Je ni kwanini Barack Obama anasema uchaguzi mmoja hautazuia 'ukweli wa uozo' wa Marekani?

Marekani inakabiliana na jukumu kubwa la kubadilisha utamaduni wa kipuuzi wenye nadharia ya kuigawa nchi, Barack Obama amesema.
Maelezo ya picha, Marekani inakabiliana na jukumu kubwa la kubadilisha utamaduni wa kipuuzi wenye nadharia ya kuigawa nchi, Barack Obama amesema.

Katika mahojiano na BBC, rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amesema Marekani imegawanyika zaidi zaidi ya miaka mine iliyopita, wakati ambao Donald Trump alishinda urais.

Na Obama ameeleza kuwa ushindi wa Joe Biden katika uchaguzi wa urais kwa mwaka huu ni mwanzo wa kufanya marekebisho mgawanyiko huo.

"Itachukua zaidi ya uchaguzi mmoja kufanya mabadiliko katika mwenendendo huo," alisema.

Kukabiliana na mgawanyiko wa taifa, si jambo la kuwaachia wanasiasa pekee lakini pia ni jambo linalohitaji kubadilika kwa mifumo na usikivu wa watu- ili kuafikiana katika lengo moja kabla ya kuanza kulumbana nini cha kufanya dhidi ya wale.

Hata hivyo amesema ana matumaini chanya katika kizazi kijacho, amesema vijana wanaweza kubadilisha dunia kwa kusaidia kubadilisha mtazamo huo kwa makini na kuwa sehemu ya mabadiliko.

Mgawanyiko uko vipi Marekani?

"Hasira na chuki kati ya watu wanaoishi mjini na vijijini, wahamiaji, kukosekana kwa haki kama usawa na nadharia nyingine za kipuuzi - ambazo baadhi zimeitwa kuongezeka kwa ukweli zimewekwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini Marekani na mitandao ya kijamii ", Bwana Obama amemwambia mwanahistoria David Olusoga, katika mahojiano na BBC.

"Tumegawanyika sana kwa sasa, ni zaidi ya nilipoingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 2008," rais wa zamani ameeleza.

Ameeleza kuwa hii ni kwasababu "Trump alikubali mgawanyiko huo na aliufurahia kwa kuwa lilikuwa ni jambo zuri kwa matakwa yake ya kisiasa".

Jambo lingine ambalo limechangia jambo hili kwa sehemu kubwa, Obama amesema , ni ongezeko la taarifa zisizo za kweli kwenye mitandao ya kijamii na ukweli kutotiliwa maanani.

Kuna mamilioni ya watu ambao wanadhani kuwa Joe Biden ni mfuasi wa ujamaa, kuna ambao wa nadharia kuwa Hillary Clinton alikuwa anajihusisha na masuala ya ushetani yanayohusiana pete za 'ulawiti '," alisema.

Mifano aliyotumia kuhusu bi Clinton ilihusiana na nadharia feki kuhusu wanasiasa wa Democratic wanaoongoza kwa kutumia nguvu za pete nje ya mgahawa wa pizza, mjini Washington.

"Nadhani kwa kiasi fulani tunahitaji kuangalia ukweli wa mambo kabla ya kuanza kubishana kuhusu madai hayo potofu."

Bwana Obama alisema Joe Biden, ana vigezo ambavyo Marekani inahitaji kwa rais wake kwa sasa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bwana Obama alisema Joe Biden, ana vigezo ambavyo Marekani inahitaji kwa rais wake kwa sasa

Bwana Obama ameelezea juu ya ubora wa Biden wakati kuna taarifa nyingi zenye utata katika vyombo vya habari ,miaka ya hivi karibuni jitihada za kusambaza habari ghushi zimekuwa kubwa na kueneza uongo kwa kiasi kikubwa duniani lakini alisisitiza kuwa ukweli umepata njia yake tayari.

Alisema tatizo la mgawanyiko ni kutokana na sababu za kijamii na kiuchumi ambazo zinaongeza ukosekanaji wa usawa na mgawanyiko wa mjini na vijijini.

Masuala kama hayo duniani kote yanawafanya watu kuhisi kuwa wanapoteza muelekeo.

Tatizo la taarifa ghushi ni umaarufu wake

Nadharia ya taarifa za uongo zimeongezeka sana wakati wa utawala wa Trump.

Hii ni kwasababu taarifa za uongo hazina ukomo katika intaneti. Zinahamasishwa na watu maarufu na wenye wafuasi wengi duniani -kama wale wenye wadhifa mkubwa duniani hata wale walioko White House.

Dunia inayoendeshwa kwa intaneti -ambapo kile kinachoangaliwa ni maoni ya watu na sio ukweli, na tunachagua kabila letu.

Hii imeweza kuanzisha msingi wa taarifa ghushi kuonekana bora zaidi.

Ongezeko la watu katika matumizi ya mitandao ya kijamii kufanya uchunguzi wao kunawasababishia kuja na hitimisho la kupotosha.

Kama Barack Obama alivyoainisha , huu uongo na madai ya kupotosha - haswa yakitolewa na vyombo vya habari au watu mashuhuri au maarufu unaonekana kuwa ndio ukweli wenyewe.

Suluhisho si kuwasilisha ukweli tu - ni muhimu kuwa ibaki hivyo.

Ni muhimu kuelewa namna watu wanavyoamini taarifa hizo za uongo mtandaoni mara kwa mara .

Huwa naongea na waathirika wa nadharia potofu mtandaoni mara kwa mara kuhusu athari iliyojitokeza na mgawanyiko uliosababishwa.

Hii inanionesha jinsi ilivyo ngumu kurekebisha athari iliyojitokeza.

Vipi kuhusu suala la ubaguzi?

Obama, ambaye aliweka historia kwa kuwa rais wa kwanza Marekani amesema suala la ubaguzi limekuwa kitovu cha mgawanyiko katika historia ya Marekani.

Kifo cha George Floyd: Kipi kilibadilika katika siku 100 baadae?
Maelezo ya picha, Kifo cha George Floyd: Kipi kilibadilika katika siku 100 baadae?

Matukio ambayo yalitokea kipindi cha kiangazi likiwemo la kifo cha George Floyd - mwanaume mweusi aliyeuawa katika mikono ya polisi - na jinsi jamii ilivyoshutumu kitendo kile Marekani na hata duniani kote, kiliweza kuleta mwanya wa kujitafakari na kufanya mabadiliko.

"Licha ya uwepo wa mgawanyiko na upendeleo katika mfumo wa sheria na haki... maandamano yaliyoonekana kutoka kwa wanaharakati yaliweza kuleta matumani makubwa ya mabadiliko."

  • Unaweza pia kusoma: