Vital Kamerhe: Mshirika mkuu wa serikali ya rais Felix Tshisekedi nchini DR Congo amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela

Chanzo cha picha, Reuters
Mshirika mkuu wa serikali ya rais Felix Tshisekedi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Vital Kamerhe amehukumiwa kifungo cha miaka 20 kwa ufisadi na wizi wa takriban dola milioni 50 za Marekani.
Kamerhe ni mwanasiasa maarufu katika siasa za taifa la DR Congo na ndie mtu muhimu wa muungano uliomsaidia rais Felix Tshisekedi kuchukua madaraka.
Ndie mwansiasa mkuu zaidi kukabiliwa na mashtaka katika taifa la Dr Congo ambapo kuna ufisadi wa kiwango cha juu.
''Katika kila tulichosikia, mahakama imebaini ukweli kuhusu makosa ya wizi wa dola milioni 48, 831, 183 za Marekani'', alisema jaji Pierrot Bankenge Mvita katika uamuzi wake.
Wakati jaji alipokuwa akitangaza hukumu hiyo , Vital Kamerhe alisalia mtulivu na hata kutabasamu mara kwa mara.
Hatoruhusiwa kuwania wadhfa wowote kwa miaka 10 baada ya kuhudumia hukumu yake na hata kushikilia wadhfa wowote wa serikali.
Mahakama vilevile itapiga tanji akaunti zake zote za benki pamoja na zile za ndugu zake , mbali na mali ilionunuliwa na fedha zilizoibwa.
Kamerhe amekana kuiba fedha zilizotengewa mradi wa ujenzi wa nyumba za serikali chini ya uogozi wa rais Tshisekedi na kuyataja mashtaka hayo kuwa ya kisiasa. Wakili wake Jean Marie Kabengela Ilunga aliutaja uamuzi huo kama ukiukaji wa haki za kibinadamu na kusema kwamba atakata rufaa .
Vital Kamerhe alimuunga mkono Tshisekedi uchaguzi wa 2018
Kiongozi huyo alimuunga mkono Tshisekedi katika kampeni zake za 2018 akitarajia kwamba atarejesha mkono mwaka 2023.
Kukamatwa kwake tarehe 8 mwezi Aprili kulizua wimbi la mshangao katika Muungano wa serikali na taifa zima kwa jumla.

Chanzo cha picha, Getty Images
Chini ya uamuzi huo , Kamerhe hatoweza kuwania urais kwa takriban miaka 10 baada ya adhabu yake. .
Wiki iliopita waziri wa haki alifichua kwamba jaji aliekuwa akisimamia kesi hiyo ambaye mara ya kwanza alidaiwa kufariki kutokana na mshtuko wa moyo mwezi uliopita , aliuawa kikatili.
Makundi ya kupigania haki yamekuwa yakimshinikiza rais Tshisekedi kuafikia ahadi zake za kampeni za kukabiliana na ufisadi wachambuzi wa kisiasa wanasema kulingana na chombo cha habari cha reuters.
''Kwa kweli nadhani hii ni ishara nzuri katika vita dhidi ya ufisadi'' , alisema Florimond Muteba kutoka kundi la usimamizi wa matumizi ya umma, kundi linalopigania haki za kibinadamu nchini DR Congo akinukuliwa na Reuters..
Lebanese businessman Jammal Samih was also sentenced to 20 years' hard labour in the same trial, while a third man in charge of logistics at the presidential office faces two years in prison.












