Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Kwa nini baadhi ya Wakenya hawaamini kuna corona
Katika mfululizo wa barua kutoka kwa waandishi wa Afrika, Waihiga Mwaura anauliza kwa nini baadhi ya Wakenya hajachukulia kwa uzito unaostahili uwepo wa virusi vya corona ambavyo vimetikisa ulimwengu mzima.
Licha ya data ya wanasayansi duniani kuonesha kwamba ugonjwa wa Covid-19 ni hatari, na umesababisha vifo vya karibu watu 600,000, nchini Kenya ukitangaza hadharani umeathirika na virusi hatari vya corona huenda ukadhaniwa kwamba unatafuta sifa ama unatumiwa na serikali ''kufanya kampeini ya uwongo''.
Dahana hii ilianza na Ivy Brenda Rotich, mgonjwa wa kwanza wa Covid-19 kutoka hospitali baada ya kupewa matibabu mwezi Aprili.
Bi Rotich alikosolewa vikali katika mitandao ya kijamii kama mtu ambaye alitumiwa na serikali kuwashawishi Wakenya kwamba ugonjwa wa Covid-19 ni wa kweli, ili ipate fedha kutoka kwa wafadhili, kukabiliana na virusi vya corona.
Wakati huo Covid-19 ulichukuliwa kuwa ugonjwa wa kigeni na kwamba Waafrika walidhaniwa hawawezi kupatika na ugonjwa huo.
Mpaka sasa licha ya watu 11,000 kuthibitishwa kuwa na Covid-19 na wengine 200 kufariki nchini Kenya kutokana na ugonjwa huo, kuna baadhi ya watu ambao hawaamini uwepo- kwa mfano mtu aliyenioshea gari langu wiki iliyopita alisisitiza ni uwongo mtupu unaoenezwa na wanahabari akidai kuwa ni mafua ya kawaida tu ambayo inachukua muda mrefu kupona.
Hivi majuzi mhubiri mashuhuri Robert Burale alilaumiwa kwa kudanganya kuwa anaugua ugonjwa wa Covid-19 licha picha zinazomuonesha akiwa amelazwa hospitali kusambaa mitandaoni.
Nae Benson Musungu, Mkurugenzi wa masuala ya vijana katika ofisi ya ya chama cha Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga, Orange Democratic Movement, alisingiziwa kwamba amekuwa akipokea kitita kikubwa cha fedha kutoka kwa serikeli ili kutangaza hadharani alipokea matibabu kwa siku 15 katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali moja jijini Nairobi.
Dhana hizi za kusikitisha zimewafanya manusura wengi wa ugonjwa wa Covid-19 kusalia kimya kwa kuhofia kushambuliwa mitandaoni.
'Wabunge wachochea dhana'
Wanasiasa na viongozi wengine walio na ushawishi na ambao baadhi yao pia wameambukizwa virusi vya corona wameamua kukaa kimya, pengine kwa kuhofia kunyanyapaliwa.
Kutokana na hilo, ni manusura wachache na wapendwa wao ambao wanajitokeza kutangaza hadharani kuhusu hali yao, huku maswali yakiulizwa katika mitandao ya kijamii: "Je wewe au jamaa zako wanamjua mtu yeyote aliyepatika na ugonjwa wa Covid-19?"
Na kwa wengine jibu ni la sijamuona: "La."
Kilichoongezea cheche za moto dhana hiyo potofu,ni hatua ya Mbunge jude Njomo mapema mwezi Julai kusema mbele ya kamati ya bunge jinsi familia yake ulivyopata usumbufu wa kiakili baada ya mama yake kupatikana na virusi vya corona siku nne baada ya kifo chake, hali iliyowalazimu kumzika ghafla nyakati za usiku.
"Nilijaribu kuwarai watupatie muda kidogo, laki tulipokea simu karibu saa tisa tukitakiwa tumzike haraka iwezekanavyo, kwa kuwa hatukua na budi tulimzika saa mbi usiku. Tunahisi hatukumpatia heshima za mwisho kusherehekea miaka 82 aliyoishi duniani " Bw. Njomo taliambia kituo cha runinga cha kibinafsi, Citizen TV.
Bw. Njomo anasema baadae familia yake ililazimishwa kufanyiwa uchunguzi maalum katika kituo cha kitaifa cha Influenza na katika Hospitali ya Nairobi na matokeo hayakuonesha wana virusi
Japo nchi imeanza kulegeza mashariti ya usafiri na kurejelea shughuli za kiuchumi, sehemu ya jamii ya Wakenya haijaamini kuwepo kwa ugonjwa huo.
Baadhi ya watu wameamua kuamini suala zima la ugonjwa wa corona ni njama inayoendeshwa na serikali hali inayolemaza juhudi za serikali kukabiliana na kuenea kwa maambukizi.
Kwa mujibu wa Profesa Omu Anzala, mtaalamu wa magonjwa yanayoambukizwa kupitia virusi katika Chuo Kikuu cha Nairobi, utamaduni wa Afrika ni miko kuangazia masuala ya afya hasa yale yanayohusiana na ugonjwa .
Kwa mfano Rais naweza kuwa mgonjwa kwa miaka mingi lakini ugonjwa wake utafanywa kuwa siri na kiongozi huyo atasafiri kimy akimya nje ya nchi kwenda kutafuta matibabu na hali yake ya afya haitawahi kuwekwa wazi kwa umma, wala kwa wafanyakazi wake.