'Kwanini nilitumia bidhaa za kujichubua'

Karishma Leckraz alianza kutumia bidhaa za kumfanya kuwa mweupe akiwa na umri wa miaka 13 baada ya kuarifiwa kwamba atakuwa mzuri zaidi ngozi yake ikiwa nyeupe.

"Nliambiawa kwamba nina umbo zuri - lakini niabu kwasababu ni mweusi sana," msichana huyo wa miaka 27 amezungumza na Radio 1 Newsbeat.

Alifundishwa kutumia bidhaa za kubadilisha rangi ya ngozi na wazazi wake walitaka awe na ngozi nyeupe.

"Mizizi ya utamaduni wetu umejikita kwa dhana kuwa ukiwa mweupe wewe ni mzuri," Karishma anasema, "Wewe ni mzuri sana."

Ni utamaduni wa Asia ya Kusini, ambapo ngozi nyeupe inachukuliwa kuwa bora.

Lakini katika wiki za hivi karibuni, kutokana na majadiliano yaliyoanza baada ya kifo cha George Floyd, kampuni ya Unilver imesema itaacha kutumia neno 'fair' kwa bidhaa za krimu ya uso inazotengeneza zile zinazofanya mtu kuwa mweupe nchini India na kubadilisha nembo yao hadi 'Glow and Lovely'

'Usikae juani kwa mud amrefu'

Kama Karishma, Sabrina Manku aliambiwa na familia yake kwamba yeye ni mweusi sana.

"Nikiwa msichana mdogo, 'Ilikuwa ni usikae kwenye jua kwa muda mrefu.' Wangetuambia kwamba hilo litakufanya kuwa mweusi."

Huko Punjabi wanasema hivyo, na hiyo ndio sababu hilo linaweza kumuumiza sana mtu moyo, msichana huyo mwenye umri wa 23 amesema.

Sabrina alikuwa na miaka 10 tu mara ya kwanza alipooneshwa krimu za kujichubua alizozitumia kwa miaka minane.

Lakini sio tu maneno ya familia yanayoweza kumfanya mtu kuanza kujichubua.

Kwa Anusha, ambaye hakutaka kutoa majina yake kamili, ni miaka ya ujana wake shuleni ambayo ilimfanya kuwa na hisia mbaya sana kuhusu ngozi yake.

"Nilijiona nikianza kujilinganisha na watu ambao walikuwa weupe."

"Wasichana maarufu wangechukuliwa na watu tofauti sio kwa jambo jingine zaidi tu ya rangi ya ngozi yao nyeupe."

Karishma aliacha kupiga picha na rafiki zake akiwa kijana.

"Sikutaka nionekane kwenye picha jinsi nilivyo mweusi," anasema.

'Nilifuata kile watu maarufu walichofanya'

Sabrina anazungumzia sinema za Bollywood - tasnia ya filamu India - ilivyokuwa na ushawishi mkubwa katika maamuzi yake ya kutumia krimu za kujibadilisha rangi.

"Niliangalia waigizaji nyota na kufuata mitindo yao, chochote ambacho wamezindua."

Nyota wa Bollywood wamekosolewa kwa kutangaza bidhaa ambazo zinaendeleza kujichubua.

"Inakufanya tu uhisi wewe ngozi yako ni nyeusi na kutumia bidhaa fulani kutafanya ubadilike kwasababu waigizaji nyota wanakuambia kwamba utaona mabadiliko."

Baadhi ya matangazo ya biashara ikiwemo yale ya wanaume kuvutiwa na wanawake weupe baada ya kuanza kutumia bidhaa ya kujichubua wakati awali walikuwa wanaonekana wao ni weusi pia kunachangia.

Na hilo, haliishi kwa matangazo ya biashara pekee.

"Nimebaini kwenye filamu, kuw ana ngozi nyeupe kunachukuliwa kuwa mzuri zaidi. Nilitaka kuonekana kama wale ninao waona kwenye televisheni," Sabrina anaongeza.

'Bado natumia bidhaa za kunibadilisha rangi kuwa mweupe'

Karishma na Sabrina hawatumii tena bidhaa zao kwasababu ya athari yake kwa ngozi zao lakini pia kwasababu siku hizi wanajiamini zaidi.

Hali ni tofauti kwa Anusha.

Familia na shinikizo la jamii kuhusu suala la kuwa mweupe kulimfanya kuanza kutumia bidhaa za kumbadilisha rangi ili awe mweupe lakini sasa hivi hali imekuwa tofauti.

"Sio kila mmoja anayenunua bidhaa ya kumbadilisha rangi anataka awe mweupe milele. Kwangu mimi, ngozi yangu inaonekana kung'aa inapokuwa imekolea.

Anusha sasa hivi anatumia bidhaa za urembo za 'mask' ambazo zinabadilisha ngozi yake iwe nyeupe.

Anakubali kwamba kama hangefahamu mambo ya kujichubua akiwa mdogo basi sasa hivi. asingekuwa anatumia bidhaa hizo.

Pia unaweza kutazama: