Virusi vya corona: Jinsi unyanyapaa unavyoathiri makabiliano dhidi ya corona Afrika

Unyanyapaa unaweza kufanya ikawa vigumu kupata takwimu kamili ya wanaokufa kwa virusi vya corona.

Jinsi alivyozikwa mwanaume aliyekua kwa virusi vipya ya corona magharibi mwa kenya kumedhirihisha kiwango kikubwa cha unyanyapaa kwa wanopatikana na ugonjwa Covid-19 barani Afrika.

Na pia kumezua wasiwasi kwamba watu huenda wakawa na hofu na uwongo wa kujitokeza kwa hiari kupimwa na kupata matibabu. Hilo linatokana na ukosefu wa kuchukua hatua za busara na serikali katika kukabiliana na wagonjwa wa Covid-19 na familia zao.

Unyanyapaa huo pia unajumuisha kuvamiwa kwa wahudumu wa afya na wtu wanaoshukiwa kuambukizwa virusi vya corona, na kurejesha kumbukumbu za yaliyoshhudiwa wakati wa janga la ugonjwa wa ukimwi lilipokuwa limefia kilele chake miaka ya 1990.

Unyanyapaa unaweza kuwa moja ya changamoto kubwa ya kijamii katika serikali barani Afrika wakati zinakabiliana na covid-19. Pia inaweza kuwa vigumu kujua takwimu sahihi za maambukizi mapya, kufuatilia walioambukizwa na hatua zilizochukuliwa kama njia ya kukabiliana na maambukizi hayo

Matendo ya chuki dhidi ya raia wa China

Wakati kisa cha kwanza cha Covid-19 kilipothibitishwa katika baadhi ya sehemu Afrika, kulishuhudiwa uvamizi au na matendo ya chuki dhidi ya raia wa China na wenye asili ya Asia.

Kenya na Ethiopia zilikosolewa kwa kuendelea kutoa huduma za ndege hadi nchini China.

Raia a Nigeria waliandamana dhidi ya uamuzi wa serikali wa kupeleka madaktari kutoka China nchini

Radio Biafra, kituo cha redio cha siri kinachopigania kujitenga kwa eneo la kusini mashariki mwa Nigeria, kilisema China imedhamiria kusambaza ugonjwa huo kote ulimwenguni. Baadhi ya wasikilizaji w akituo hicho walidai kuwa vifaa vya matibabu vilivyotolea kama msaada na China kwa nchi hiyo vilikuwa na sumu.

"Inaoneka China imejipanga kuchukua uongozi Duniani. Hiyo ndio sababu imetengeza vifaa vingi vya matibabu ambavyo ni ghushi ili kulemaza uchumi wa nmataifa mengine na kupunguza idadi ya watu hususan Afrika," amsikilizjai mmoja alisema.

Afrika Kusini ilikosolewa kwa kurejesha zaidi ya raia wake 100 kutoka mji wa Wuhan kitovu cha ugonjwa wa Covid-19.

Majadiliano ya kuweka wazi taarifa za wagonjwa

Watu wamegawanyika kuhusu ikiwa majina ya walioambukizwa virusi vya corona wanastahili kutajwa na kuwekwa wazi kwa umma ili iwe rahisi kufuatilia.

Chama cha wanahabari nchini Ghana kimeonya kwamba kuweka wazi taarifa za walioathirika kutafanya wawe katika hatari ya kuchukiwa na kunyanyapaliwa.

Nchini Liberia, hoja hiyo ilisababisha mtafaruku kati ya maafisa waandamizi baada ya mwanamke aliyepatikana na virusi vya corona kujificha kw ahofu ya kunyanyapaliwa.

Mmoja kati ya wagonjwa wa awali kupona kutokana na ugonjwa wa Covid-19 nchini kenya alianza kudhalilishwa mitandani licha ya vyombo vya habari kumuangazia kama shujaa.

Wonjwa na wahudumu wa afya Afrika Kusini amezema kwamba unyanyapaa umewaathiri pakubwa katika afya ya akili.

