Virusi vya Corona: Maisha ya kutekeleza amri ya kusalia ndani kwa wahamiaji haramu

'Carla' ni mfanyakazi asiye na kibali halali cha kufanya kazi Uingereza.
Anaishi katika nyumba ndogo pamoja na wengine 11.
Mtu pekee katika nyumba hiyo mwenye kibali cha kufanyakazi ameajiriwa na Wizara ya Afya (NHS) mfumo ambao unagharamiwa na serikali.
"Tuna wasiwasi juu yetu na sisi wenyewe pia," anasema.
"Ninapokuwa mgonjwa (na virusi vya corona), naogopa siwezi kupiga simu kwa namba rasmi ya 111. Kwasababu watajua kuwa mimi niko humu nchini kiharamu."
Carla, ambaye ni raia ya Ufilipino, anaondoka tu kwenye nyumba hiyo wakati anaenda kumnunulia mtoto wake chakula.
Lakini kwasababu kazi aliokuwa akifanya ya kutunza wazee ilisimamishwa, anatumia pesa yake ya mwisho aliobaki nayo £3 ($3.63).
Kuishi kwa hofu
Mashirika ya kutoa msaada yanakadiria kwamba kuna watu takribani million 1 nchini Uingereza walio katika hali kama hizo kwasababu ya virusi vya corona.
Hawawezi kupata usaidizi wa kifedha na wako katika hatari ya kufa kwa njaa na pia wanawakilisha wale walio katika hatari ya kiafya.
"Matokeo yake ni ya kusikitisha," anasema Susan Cueva kutoka Muungano wa Kanlungan Filipino, ni wa raia wa Ufilipino nchini Uingereza.
Tangu mapema Aprili, alianza kuona vile watu wa jamii yake wanavyokufa.
"Wengine walikataa kupata usaidizi licha ya kwamba hali yao ilikuwa inaendelea kuwa mbaya," anasema Cueva, ambaye anatumia muda wake mwingi wa jioni kuzungumza na wahamiaji wasiokuwa na vibali wakubali kwenda katika vituo vya afya kupata matibabu.
Ana umri wa miaka 23 na anatoka Brazil.
Aliingia Marekani kwa kutumia visa ya utalii na alikuwa akifanya kazi katika mgahawa mmoja lakini virusi vya corona vimebadilisha kila kitu maishani mwake.

Amepoteza kazi yake London, hakuweza kulipa kodi ya nyumba na chakula alichokuwa nacho pia kinaelekea kuishi.
"Hali ilikuwa mbaya zaidi pale serikali ilipoanza kutkeleza kanuni ya kuosogeleana, kwasababu polisi walikuwa wengi mitaani," anasema.
"Unaogopa kusimamishwa na maafisa wa polisi na mwishowe ujipate ukiwa gerezani."
Sintofahamu iliyopo ya ikiwa mtu kama huyo ataweza kupata huduma ya aya bure pia ni jambo jingine linalomsumbua G.
Raia wowote wa kigeni ikiwemo wale wanaoishi nchini humo bila kibali, wanalazimika kulipia matibabu yao pengine labda awe ni miongoni mwa kundi ambalo linalipiwa na serikali.
Wizara ya afya Uingereza inweza kuuliza wizara ya mambo ya ndani kuhusu uraia wa mgonjwa na hadhi yake ya ukaazi ili kufanya maamuzi ya ikiwa anastahili kulipia gharama zake au la.
Wizara ya afya Uingereza pia inaweza kupitia taarifa z amgonjwa kama vile jina, namba yake ya simu, anwani ya nyumbani kupitia wizara ya mambo ya ndani.
Wizara hiyo imeiambia BBC kwamba hakuna uthibitisho wa taarifa zozote za wahamiaji zinazohitajika ili mtu aweze kupimwa au kupata matibabu ya ugonjwa wa covid-19.
Pia inasema kwamba hakutakuwa na malipo yoyote yenye kuhusishwa na kupimwa virusi vya corona.

