawana njia ya kuwasiliana nao.

Shirika la kutetea haki la Human Rights Watch, limekuwa likiwanukuu wakimbizi waliowasili Sudan hivi karibuni, likiripoti kuwa wanajeshi wa Ethiopian wamekuwa wakiwazuilia raia katika mji wa Humera, karibu kilomita 20 sawa na ( maili 12.5) kutoka mpakani, likisema hatua hiyo imechangia "kupungua kwa kiwango kikubwa idadi ya wakimbizi wanaowasili Sudan".

Data kutoka Shirika Umoja wa Mataifa la Kushughulikia Wakimbizi (UNHCR) zinaonesha idadi hiyo ilikuwa juu karibu Novemba 10, ambapo watu zaidi ya 6,800 walivuka mpaka na kuingia Sudan kwa siku moja. Idadi ya wakimbizi waliokuwa wakiingia nchini humo kwa siku ilikuwa 3,000, maafisa waliambia BBC. Hatahivyo, tangu vikosi vya Ethiopia kupelekwa katika eneo hilo la mpakani idadi ya wakimbizi wanaovuka mpaka na imeshuka hadi karibu 700 kwa siku.

The River Sittet
Maelezo ya picha, Mto Sittet uko katika mpaka wa Ethiopia na Sudan

Msichana mdogo aliye na umri wa miaka 11- ni miongoni mwa wakimbizi ambao wanazuiliwa. Alitoroka peke yake nyumbani, aliposikia milio ya risasi - bibi yake alikuwa mzee sana kutoroka.

"Nilikesha mwituni, niliingiwa na uwaoga sana. Si kuwa na nguo wala pesa," alisema. "Baadaye niliona mtu akiendesha tinga nikamuomba anisaidie na usafiri hadi mpakani."

Alipovuka mtu Sittet, alipeana namba ya simu ya baba yake. Baba na binti yake waliunganishwa katika kambi ya wakimbizi wa Um Raquba siku ya Jumatano. Baba yake, ambaye alizunguka naye katika kambi hiyo akimshika mkono, alisema alikuwa ameshuhudia watu wakipigwa risasi.

Ndani ya kipindi cha wiki tatu zaidi ya wakimbizi 43,000 wamekimbilia nchini Sudan, kwa mujibu wa UNHCR. Mashirika ya kutoa misaada yamekuwa yakijizatiti kuhudumia idadi ya inayozidi kuongezeka ya wakimbizi hao wa Ethiopia. "Misaada ya kibinadamu imeendelea kupungua," UNHCR ilisema, ikiongeaza: "Usaidizi wa dharura unahitajika."

Map of Tigray region

Mzozo huu unahusu nini?

Mwaka jana Bw Abiy alivunja muungano tawala , unaojumuisha vyama vilivyoundwa kwa misingi ya kikabila , na kuviunganisha katika chama kimoja, national party, the Prosperity Party, ambacho TPLF walikataa kujiunga.

Utawala wa Tigray unayaona mageuzi ya Bw Abiy kama jaribio la kujenga mfumo serikali moja na kuharibu mfumo uliopo sasa wa shirikisho.

Pia hukasirishwa na kile inachokiita urafiki wa waziri mkuu na rais wa Eritrea Isaias Afwerki "usiokuwa na kanuni "

Bw Abiy alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2019 kwa juhudi zake za kuleta amani kwa kumaliza mzozo wa muda mrefu wa nchi yake na Eritrea.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu anaamini kuwa maafisa wa TPLF wanahujumu mamlaka yake.

Bw Abiy alimuru mashambulio ya kijeshi dhidi ya TPLF baada ya kusema kuwa wapiganaji wake walikuwa wamevuka "mstari wa mwisho mwekundu".

Aliwashutumu kwa kushambulia kambi ya kijeshi ya vikosi vya shirikisho tarehe 4 Novemba. TPLF walikanusha kuishambulia kambi ya majeshi.

line

Maelezo zaidi kuhusu mzozo wa Tigray Ethiopia:

line