Coronavirus na chloroquine: Je kuna ushahidi kwamba dawa hii inatibu?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kumekuwa na wimbi la uhitaji wa dawa zinazotumika dhidi ya ugonjwa wa malaria kwa ajili ya kupambana na virusi vya corona, wakati serikali mbalimbali duniani zikitafuta tiba ya ugonjwa huu mpya.
Chloroquine na dawa zenye uhusiano nazo, hydroxychloroquine, zimekuwa zikitazamwa hasa- pamoja na shirika la afya duniani kusema kuwa hakuna ushahidi kuwa dawa hizo zinafanya kazi.
Hivyo basi ushahidi wa sasa kuhusu ufanisi kama tiba dhidi ya virusi vya corona, na ni nani anazitumia?
Tunafahamu nini kuhusu dawa hizi?
Rais Trump mara kadhaa ameeleza umuhimu wa hydroxychloroquine katika taarifa zake Ikulu.
Katika mazungumzo na vyombo vya habari hivi karibuni alizungumzia kuhusu dawa hii akisema: ''utatakiwa kupoteza nini? Meza.''
Katika video iliyoondolewa na Facebook kwa makosa ya kukiuka taratibu za utoaji taarifa, Rais wa Brazil Jair Bolsonaro alidai kuwa ''hydroxychloroquine inafanya kazi kila mahali''.

Chanzo cha picha, Reuters
Vidonge vyenye chloroquine ndani yake kwa muda mrefu vimekuwa vikitumika kutibu malaria na kushusha homa na maumivu, na kuna matumaini kuwa vinaweza pia kuzuia virusi vinavyosababisha Covid-19.
''Chloroquine inaonesha kuwa imeweza kuzuia virusi vya corona kwenye tafiti za maabara. Kuna ushahidi kutoka kwa madaktari ukisema kuwa inaonekana ikisaidia,'' anasema mwandishi wa habari wa masuala ya afya wa BBC.
Kuna ushahidi mdogo kwa sasa kutoka kwenye majaribio ya sasa kuhusu ufanisi katika matumizi ya kutibu wagonjwa wenye covid-19.
Pia kuna hatari ya kuwepo kwa athari zitokanazo na matumizi yake kama vile kuharibika kwa ini na figo.
''Tunahitaji majaribio yenye hadhi ya juu ili kuweza kutathimini ufanisi wake,'' anasema mwandishi wa ripoti kuhusu majaribio ya dawa za kupambana na malaria kwa ajili ya matumizi dhidi ya covid-19. Kome Gbinigie.
Zaidi ya majaribio 20 yamefanyika, ikiwemo Marekani, Uingereza, Uhispania na China.
Uingereza inafanya majaribio ya dawa hizo za kutibu malaria ili kutathimini kama zina uwezo wa kutibu Covid-19 kwa wagonjwa walioathirika.
Nchini Marekani, majaribio kadhaa yanaendelea kwa dawa aina ya Chloroquine na hydroxychloroquine na dawa za azithromycin kwa ajili ya kutibu wagonjwa wa covid-19.
Nchi zipi zimeruhusu matumizi ya dawa hizo?
Mamlaka ya udhibiti wa dawa na chakula nchini Marekani, FDA, chombo kinachotoa leseni kwa dawa katika bara la Amerika, imetoa nafasi ya dawa hizi kutumika kama ''dharura'' katika kutibu virusi kwa wagonjwa wachache walio hospitalini.
Haina maana kuwa FDA inasema kuwa zinafanya kazi moja kwa moja. Lakini ina maana kuwa katika mazingira yasiozuilika, haospitali zinaweza kuomba kutumia dawa hizo kutoka kwa bohari za serikali kwa ajili ya matumizi ya kutibu covid-19. Serikali ya Marekani imesema dozi milioni 30 za hydroxychloroquine zimetolwa na kampuni ya kutengeneza dawa kwa bohari ya taifa.
Nchi nyingine pia zinatumia dawa za kupambana na malaria kwa viwango vinavyotofautiana. Ufaransa imeidhinisha madaktari kutoa dawa hiyo wa wagonjwa wa covid-19 lakini waangalizi wa masuala ya dawa wametahadharisha kuhusu athari zake .
Wizara ya afya ya India imeidhinisha matumizi ya hydroxychloroquine kama dawa ya kutibu kwa ajili ya wafanyakazi wa afya, pia watu waliochangamana na watu walio na maambukizi.
Hata hivyo, idara ya utafiti ya Serikali ya India imeonya kuhusu matumizi yasiyodhibitiwa ya dawa za kuzuia matumizi ya dawa na kusema kuwa ni dawa za ''majaribio'' kwa hali ya dharura pekee.
Nchi kadhaa za mashariki ya kati zimeridhia matumizi au zinafanya majaribio.
Ikiwemo Bahrain (ambayo inadaikuwa ilikuwa ya kwanza kutumia hydroxychloroquine kwa wagonjwa wa corona, Morocco,Algeria na Tunisia.

Chanzo cha picha, Reuters

Unaweza pia kusoma:

Je dawa aina ya chloroquine inapatikana vya kutosha?
Wakati uhitaji wa dawa hizi ukiongezeka kama dawa muhimu ya kutibu virusi vya covid-19, nchi nyingi zimeshuhudia uhitaji wa kiasi kikubwa na upungufu.
Chloroquine imekuwa ikipatikana kwa kiasi kikubwa kwenye maduka ya dawa, hasa katika nchi zinazoendelea, kwa ajili ya kutibu malaria.
Ingawa dawa hizi zimekuwa hazina ufanisi dhidi ya malaria, kutokana na ugonjwa kuzidi kuwa sugu.
Jordan imepiga maruku uuzwaji wa hydroxychloroquine kwenye maduka ya dawa ili kuzuia dawa kujazana.
Vivyohivyo wizara ya afya ya Kuwait imeamua kuondoa dawa zote zenye aina hiyo ya dawa kutoka kwenye maduka ya dawa binafsi na kudhibiti upatikanaji wake kwenye hospitali na vituo vya afya.
Kenya imepiga marufuku uuzaji wa chhloroquine , kwa sasa inapatikana kwa ruhusa maalumu ya wataalamu waafya.
India ni mzalishaji mkubwa wa dawa hizi, nayo imeweka marufuku kuzisafirisha nje dawa hizo.
Rais Trump alitoa ombi binafsi kwa waziri mkuu wa India Narendra Modi, ili apate dawa hizo kwa matumizi ya Marekani.
Imeripotiwa kuwa India inalifikiria ombi hilo.

Chanzo cha picha, Reuters
Taarifa kuhusu utafiti wa mwezi Februari nchini China kuhusu matumizi ya chloroquine kupambana na virusi vya corona ilisababisha mjadala mkubwa jijini Lagos, hivyo watu walianza kununua dawa kwa wingi.
Kutokana na kauli ya Trump kuhusu dawa hizo na ufanisi wake katika kupambana na covid-19 maduka ya dawa yaliuza dawa hizo na kuzimaliza kwa haraka sana.
Lakini kituo cha udhibiti wa magonjwa nchini Nigeria kimewaambia watu kuacha kutumia dawa hiyo.'' WHO haijaidhinisha matumizi ya chloroquine kwa ajili ya kudhibiti covid-19.''
Maafisa katika jimbo la Lagos wanasema kumekuwa na watu kadhaa wameathiriwa na matumizi ya kupita kiwango cha kawaida cha chloroquine.
Unaweza pia kutazama:















