Vyakula vya mwisho kuagizwa na wafungwa waliohukumiwa kunyongwa Marekani

Ili kuelewa mfumo wa hukumu ya kunyongwa nchini Marekani, mpiga picha Jackie Black ameweka pamoja picha za vyakula vilivyoagizwa na wafungwa kabla ya kunyongwa.

Chakula cha Chipsi ,vibanzi, mayai ya kukaanga na tosti y amkate

Chanzo cha picha, Jackie Black

Maelezo ya picha, Chakula cha mwisho kilichoagizwa na Clydell Coleman, aliyenyongwa Mei 5 1999

"Ushawahi kujiuliza ukiambiwa uagize chakula chako cha mwisho duniani kabla ya kunyongwa kutokana kosa ambalo huenda umefanya au haukufanya utaagiza nini?" anauliza mpiga picha katika mradi wa sanaa .

"Pengine tukiweka mawazo yetu mbele ya chakula hicho tunaweza kupata taswira kamili.

"Pengine tunaweza kujiuliza madhumuni ya hatua hiyo katika mfumo wa haki ni nini?

"Pengine tunaweza kujipata tukimhurumia mfungwa aliyejipata katika hali kama hiyo."

Mpiga picha Black pia alikusanya taarifa kuwahusu wafungwa hao, ikiwa ni pamoja na muda waliozuilwa gerezani, kiwango chao cha elimu, kazi zao na tamko lao la mwisho kabla ya kunyongwa.

David Wayne Stoker

A meal featuring two burgers, french fries and ice cream

Chanzo cha picha, Jackie Black

Alinyongwa: Juni 16 1997

Masomo: Miaka minane

Kazi: Seremala

Kauli ya mwisho: "Nasema pole kwa kumpoteza mpendwa wako... lakini sikumuua mtu yeyote."

2px presentational grey line

Anthony Ray Westley

A meal featuring french fries, fried chicken and white bread

Chanzo cha picha, Jackie Black

Alinyongwa: Mei 13 1997

Masomo: Miaka minane

Kazi: Kazi ya mikono

Kauli ya mwisho: "Nataka mjue kwamba mimi sikumuua mtu yeyote. Nawapenda nyote."

2px presentational grey line

Thomas Andy Barefoot

A meal featuring, beans, rice, sweetcorn, crackers and cola

Chanzo cha picha, Jackie Black

Alinyongwa: Oktoba 30 1984

Masomo: Haijaorodheshwa

Kazi: Mhudumu katika kisima cha mafuta

Kauli ya mwisho: "Natumaini kwamba siku moja tutatafakari maovu tunayofanya sasa kama uchawi. Nataka kila mtu ajue kwamba sina kinyongo. Natumani kila mmoja niliyemkosea atanisamehe.

"Nimekua nikiombea siku nzima roho ya mke wa [mhasiriwa] ipate utulivu na kuondokana na chuki kwa sababu chuki aliyonayo rohoni mwake inaweza kumpeleka motoni mtu mwingine. Naomba msamaha kwa kila jambo baya nililomfanyia mtu yeyote. Natumani watanisamehe."

2px presentational grey line

James Russell

A red apple

Chanzo cha picha, Jackie Black

Alinyongwa: Septemba 19 1991

Masomo: Miaka 10

Kazi: Mwanamuziki

Kauli ya mwisho: Inaripotiwa lilidumu kwa dakika tatu, huenda haikurekodiwa ama halikutafsiriwa.

2px presentational grey line

Jeffrey Allen Barney

A bowl of cereal with milk, a milk carton and two packets of Frosted Flakes

Chanzo cha picha, Jackie Black

Alinyongwa: Aprili 1986

Masoma: Haikuorodheshwa

Kazi: Haikuorodheshwa

Kauli ya mwisho: "Naomba msamaha kwa kosa nililofanya. Nastahili adhabu hii. Yesu nisamehe."

2px presentational grey line

Johnny Frank Garrett

A bowl of chocolate and strawberry ice cream

Chanzo cha picha, Jackie Black

Alinyongwa: Februari 11 1992

Masomo: Miaka saba

Kazi: Mfanyakazi wa mikono

Kauli ya mwisho: "Nataka kutoa shukurani kwa familia yangu kwa kunipenda na kunijali. Na kwa watu wengine duniani mtajua wenyewe."