Lakini zaidi ya mashirika 30 ya haki za binadamu ikiwemo Liberty, Medact, na Baraza la Pamoja la Ustawi wa Wahamiaji (JCWI), wanasema kuongeza ugonjwa wa Covid 19 kwenye orodha ya magonjwa ambayo mtu anatibiwa bure, hilo pekee halitoshi.
Hilo limeungwa mkono na kundi la wanachama 60 wa bunge la Uingereza, wakiongozwa na mbunge wa chama cha Labour Bell Ribeiro-Addy, ambali limemuandikia barua Waziri wa afya na ustawi wa jamii Matt Hancock.
"Hilo haliondoe sera zisizo rafiki ambazo zimekuwepo kwa miaka mingi ambapo wahamiaji wameambiwa kwamba watalipia gharama zao za afya ama kukabiliana na mkono wa sheria wanapotafuta huduma ya umma," barua hiyo inasema.
Kwa 'G', hile limewadia kuchelewa.
Tayari alishatuma maombi ya mpango wa serikali ya Uingereza ambao unalipia nauli wahamiaji waliojitokeza kwa hiari kutaka kurejea makwao.
Kampuni ya kutoa msaada ya Casa do Brasil lilimwakilisha yeye na serikali ya Uingereza.
"Kwa wastani, tunapokea simu 5 hadi 6 kwa siku. Katika wiki zilizopita, idadi hiyo imeongezeka na kufikia 20 hadi 30," anasema Vitoria Nabas, wakili wa wahamiaji na mkurugenzi wa kampuni ya Casa do Brasil.
"Idadi kubwa ya watu wanaotaka usaidizi huo wamefikia kiwango cha kutamausha wasiji la kufanya."


Wahamiaji wasio na vibali
Hakuna idadi kamili ya wahamiaji haramu wanaishi Uingereza.
Inaweza kujumuisha wale ambao waliingia nchini humo kupitia usafirishaji haramu wa watu, wale ambao waliingia kwa visa nyingine na kupitisha muda wao wa kukaa humo, pamoja na ambao hawakufanikiwa kupata vibali vya kuwatambua kama wanaotafuta hifadhi.
"Mara nyingi nilijjipata mikononi mwa wasafirishaji watu kwa njia haramu na hatimae nikaingia kwenye meli iliyonisafirisha hadi Uingereza," anasema Zhao', mfanyakazi wa kwenye hoteli, ambaye ameishi Uingereza kwa miaka 12.
Alizungumza na BBC kupitia ofisi ya China kwa makubaliano kwamba hatatambuliwa.
Kama wafanyakazi wengine haramu, alikuwa na wakati mgumu sana wa kujitenga mwenyewe katika sehemu wanayoishi ambapo wamerundikana.
"Ninafuraha kwamba nimefanikiwa kufika umbali huu," anasema.
"Mara nyingi huwa sina cha kufanya lakini kwa bahati nzuri rafiki zangu ambao wako kwenye hali kama hiyo wananisaidia sana na kuniangalia."

Dr Rhetta Moran kutoka Rapar, kundi la kutete ahaki za binadamu lenye makao yake Manchester, anasema wahamiaji wasiokuwa na vibali wamekuwa wakitumiwa kama visingizio kisiasa kwenye mjadala ambao huwa moto sana kuhusu wahamiaji katika vyombo vya habari na serikalini.
"Serikali ilishindwa kupata idadi kamili kutoka kitambo na haijawahi kuwa tayari kutaka kujibu swali la idadi ya wahamiaji," anasema.
Daktari Moran amekuwa akifanya kampeni inayotaka serikali kwamba itoe makazi na huduma ya afya kwa kote, bila kujali hadhi yao ya makazi.
Lakini wahamiaji wasio na vibali wamekuwa wakipata usaidizi wa serikali katika baadhi ya matukio.
"Mimi ni mgonjwa wa saratani na kwasasa hivi nasaidiwa na serikali," anasema Wang', Raia wa China mwathirika wa migogoro ya nyumbani.
Jamaa yake alimsaidia kuhamia Uingereza zaidi ya miaka 10 iliyopita, na kuccha familia yake na watoto. Kwasasa anaishi kwa makazi ya serikali.
"Hospitali imekuwa ikinitunza vizuri," anasema. "Nahitajika kuwa makini sana kwasababu kinga yangu ya mwili iko chini na hilo lina maanisha niko katika kundi la walio kwenye hatari ya kuambukizwa."
'G' kwasasa yuko nyumbani nchini Brazil,
Ndoto yake ya kupata maisha mazuri Uingereza ilikufa.
"Hadi lini kibali cha makazi kitaendelea kuwa na nguvu ya kuamua nani ikiwa mtu ni binadamu au la?" anasema.












