Virusi vya corona: Kwa nini ni vigumu kutibu magonjwa ya virusi ikilinganishwa na yale ya bakteria

Unapougua ugonjwa unaotokana na bakteria unaweza kuuponya kwa kutumia dawa aina ya antibiotic lakini viruysi ni vigumu kukabiliana navyo

Chanzo cha picha, iStock

Maelezo ya picha, Unapougua ugonjwa unaotokana na bakteria unaweza kuuponya kwa kutumia dawa aina ya antibiotic lakini viruysi ni vigumu kukabiliana navyo

Tunapokutwa na kikohozi , pua inayotoka makamasi, joto mwilini, na maumivu ya misuli, hutembelea katika kituo cha afya ili kupata tiba ya haraka.

Iwapo tatizo la dalili hizo ni bakteria, tuna bahati. Kwani tiba ya antibaotiki kwa kiwango kikubwa hutusaidia na kurudia hali yetu ya kawaida katika siku chache ama wiki.

Lakini iwapo sababu ya dalili hizo ni virusi mambo yanakuwa magumu.

Maelezo zaidi

Hatuna kiwango kikubwa cha dawa za kukabiliana na virusi na zilizo na ufanisi mkubwa.

Mara nyingi binadamu hutegemea mfumo wake wa kinga mwilini kukabiliana na viriusi hivyo.

Maambukizi ya bakteria

Ijapokuwa kwa kawaida viumbe (virusi na bakteria) huchanganywa, makundi yote mawili ya viumbe hivyo ni tofauti sana na hatupaswi kuviweka katika mfuko mmoja.

Bakteria ni viumbe hai vilivyo na seli moja ambavyo havina kiini kilichoainishwa (prokaryotes), tofauti na seli za binadamu (kiini, eukaryotes).

Wakati bakteria wanapoishi nasi, wanakuwa katika sehemu tunayojua kama microbiota.

Kuna mamia ya maelfu ya spishi ambazo ni sehemu ya wazo hili, kwa njia ambayo tunaweza kuiona kama kiungo kimoja zaidi cha mwili wetu.

Utumbo wa mwanadamu

Chanzo cha picha, iStock

Maelezo ya picha, Wanadamu wana bakteria nyingi zaidi ya wanyama katika miili yao

Jeni zake (microbiome) hutoa habari ya maumbile karibu mara hamsini zaidi kuliko ile tunayo katika seli za binadamu katika miili yetu.

Tunaishi nao kwa njia ya amani na seli zetu na zile za bektaria zinaishi kwa njia hiyo.

Tunawajua bakteria wetu vizuri sana hali ya kwamba tunadhibiti madhara yao na kukabiliana na magonjwa yanayosababishwa na viumbe hivyo.

Kutibu ugonjwa wa bakteria, ikiwa una antibiotic inayofaa, inaweza kuwa nafuu.

Isipokuwa maambukizi makali yanayosababisha homa ya mapafu ama kifua kikuu

Maambukizi ya virusi

Lakini virusi ni tofauti kwani viumbe hivi husababisha maambukizi kwa lengo la kuathiri seli inayovipatia makao ili kuishi na kuzaana.

Kama ilivyo kwa binadamu wanaosafiri, kila kirusi huchagua aina ya malazi.

Wakati virusi vinapopata ufunguo wa kufuli inayorahisisha ufikiaji wa seli, mlango hufunguliwa na maambukizi kuanza kutekelezwa

Virusi huvamia na kudhibiti seli za wanadamu na kusababisha madhara mabaya katika afya yetu

Chanzo cha picha, iStock

Maelezo ya picha, Virusi huvamia na kudhibiti seli za wanadamu na kusababisha madhara mabaya katika afya yetu

Wakati virusi vinapovamia seli ya mwanadamu , huteka udhibiti wake kwa manufaa yao vyenyewe huku mwanadamu akiathirika pakubwa na hatua yake ya uharibifu mwilini.

Na wakati mwingi hutumia mbinu tofauti ambazo ni tofauti zaidi ya zile za seli za mwanadamu. Kitu kibaya zaidi ni kwamba dawa za antibiotics haziwezi hata kupunguza makali yake.

Wakati dawa hizo zinapotumika kutibu maambukizi ya virusi, hatari yake mwilini ni kuudhofisha bakteria zilizopo mwilini, isipokuwa madhara yanayosababishwa na virusi pamoja na bakteria.

Matumizi ya dawa za antibiotics unapokabiliana na ugonjwa wa virusi ni kwamba huathiri vibaya afya yetu.

Je tayari tuna tiba ya kukabiliana na virusi?

Iwapo hakuna pathojeni zinazosababisha magonjwa au iwapo mfumo wetu wa kinga umedhoofishwa na sababu nyengine, matokeo ya virusi hivyo huenda hayana athari kali kama inavyofanyika na homa ya kawaida.

Kinga ya miili yetu hukabiliana na kutatua tatizo hilo mara moja. Ili kukabiliaa na virusi vikali zaidi kuna tiba za kukabiliana na virusi.

Wanasayansi wamefanikiwa kuvikabili virusi vya ukimwi kwa kutumia dawa za kupungiuza makali

Chanzo cha picha, iStock

Maelezo ya picha, Wanasayansi wamefanikiwa kuvikabili virusi vya ukimwi kwa kutumia dawa za kupungiuza makali

Hususan kutokana na mzigo ambao umelegtwa na virusi vya ukimwi ambavyo vimeongeza idadi dawa kulingana na virusi vilivyopo.

Kila tiba inaweza kutumika kulingana na aina ya virusi , kwa sababu kila kirusi kina uwezo wake.

Lengo dawa ya kukabiliana na virusi ni kuzuia virusi hivyo kuzaana. Kila dawa hufanya hivyo wakati fulani , kuzuia virusi hivyo kutoshambulia seli .

Nijia zote hizo zinalenga kuupatia mfumo wetu muda wa kujizatiti ili kukabiliana na ugonjwa huo kutoka ndani.

Dawa ya virusi ama chanjo dhidi ya coronavirus

Ugonjwa wa ukimwi unaweza kutibiwa kwa kutumia dawa za kukabiliana na virusi kwa jina antiretrovirals ambazo hushambulia protini fulani ambayo husaidia virusi hivyo kuzaana.

Hatahivyo idadi ya magonjwa mengine ya virusi kama vile coronavirus ama flu mkatati huo hauwezi kufua dafu.

Kwa sasa ili kuweza kukabiliana na virusi vya coronavirus , dawa za virusi zilizotumika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola , Matburg au MERS zinahitajika .

Antiretrivirals

Chanzo cha picha, iStock

Maelezo ya picha, dawa za antiretrivirals zinatumika kutibu covid-19 na yamefanikiwa ktika kutibu hali kama hizo