Mgogoro wa Tigray Ethiopia: Fahamu uwezo wa jeshi la Tigray

jeshi la Tigray limeapa kutetea eneo inalomiliki

Chanzo cha picha, Hisani

Maelezo ya picha, jeshi la Tigray limeapa kutetea eneo inalomiliki

Katika jimbo la Tigray nchini Ethioipia, vita vinaendelea kati ya majeshi ya serikali ya Ethiopia na wapiganaji wa chama cha TPLF.

Vita hivyo vimekuwa vikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili sasa huku vikosi vya Tigray vikidaiwa kurusha roketi katika mji mkuu wa jimbo la Amhara wa Bahir Dar na mji wa Gondar.

Vikosi vya Tigray pia vilirusha roketi katika mji mkuu wa Eritrea wa Asmara kulingana na kiongozi wa jimbo la Tigray Debretsion Gebremichael.

Lakini tunauliza je jimbo hilo lina uwezo gani wa kijeshi?

Ijapokuwa wachanganuzi wanasema kwamba eneo hilo halina uwezo wowote wa kijeshi , imedaiwa kwamba jeshi lake hivi karibuni lilishambulia wanajeshi wa seriikali.

vikosi maalum vya jeshi la Tigra

Chanzo cha picha, Hisani

Inakadiriwa kwamba utawala wa Tigray unaweza kumiliki wanajeshi 200,000 ikijumlisha wanajeshi wake na maafisa wa polisi katika eneo hilo.

''Jeshi hilo linashirikisha wanajeshi walioshambuliwa na wenzao wa serikali ya Ethiopia katika siku ya mwisho kwa kuwa lilikuwa jeshi kubwa lilomiliki silaha nyingi'' , alisema jenerali Dolaal Halhal akizungumza na BBC Somali.

Jenrrali huyo anaamini kwamba vita vinavyoendelea katika eneo hilo sio vita haswa. Amesema kwamba wanajeshi wa serikali ya Ethiopia wamekuwa wakiwasili karibu na jimbo hilo kutoka maeneo mbali mbali ya taifa hilo.

Wengine wanasema kwamba vita hivyo vilianza na kuifanya serikali kuondoa wanajeshi wake kutoka kambi tofauti katika maeneo mbalimbali ya taifa hilo.

Je wapiganaji wachama cha TPLF wana miliki silaha gani?

Huku wapiganaji hao wakifanikiwa kurusha makombora ya roketi kati miji na viwanja vya ndege nchini Ethiopia pamoja na taifa jirani la Eritrea, kumekuwa na maswali mengi kuhusu silaha zinazomilikiwa na jimbo hilo na zinakotoka.

Alipoulizwa na BBC Somali kuhusu chanzo cha kuwepo kwa silaha zinazotumika na wapiganaji hao, jenerali Dolaal alisema kwamba silaha hizo hazitoki kokote na kwamba tayari zilikuwa katika eneo hilo na zilichukuliwa na wapiganaji wanaounga mkono kujitenga kwa jimbo hilo kupigana na serikali ya Eritrea ambayo miaka ya nyuma ilikuwa ikikabiliana na Ethiopia.

'Thuluthi moja ya silaha zinazomilikiwa na wapiganaji hao zilisambazwa katika eneo hilo na jeshi la Ethiopia', aliongezea

waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Chanzo cha picha, Reuters

Je ni kwnaini Abiy Ahmed alitumia nguvu?

Serikali ya Ethiopia imeshutumu chama tawala cha jimbo la Tigray kukabiliana na wanamgambo katika eneo hilo. Katika hotuba iliorushwa mubashara na runinga alisema kwamba hatua ya kijeshi katika jimbo hilo imefaulu na itaendelea

Taarifa kutoka kwa waziri mkuu Abiy Ahmed ilisema : Wamevuka mpaka na njia ya pekee iliosalia ni kutumia nguvu ili kuokoa raia na taifa.

Ghasia katika eneo hilo zimesababisha wasiwasi katika jimbo la Tigray na sasa wengi wa raia wanaotorokea nchini Sudan pia wanakabiliwa na tisho la maambukizi ya corona.

Jamii ya kimataifa imetoa wito kwa pande husika kusitisha mapigano kwa lengo la kuweka amani.