Baada ya Trump, Biden atachukua hatua gani kuhusu Iran?

Viongozi wa Iran walisema sera zake hazitabadilika kutokana na matokeo ya uchaguzi wa Marekani

Chanzo cha picha, EPA

Rais mteule wa Marekani Joe Biden anasema mfumo wa kimataifa "ulikuwa unaelekea kusambaratika".

Ameahidi kuokoa sifa ya Marekani na amesema kuwa ana haraka. "Hakutakuwa na muda wa kupoteza,"aliandika katika jarida la masuala ya kigeni mapema mwaka huu.

Katika orodha ya mambo mengi anayopanga kufanya, ameahidi kuirudisha Marekani katika mkataba wa kimataifa wa nyuklia wa mwaka 2015- mpango wa pamoja wa utekelezaji unaofahamika kama (JCPOA), kuipatia jina lake rasmi, ikiwa suala hilo lililozua mjadala mkali wakati wa mtangulizi wa Donald Trump katika Ikulu ya White House Barack Obama, litapata ufanisi.

Tangu alipoiondoa Marekani katika mkataba huo mwezi Mei mwaka 2018, Rais Trump amefanya kila jitihada kuusambaratisha.

Lakini licha ya zaidi ya miaka miwili ya sera ya Bwana Trump ya "vikwazo kamili" dhidi ya Iran, nchi hiyo ya Kiislamu haijatetereka na inakaribia kupata teknolojia inayohitajika kuunda silaha za nyuklia kuliko wakati Marekani ilipoanza kuiwekea vikwazo.

Je, Joe Biden,ambaye ataingia mamlakani rasmi mwezi Januari mwakani, ataweza kuendeleza mpango huo? Ikizingatiwa hali ilivyo kwa sasa na mgawanyiko wa kisiasa unaoshuhudiwa nchini Marekani, je ataweza?

"Mpango huo uko wazi kabisa," anasema Aniseh Bassiri Tabrizi, mtaalamu wa Iran kutoka Taasisi ya London Royal United Services (Rusi). " lakini haitakuwa rahisi."

'Hakuna kurudi nyuma'

Ni sawa kusema kuna changamoto kubwa.

Mtandao tata wa vikwazo vya Marekani vya miaka miwili vinampatia Bwana Biden muda wa kutosha kuamua ikiwa ataitumia au la. Kufikia sasa amezungumzia hatua ya kuitaka Iran itakavyotekeleza JCPOA.

Tehran lazima irudie utekelezaji kamili wa makataba," aliandika mwezi Januari. Lakini hiyo tayari ni changamoto. Baada ya hatua ya Donald Trump kujiondoa Katika mkataba wa JCPOA, Iran ilianza kukiuka mkataba huo.

Iran iliamua kukiuka makubaliano baada ya kurejeshwa kwa vikwazo kulikofanywa na Donald Trump

Chanzo cha picha, WANA VIA REUTERS

Katika ripoti yake ya robo ya mwaka, Shirika la kimataifa la nguvu za atomiki (IAEA) limesema vifaa vyake vimeundwa kwa kiwango cha madini ya urani mara 12 kuliko kiwango kilichowekwa na JCPOA

Pia ilikuwa imeanza kuzalisha madini ya urani kwa kiwango cha juu zaidi ya asilimia 3.67 tofauti na yale yaliyofikiwa katika mkataba wa nyuklia.

Wakati huenda ukahoji kuwa haya ni masuala ambayo utekelezaji wake ni rahisi ukiamua kufanya kazi na maafisa wa Iran- Maafisa hao wamesema mara kadhaa kwamba hatua ya kutozingatia mkataba ni mambo ambayo yanaweza kuangaziwa upya - hatua iliyopingwa na watafiti wa Iran haiwezi kufutiliwa mbali kirahisi.

"Hatuwezi kurudi nyuma," anasema Ali Asghar Soltanieh, balozi wa zamani wa Iran katika shirika la IAEA. "Sasa tumetoka herufi A na kwenda B, na hapo ndipo tulipofika."

Shinikizo la kisiasa

Lakini Iran, ambayo imeweza kuhimili dhoruba ya Trump, ina masharti yake. Maafisa wanasema kuondolewa kwa vikwazo pekee haitoshi. Iran inatarajia kulipwa fidia ya miaka miwili na nusu ya kulemazwa kwa uchumi wake.

Iran inapojiandaa kuanza uchaguzi wake mwezi Juni mwaka ujao, viongozi wanaopigania mageuzi wameanza mikakati ya kuwania nyadhifa mbali mbali.

Umaarufu wa Rais Hassan Rouhani umeshuka kutokana na hali mbaya ya uchumi.

Thamani ya sarafu ya Iran imeporomoka na mfumuko wa bei umeongezeka

Chanzo cha picha, EPA

Je, Joe Biden ataona umuhimu wa kuimarisha nafasi ya Bwana Rouhani kwa kuanza na kulegeza vikwazo dhidi ya Iran?

Nasser Hadian-Jazy, Profesa wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Tehran, anasema Joe Biden anastahili kuweka wazi mpango wake kuhusu Iran kabla ya kuingia rasmi ofisini.

"Ujumbe wa hadhara kwamba atarejea katika mkataba wa JCPOA, bila masharti, haraka iwezekanavyo," anasema. "Hiyo inatosha."

Rais Hassan Rouhani amesema Iran itatumia "fursa yoyote" kuondosha shinikizo la vikwazo

Chanzo cha picha, EPA

Asipofanya hivyo, anaongeza kuwa, huenda akawakaribisha ''waharibifu" nchini Iran, na kuharibu nafasi ya Marekani katika ushawishi wa eneo zima la Mashariki ya Kati.

Hata hivyo katika miji ya London, Paris na Berlin, kuna dhana kwamba ulimwengu umesonga mbele na kwamba kujiunga tena kwa Marekani katika mkataba wa awali huenda isiwe hivyo.

Lakini Bwana Biden mwenyewe anakabiliwa na changamoto , ni vipi anaweza kushughulikia suala la Iran? .Uungwaji mkono wa mpango wa pamoja wa utekelezaji wa JCPOA nchini Marekani umekumbwa na mgawanyiko huku Warepublican wakiupinga.