Uchaguzi Marekani 2020: Obama amsuta Trump kwamba anachukulia urais kama kipinndi cha televisheni

Barack Obama amemshutumu Donald Trump kwa kuchukulia urais kama "onyesho la kipindi cha televisheni ", katika hotuba aliotoa kwenye kongamano la cha Democratic.
Rais huyo wa zamani wa Marekani amesema kuwa mwenzake aliyemrithi, wa chama cha Republican ''hajapata uzoefu wa kazi ya urais kwa sababu hawezi.''
Akiwa Ikulu ya White House, Bwana Trump amejibu kwa kusema kuwa yeye alichaguliwa kwa sababu ya 'hofu' Bwana Obama alioacha Marekani.
Usiku huu wa tatu wa mkutano wa chama cha Democrat, Kamala Harris amekubali uteuzi wake kama makamu wa rais.
Katika kilele kamili cha kongamano hilo la siku nne mgombea urais kwa chama cha Democrat Joe Biden atatoa hotuba yake siku ya Alhamisi.
Tiketi hii ya Biden- Harris itakua ni ushindani dhidi ya Rais Trump na makamu wa rais Mike Pence katika uchaguzi wa Novemba 3.
Janga la Corona limelazimisha chama cha Democrat kuachana na mbwembwe na shamrashamra ambazo hutokea wakati wa mikutano ya aina hiyo, na kulazimika kufanya mkutano kupitia mtandao ambapo hotuba ama zinarekodiwa kabla au zinatolewa kwa njia ya moja kwa moja.
Obama alisema nini?
Jumatano usiku, Bwana Obama alitoa shambulio lake kali zaidi dhidi ya Bwana Trump, akizungumza moja kwa moja kutoka Jumba la kumbukumbu ya Mapinduzi ya Marekani huko Philadelphia.
Alisema. "Hajaonesha [Bwana Trump] ari yoyote ya kutia bidii katika kazi yake. Hajaonyesha nia ya kupata makubaliano".
"Hajaonyesha nia ya kutumia nguvu za ofisi hiyo kusaidia yeyote zaidi ya yeye mwenyewe na rafiki zake".
"Hana nia yoyote ya kuchukulia urais zaidi ya kama kipindi kingine cha televisheni ambacho anaweza kukitumia kupata umaarufu anoutaka sana".
Amesema kuwa athari za urais wa Trump zimekuwa,"msukumo wetu mbaya zaidi kujitokeza, ufahari na sifa zetu kote ulimwenguni zimepotea vibaya, na taasisi zetu za kidemokrasia zimetishiwa jinsi haijawahi kutokea awali.
Bwana Obama amezungumzia, "matukio mengi, ubinafsi, ukosefu wa ubinadamu na nadharia za uwongo".
"Musiwaruhusu wachukue nguvu yanu," akasihi wapiga kura wa Marekani. "Musiwaruhusu wachukue demokrasia yenu."
Bwana Obama kisha akageukia kuanza kuwahimiza wapiga kura kumchagua aliyekuwa makamu wa Rais Bwana Biden ambaye amesalia na siku 76 zijazo -huku akimsifu kuwa 'rafiki yangu' na 'ndugu yangu'
Kulingana na shirika la habari la Associated Press, vyanzo vya karibu na Bwana Obama vinasema kuwa anamuunga mkono kikamilifu Bwana Biden, lakini ana wasiwasi kuhusu ushiriki kati ya wapiga kura vijana na haswa wapiga kura.
Marais wa zamani wa Marekani wengi huamua kwa heshima kutozungumza juu ya wanaowarithi.
Lakini Bwana Obama alionya miaka minne iliyopita, akiwa bado ofisini kuwa atachukulia kama. 'matusi kwake binafsi' iwapo Wamarekani watamchagua Bwana Trump aliyekuwa wakati huo mgombea wa chama cha Republican na nyota wa kipindi cha Televisheni cha "The Apprentice".
Rais huyo wa 44 amezidi kuzungumza kwa uwazi kuhusu aliyemrithi baada ya kumtazama akiharibu alichokiacha kama urithi kwa Wamarekani.

