Virusi vya corona: Ni kwanini mwandishi huyu aliwakera Wachina?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kitabu cha kumbukumbu kilichoandikwa na mwandishi nguli wa China, akielezea maisha yake mjini Wuhan wakati mlipuko wa virusi vya corona ulipotokea na sasa amekitafsiri kwa lugha ya kiingereza.
Fang Fang alianza kuchapisha mtandaoni katika akaunti yake, na kuandika kuhusu maisha yalivyo katika mji wake mnamo mwezi Januari wakati ambao iliaminika kuwa bado ni janga ta taifa hilo tu.
Kitabu hicho cha kumbukumbu ambacho kiliandikwa na mwandishi huyo mwenye umri wa miaka 65 kimesomwa na watu wengi baada ya kuelezea jinsi virusi hivyo hadimu vilivyoingia katika mji wa China.
Mapema mwaka huu, Wuhan ulikuwa mji wa kwanza duniani kuweka marufuku ya kutotoka nje ili kuzuia maambukizi ya corona kuenea. Mji huo ulikata mawasiliano na si na miji mingine ya China bali dunia nzima.
Wakati marufuku ya kutotoka nje ikiendelea, Fang Fang alizidi kupata umaarufu. Wachapishaji walitangaza kuwa watakusanya machapisho yake na kuchapisha kwa lugha mbalimbali.
Lakini umaarufu wa Fang Fang kukua kimataifa umebadili mtazamo wake katika nchi yake. Anatazamwa kwa chuki sana nchini China - wengi wakiwa wamekasirika kwanini ameripoti na hata kumuita kuwa msaliti.
Kitabu chake cha kumbukumbu kinahusu nini?
Mwishoni mwa mwezi Januari, mara baada ya China kuweka amri ya watu kutotoka nje katika mji wa Wuhan, Fang Fang - ambaye jina lake asili ni Wang Fang - alianza kuandika matukio ambayo yalikuwepo katika mji huo wa China kupitia kurasa ya mtandao wa kijamii wa China unaofahamika kama Weibo.
Katika 'diary' yake, aliandika kila kitu kuhusu changamoto za maisha yake ya kila siku na athari ambazo watu walizipata kwa kulazimishwa kujitenge.
Mchapishaji HarperCollins alisema kuwa mwandishi alitoa sauti ya hofu, msongo wa mawazo, hasira na matumaini kutoka kwa mamilioni ya wananchi wenzake.
Alibaini kuwa mwandishi amezungumzia kuminywa kwa haki, matumizi mabaya ya madaraka na changamoto nyingine ambazo zilizojitokeza wakati wa mlipuko pamoja sintofahamu iljyotokea katika mitandao .
Katika chapisho moja la gazeti la Sunday Times aliandika jinsi alivyoenda kumchukua binti yake katika uwanja wa ndege.
Magari kuyaona mtaani ilikuwa ni vigumu sana. Siku hizo chache zilikuwa zimewafanya watu wapate taharuki na hofu ya kutojua hatima yao.Watu wote walikuwa wamevaa barakoa," alisema.
Jinsi janga hili lilipogeuka kuwa la kimataifa?
Wakati ambao taarifa zilikuwa zinatolewa kwa kuminywa sana na vyombo huru vya habari ni vichache, ghafla Fang Fang aliibuka kuwa chanzo cha habari cha kuaminika, na historia yake ya kuwa mwanahabari aliyefahamika na hata aliyewahi kupata tuzo.
"Taifa hili linahitaji linahitaji waandishi wenye udhubutu kama yeye.Umma unashindwa kuamini taarifa nyingi ambazo zinatolewa na vyombo vya habari vya serikali, mtumiaji mmoja wa mtandao wa Weibo aliripotiwa akisema hayo katika tovuti ya The Independent.
Umaarufu wake na kile alichoandika kilisambaa kwa kasi na taarifa hizo hazikuchukua muda kabla hazijatoka nje ya China.
Kwa nini China imemgeuka?
Uzalendo wa kitaifa upo sana katika mitandao ya kijamii ya China na hata watu udiriki kufanya uhalifu mtandaoni kwa maslahi ya taifa lake.Maelfu ya wananchi wenye hasira wako tayari kutetea kila kitu ambacho kinakosolewa kuhusu China au kuhojiwa na kudhihakiwa na wageni.Na Fang Fang si mwandishi wa kwanza wa China kudhihakiwa mtandaoni.
Katika kesi hii, wakati virusi vikiwa vinaendelea kusambaa duniani kote, watu walianza kuhoji jinsi China ilivyokabiliana na mlipuko wa Corona.Taifa hilo likikosolewa na raia wengi wakitaka kujitetea.
Ndio kipindi ambacho ilifahamika kuwa kazi za Fang Fang zilikuwa zimeuzwa ulaya.
Wuhan imeanza kurejea katika maisha ya kawaida baada ya wiki za amari kari ya kutotoka nje.

Chanzo cha picha, AFP
Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha habari kuhusu kile kiluchopo katika mtandao wa Weibo, huu ni wakati ambao watu walipomgeuka baada ya kugundulika kuwa kitabu hicho cha kumbukumbu kimeuzwa kwa wachapishaji wa kimataifa wa Amazon".
Wachina wengi walikosoa kutafsiriwa kwa nakala hiyo ya Fang kuhusu mlipuko wa Corona katika mji wa Wuhan ni usaliti, iliripotiwa.
Ghafla aligeuka kuwa msaliti wa China na sio chanzo cha habari cha kuaminika tena, wengi wakisema kuwa alikuwa akitumia janga kupata umaarufu.
"Ametumia fursa ya wakati huu taifa liko katika janga kujitafutia umaarufu," alisema mtumiaji mmoja wa mtandao wa Weibo. "Hii haikubaliki ."
Hasira za watu dhidi yake hazikuzuia kitabu kutochapishwa na mchapishaji wa Marekani HarperCollins -wakati ambao Marekani na China wakiwa wana mzozo mkubwa wa kidiplomasia.

Chanzo cha picha, AFP
Chombo cha habari cha taifa la China kiliweka wazi pia nafasi ya Fang Fang iko wapi?
"Kuibuka kwake katika vyombo vya habari vya kimataifa ni sawa na kengele ya kutuamsha Wachina wengi kuwa mwandishi huyo inawezekana anatumika na nchi za magharibi ili kuchafua jitihada ambazo China ilizifanya " gazeti la Global Times.
"Kitabu hicho kimeangalia upande wa mabaya tu ambayo yalitokea mjini Wuhan na hakuandika jitihada ambazo wananchi walizifanya kuunga mkono jitihada za kuzuia maambukizi.
Kitabu hicho kimepokelewaje?
Ni ngumu kusema kitabu kimepokelewaje kwa sababu kilitoka Ijumaa ya wiki iliyopita tu.
Ingawa tayari kuna wengine wamesifu umahiri wa uandishi wake wakati akiwa katika marufuku ya kutoka nje huku wengine wakidai kuwa taarifa hizo ni za uongo.

Taarifa zaidi kuhusu virusi vya corona













