Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Covid -19 ilivyobadilisha utamaduni wa waafrika
Katika mfululizo wa makala maalum kutoka Afrika mwanahabari Joseph Warungu anaangazia vile virusi vya corona vimebadilisha maisha ya Wakenya kuanzia kujifungua hadi kifo.
Sheila Atieno amejitayarisha kumsaidia mwanamke kijana ambaye ana ujauzito wa wiki 32. Daktari Atieno amekuwa akifanya kazi hii kwa siku nyingi. Lakini safari hii, mwanamke huyu atakapojifungua, hali itakuwa tofauti.
Mama mjamzito aliletwa katika wadi maalum hospitali ya umma mji mkuu wa Nairobi baada ya kupatikana na virusi vya corona.
Daktari Atieno, mshauri wa magonjwa ya wanawake, ni miongoni mwa timu ndogo ya madaktari waliotambuliwa kumsaidia mwanamke huyu ambaye ameonesha dalili za virusi vya corona.
Maisha ya Daktari Atieno yamebadilika ghafla. Ni mama wa watoto wawili walio chini ya umri wa miaka miwili.
"Imekuwa vigumu sana kwangu kisaikolojia kukubali kwamba nitamhudumia mama wajawazito walioambukizwa virusi vya corona," amemuamirifu mwanahabari wa BBC.
"Nakaribia kwenda kufanya upasuaji ambao mara nyingi unahusisha kushika majimaji ya mwilini kwa kiwango cha juu. Ingawa kazi hiyo nitaifanya kama nimevalia nguo za kujikinga, hali hiyo inakufanya usijisikie huru.
"Na nitakapofika nyumbani, watoto watataka kunikimbilia. Lakini siwezi kuwagusa mpaka nitakapooga, nibadilishe nguo na nijipake kitakasa mikono (sanitizer).
"Ni kitu kinachosumbua hisia na akili. Lakini sina budi - ni kazi yangu kukaribisha viumbe wapya wanaokuja duniani ama kuwe au pasipo kuwa na janga," Dr Atieno amesema.
Maharusi wapya
Francis na Veronica Gitonga ni wanandoa wapya ambao bado wanafurahia fungate yao kijijini mwao Nyahururu, takriban kilomita 200 kutoka Nairobi.
Walikuwa wamepanga harusi yao ifanyike Aprili 5. Walikuwa wamekaribisha wageni 500 kushuhudia siku yao hii.
Lakini ni watu 6 tu walioruhusiwa kuingia kanisani siku hiyo - bibi na bwana harusi, wasimamizi wao na viongozi wawili wa kidini waliowafungisha pingu za maisha. Hakuna mzazi, familia wala yeyote kutoka kijijini mwao aliyehudhuria sherehe yao.
Kanuni ya kutokaribiana na marufuku ya kusafiri kulikosababishwa na ugonjwa wa Covid -19 kumefanya mamia ya wengine kushindwa kuhudhuria harusi yao.
Mahali pa kula kulikuwa nyumbani kwao ambapo watu 12 pekee ndio waliokuwepo.
Walikuwa na fursa ya kuahirisha harusi yao hadi maisha yatakaporejea katika hali ya kawaida. Lakini waliamua kuendelea mbele na mipango yao.
Walipoulizwa ikiwa wanajutia kwa kutochelewesha harusi yao ili kuwezesha familia na marafiki zao kujumuika nao, walisema:
"Hapana, hatuna cha kujutia," asema Bwana Gitonga, mshiriki wa kanisa la Redeemed Gospel Nyahururu.
"Tulihisi kama vile Mungu ametuzungumzia na kutaka tuendelee na harusi yetu. Aidha, Veronica na mimi tunapendana kwa dhati na kuunganishwa kanisani mbele ya Mungu ndicho tulichokuwa tunataka.
Bwana Gitonga alisema ugonjwa wa Covid-19 sio kwamba umebadilisha mipango ya wapendwa hao, lakini pia imekuja na maunfaa yake.
"Harusi yetu ingegharibu karibia elfu 300,000 pesa za Kenya sawa na ($2,800; £2,250). Lakin kwasababu hatukuwa na wageni, na mengineo, tumetumia shilingi elfu 50 za Kenya.
"Na sasa tunapigiwa na watu kutoka maeneo mbalimbali wakisema kwamba harusi yetu imewatia moyo na kutaka kufanya karusi za kawaida tu badala ya zile za kifahari na mwisho munaishia na madeni."
Simulizi ya bwana na bibi Gitonga wakati janga la corona linaendelea
Familia inayoomboleza
Wakati wa amri ya kutotoka nje usiku ilipowekwa na serikali kujaribu kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona kijana mdogo, 13, Yassin Hussein Moyo, alipigwa risasi na polisi.
Yassin ni miongoni mwa mwaathirika. Katika maeneo mbalimbali, raia wana wanauguza majeraha ambayo chanzo ni ni polisi kutumia nguvu kupita kiasi na cha kushangaza ni kwamba moja ya malengo yao ni kuhudumia watu wote.
Maneno ya baba yake Yassin, Hussein Moyo, yaligusa wengi pale aliposema akiwa mazishini kwa kijana wake: Mchana tunakabiliwa na tishio la virusi vya corona na usiku tunalazimika kukabaliana na tishio la polisi."
Idadi kubwa ya Wakenya, ambao wengi wanategemea ajira zisizo rasmi mara nyigni wanasikiza kwenye nyombo vya habari wakisema vile wanakumbana na changamoto ya kukabiliana na virusi vya corona, njaa na polis
Mwanasiasa mkongwe
James Orengo ni mwanasiasa mkongwe na seneta wa chama cha upinzani Orange Democratic Movement (ODM). Mara nyingi hujipata akikosoa serikali.
Katika kikao maalum cha bunge la Seneti kuhusu sheria za uchaguzi, Bwana Orengo ambaye ni wakili, alizungumzia hatari za kupitisha sheria mbaya na kuonya wabunge wa uoande wa serikali dhidi ya kuridhika na kila hatua inayochukuliwa na serikali.
Akifuatilia kesi yake kupitia skrini ya televisheni akiwa kizuizini, alipata faraja baada ya kusikia kwamba ataendelea na kesi yake akiwa huru baada ya hakimu kuagizwa aachiliwe bila bondi.
Mfungwa mwenye bahati
Ugonjwa wa Covid-19 umesababisha mfumo wa mahakama kuendesha shughuli zake kidijitali.
Miongoni mwa waliofadika na hatua hiyo ni mwanamume mmoja aliyekuwa anashtumiwa kwa kuiba bibilia kutoka duka moja la kufanya manunuzi.
Ni sehemu ya mpango wa serikali ya kuhakikisha inakabiliana na ugonjwa wa Covid-19 kwa kupunguza wafungwa kadiri inavyowezekana, hatua ambayo tayari imechangia kuachiliwa kwa wafungwa 4,800 wa makosa madogo madogo.
* Jina halisi la daktari limefichwa kwasababu hana idhini ya kuzungumza na vyombo vya habari