Siku ya Jumatatu wakati wa kongamano la Demokrat, Mitchelle Obama alitoa hotuba iliyomshambulia mrithi wa mume wake, akimuonesha kuwa kama mtu asiyejua kazi yake na "anayejigamba". Hili liliwashangaza Wamarekani wengi kwasababu sio kawaida wake wa rais wanaotawala na waliokuwa uongozini kuzungumzia masuala ya siasa moja kwa moja.
Trump alijibu nini?
Wakati wa mkutano na wanahabari siku ya Jumatano katika Ikulu ya Marekani, Bwana Trump aliulizwa juu ya matamshi ya Rais Obama.
"Naona hofu kuu aliotuachia na upuuzi wa shughuli miamala alizofanya", rais wa Marekani alisema hivyo.
"Tazama alivyokuwa mbaya, alivyokuwa rais asiyejua kufanya kazi yake, alikuwa hajui cha kufanya, utenda kazi mbaya."

"Sasa rais Obama hakufanya kazi nzuri, na sababu niko hapa ni Rais Obama na Joe Biden."
Aliongeza: "Walifanya kazi mbaya sana mpaka niko hapa sasa mbele yenu kama rais."
Kwenye ukurasa wake wa Twitter, Bwana Trump aliandika, "Karibu, Barack na Hillary mpotovu. Tuonane ulingoni!"
Rais anatarajiwa kukubali uteuzi wake tena kama mgombeaji wa Republican kutoka kwa bustani ya White House wiki ijayo wakati wa kongamano la chama chake.
Nani mwengine aliyezungumza katika mkutano huo?
Nani mwengine aliyezungumza katika mkutano huo?

Chanzo cha picha, BBC Sport
Jumatano usiku, Hillary Clinton, aliyekuwa mgombea urais wa chama cha Democrat mwaka wa 2016 pia alimshambulia mtu aliyekatiza matumaini yake ya kuingia White House.
Akizungumza kutoka nyumbani kwake huko Chappaquiddick, New York, alisema: "Ninatamani kuwa Donald Trump angekuwa rais bora. Lakini cha kusikitisha ni kwamba yuko jinsi alivyo."
Hillary aliyekuwa mke wa rais na waziri wa mambo ya nje wa Marekani, aliongeza kusema, "Kwa miaka mine, watu wameniambia, 'Sikutambua jinsi alivyo mtu hatari'. 'Natamani ningeweza kurudi nyuma na kufanya tena maamuzi.' Au hata, 'Ningepiga kura.'
"Naam, hii haiwezi kuwa tena kuwa ninge, ninga, nita."
Aliongeza: "Pigeni kura kana kwamba maisha yetu yamo hatarini, kwa sababu yamo."
Urithi wa Obama na Donald Trump
Barack Obama na Donald Trump wanabadilishana cheche za maneno wakati halisi sasa. Wakati rais wa zamani amewahi kumkosoa nyakati za awali, katika hotuba yake ya kongamano la Kitaifa la chama cha Democratic usiku, amemshambulia rais wa sasa kwa jina.
Kwa zaidi ya miaka mitatu, Trump ameuchukua uchaguzi wa 2016 - ambao alishinda kwa kiasi kidogo - kama mabadiliko kamili ya mtangulizi wake na kutawaliwa ipasavyo.
Hili limekuwa wazo hatari, ukizingatia kwamba kura za maoni zinamuonesha Bwana Obama kwa sasa ni mmoja wa watu maarufu katika siasa nchini humo, wakati Bwana Trump sifa nzuri za kuvutia kwa kipindi kirefu cha urais wake.
Mzozo wa Jumatano unaonyesha kwamba uchaguzi ujao kati ya Bwana Trump na Joe Biden, Wamarekani watakuwa wakifanya uchaguzi sio tu kati ya watu wawili, bali pia utakuwa kati ya utawala Obama na Trump.
Na wote rais wa sasa na wa zamani wanachukua mchakato huu kwa dhati.