2px presentational grey line

William Prince Davis

A meal featuring chicken nuggets, rolls, beans, crisps and cola

Chanzo cha picha, Jackie Black

Alinyongwa: Septemba 14 1999

Masomo: Miaka saba

Kazi: Kuezeka nyumba

Tamko la mwisho: "Ningelipenda kusema pole sana kwa familia yangu kutokana na machungu niliyowasababishia kutokana na kitendo changu... Ningelipenda pia kuwashukuru wanaume wote waliohukumiwa kifo kwa jinsi walivyonionesha upendo miaka yote tuliojumuika pamoja.

"Natumani kutoa sehemu ya mwili wangu kama msaada wa kutumiwa katika utafiti wa kisayansi itakayomfaa mtu... Sina mengine ya kusema, na kwa wahudumu wa magereza, samahani nikimalizia nauliza vipi na wale vijana wachungaji ng'ombe?"

2px presentational grey line

Gerald Lee Mitchell

A packet of sweets

Chanzo cha picha, Jackie Black

Alinyongwa: Oktoba 22 2001

Masomon: Miaka 10

Kazi: Seremala

Tamko la mwisho: "Naomba msamaha kwa machungu niliyowasababishia. Naomba msamaha kwa kumuua mpendwa wenu. Namuomba Mungu anisamehe. Na pia nawaomba mnifanyie hivyo. Najua itakuwa vigumu. Lakini naomba msamaha kwa kitendo nilichofanya.

"Kwa familia yangu,Nawapenda kila mmoja wenu. Jipeni nguvu. Nitawapenda daima, na milele. Najua kwamba naenda kuwa Baba. Toeni machozi ya furaha kwa ajili yangu."

2px presentational grey line

Robert Anthony Madden

An image with the words: "Asked that final meal be given to a homeless person. (Request denied)."

Chanzo cha picha, Jackie Black

Maelezo ya picha, Aliomba chakula chake kipewe mtu asiyekua na makao- (ombi lilikataliwa)

Alinyongwa: Mei 28 1997

Masomo: Miaka 12

Kazi: Mpishi

Kauli ya mwisho: "Naomba msamaha kuwa kuwapoteza wapendwa wenu. Lakini sikuhusika na mauaji ya watu hao. Natumani kuwa tutajifunza kitu kuhusiana na suala hili. Na pia tutakomesha chuki na kisasi na kuthamini masuala yalio na umuhimu katika dunia hii.

"Namsamehe kila mtu aliyehusika na mchakato huu, ambao nahisi una makosa."

2px presentational grey line

James Beathard

A meal featuring lettuce, onion rings, french fried, carrots and chicken nuggets

Chanzo cha picha, Jackie Black

Alinyongwa:Disemba 9 1999

Masomo: Miaka 15

Kazi: Fundi makanika wa pikipiki

Baada ya hukumu dhidi yake kutolewa, shahidi mkuu upande wa mashitaka alibadilisha kauli katika hatua ambayo iliwafanya wanachama watatu wa bodi ya kutathmini makosa kupendekeza achukuliwe hatua kwa niaba yao.

Kauli ya mwisho:"Nataka kuanza kwa kukubali upendo ambao nimekuwa nao katika familia yangu. Hakuna mwanaume katika ulimwengu huu ambaye amekuwa na familia bora kuliko mimi. Nilikuwa na wazazi bora zaidi duniani. Sijawahi kujivunia mtu yeyote duniani kuliko binti yangu na mwanangu wa kiume.

"[kuna] mambo machache ambayo ningelipenda kusema kwasababu huu tu ndio wakati ambao watu watasikiliza kile nitakachosema. Marekeni imefikia [mahali] ambapo sasa [hakuna] haiheshishimu maisha ya binadamu. Kifo changu ni dalili tu ya ugonjwa. Wakati umewadia kwa serikali kukomesha maovu inayofanyia nchi zingine na kuua watoto wasiokua na hatia. Vikwazo vinavyoendelea dhidi ya mataifa kama vile Iran na Iraq, Cuba na nchi mengine - havifanyi lolote kubadilisha ulimwengu na vinaumiza watoto wasio na hatia.''

"Siku moja ulimwengu utajua ukweli, na watu watajua nini kilichofanyika, [alimradi]tunaunga mkono uhuru wa habari. Naona jinsi vyombo vya habari vinavyojaribu kujiweka kama taasisi huru."

Chakula cha mwisho cha wafungwa katika makavazi ya sanaa ya Parrish, mjini New York, hadi Januari 31, 2021.

Picha zote zina hati miliki.