"Hata wakati huu kama mtu aliyepona ugonjwa wa Covid-19, bado napata mfadhaiko, tunahitaji kuwa na washauri ili kupona. Licha ya kwamba tumenusurika na ugonjwa wenyewe bado tunatatiziko kiakili, hujapona kutokana na unyanyasaji," mgonjwa alizungumza na tovuti ya ENCA Afrika Kusini.

Kutoamini vituo vya afya

Wahudumu wa afya wamehtumiwa kwa kupuuza wagonjwa wa Covid-19, kwa mujibu wa BBC Monitoring

Hali ya vituo vya afya na utayarishaji wa wafanyakazi wa afya kuhusu namna ya kushughulikia wagonjwa wa Covid-19 pia kumechangia watu kutokuwa tayari kutafuta matibabu.

machi, mwanamke wa Afrika Kusini alijiua akiwa katika karantini kwenye kituo kimoja cha matibabu magharibi mwa Kenya. Kituo cha habari cha Citizen nchini kenya, kilisema kwamba mwanamke huyo alikuwa akilalamikia hali mbaya katika kituo cha karantini.

Mwanamuziki mmoja nchini Gabon alisemekana kutoroka kutoka kituo cha afya katika mji huo kwasababu ya kukosa matibabu bora.

"Nimekuwa hopitali kwa karibia siku 10 na nisema hivyo kwasabau sikuwahi kupata matibabu yoyote, sikuona haja ya kuendelea kukaa kwenye hospitali hiyo. Hakuna aliyenipa hata nusu kipande cha paracetamol. Kwahiyo hakukuwa na haja ya kuendelea kuwepohospitalini. ikiwa unasema nimepata ugonjwa wa Covid-19 basi aanza kunitibu," mwanahabari huyo alisema kwenye vide iliyosambaa mtandaoni.

Familia moja nchini Kenya ilidai kwamba kijana wao ambaye alipimwa akapatikana hana virusi vya corona, alikufa baada ya hospitali moja mjini Mombasa kukosa kumpatia huduma bora.

"Hata wakati wa kifo, unyanyapaa bado unaendelea kujitokeza(Clinton) Shilisia. baba yake anasema alitaka mtoto wake afanyiwe upasuaji lakini mwanapatholojia katika hospitali kuu ya Mombasa, aliogopa kwamba 'huenda angepata virusi vya corona'," Gazeti la People daily newspaper limesema.

Kifo na Ghadhabu

Hatua za kutokaribiana zimesababisha jamii nyingi kutojua la kufanya kuhusu namna ya kuaga wapendwa wao pale wanapoaga dunia.

Waislamu nchini Nigeria wamepokea miongozo kutoka kwa Baraza la eneo la Waislamu kuhusu namna ya kuzika wapendwa wao bila ya kudhuru wale wanaoendelea kuishi.

Lakini nchini Ghana, hifadhi za maiti zimejaa huku familia zikisubiri ushauri wa serikali kama inawezekana kuruhusiwa kuzika wapendwa wao.

"Kawaida mazishi huwa ni jambo kubwa na mara nyingi hufanyika wikendi. Mazishi mengi hujumuisha kuimba na kucheza na inaweza na pia inaweza kuwa ghali sawa a harusi... huku familia zikiwa haziko tayari kuchukua miili yao hadi kanuni ya kutokaribiana itakapolegezwa, hifadhi za maiti zinajaa haraka sana hata kuliko ilivyokawaida huku nyengine zikiwa tayari zimesha jaa kabisa," Tovuti ya Joy amesema.

Nchini Gabon timu ya ugonjwa wa Covid-19, ililazimika kuomba msamaha kwa kumzika daktari mmoja aliyekufa na kumzikwa bila ya jeneza.

Haja ya kushirikiana

Maafisa katika mji wa Cape Verde wamesema kwamba unyanyapaa umefanya kazi ya wizara ya afya kuwa ngumu.

"Watu ni lazima washirikiane kwasababu bila hivyo kazi hiyo inaendelea kuwa changamoto na pia wanaweka watu wengine katika hatari," Mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzia maambukizi Cape amesema.

Mamlaka nchini kenya, Afrika Kusini na kwengineko barani humo pia wamekuwa wakitoa ombi kama hilo.