Coronavirus: Njia tano zilizotumiwa na baadhi ya mataifa kuzuia kasi ya virusi vya corona

Utambuzi wa virusi vya corona unaanza katika uwanja wa ndege wa Singapore

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Utambuzi wa virusi vya corona unaanza katika uwanja wa ndege wa Singapore

Ni vigumu kupata mtu yeyote asiyetambua mlipuko wa virusi vya Coivid-19 kuwa ni janga baya zaidi duniani tangu Vita vya Pili vya Dunia.

Huku baadhi ya mataifa yakipata maafa mabaya zaidi kama vile China, Uhispania, Italia na Marekani , mengine yameidhinisha mikakati ambayo imezuia kusambaa zaidi kwa virusi vya corona.

Na mipango hiyo iko tofauti kuanzia kuwafanyia raia wake vipimo vingi hadi kujitenga katika mikutano ya watu wengi., kusalia majumbani hadi kuchunguza maeneo ambayo raia wake wapo hatarini zaidi kuambukizwa.

1.Kwa nini Ujerumani ina vifo vichache vya coronavirus ikilinganishwa na mataifa mengine

Licha ya kuwa taifa la tano lenye idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya covid 19 duniani (wagonjwa 71,808), idadi ya waathiriwa waliofariki 775 ni ndogo sana ukilinganisha na mataifa mengine ambayo yameripoti idadi inayolingana nao ya maambukizi kama vile Italia (wagonjwa 105,792 vifo 12,428), Uhispania (wagonjwa 95,923 vifo 8,464) na Uchina (wagonjwa 82,294 vifo 3,310).

Hata Uingereza yenye wagonjwa 25,481 ambao ni wachache kulinganisha na Ujerumani, ina idadi ya vifo 1,793 ambayo ni zaidi ya mara mbili ya Ujerumani.

Ujerumani ilisema kwamba ina uwezo wa kupima visa 160,000 kwa wiki

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ujerumani ilisema kwamba ina uwezo wa kupima visa 160,000 kwa wiki

Ipi siri ya mafanikio hayo ya kuzuia idadi ya vifo?

''Ijapokuwa hatujui sababu mwafaka, ukweli ni kwamba ...baada ya taifa hilo kugundua kuhusu hatua za dharura , lilianza kupanua vipimo vyake miongoni mwa raia ili kuzuia uwezekano wa maambukizi zaidi'', alisema Robert Koch kutoka taasisi ya masuala ya virusi akizungumza na BBCMundo.

Maelezo zaidi
Banner

Mojawapo ya sababu muhimu ya idadi ndogo ya vifo ni jinsi taifa hilo lilivyofanikiwa kuwatambua mapema wanaobeba virusi hivyo, hatua iliozuia kuenea kwake.

Mamlaka ya Ujerumani ilisema kwamba ina uwezo wa kufanya vipimo 160,000 kwa wiki.

Mataifa mengine ambayo yana maambukizi chungu nzima yamekuwa yakiwafanyia vipimo waliothibitishwa kukutwa na virusi hivyo huku yakiwapuuza wale walio na dalili chache .

2.Jinsi Japani ilivyofanikiwa kudhibiti covid-19 bila kutumia karantini

Huku ulimwengu ukikabiliana na mlipuko wa virusi vya corona, taifa la Japani lilpo eneo mwafaka kwa virusi hivyo kufanya madhara makubwa. Taifa hilo lipo karibu na Uchina kijografia.

Pia Japani ina idadi kubwa ya watu walio na umri wa juu kuanzia miaka 65 duniani na lina kiwango kikubwa cha watu wanaotumia tumbaku suala linalofanya raia wake kuwa miongoni mwa watu walio hatarini kuambukizwa virusi vya corona.

Japan

Chanzo cha picha, Getty Images

Lakini huku mataifa mengine yakichukua mbinu ya kukaa mbali na mikutano ya watu wengi ili kuzia kusambaa kwa virusi hivyo, serikali ya Japani iliamua kuendelea kuwaruhusu raia wake kukongamana.

Ijapokuwa wanapendekeza watu kuwa mbalimbali , mamlaka haijawalazimu raia kuchukua hatua kama zile zilizochukuliwa na China , Uhispania na Italia katika wiki za hivi karibuni.

Hakuna marufuku iliyowekwa kwa watu kutoka nje kama ilivyo kwa baadhi ya mataifa.

Ikilinganishwa na China na Korea, maambukizi nchini Japan na vifo viko chini sana.

Japani ina wagonjwa 2,233na mpaka sasa imeripoti vifo 66.

Mojawapo ya sababu ya idadi hiyo kuwa chini ni hatua ya taifa hilo kutambua maeneo ya maambukizi na kuwalinda wale walio hatarini kupata maabukizi hayo mbali na makundi ya milipuko.

Hata hivyo, taifa hilo limchukua hatua za kuzuia safari za ndege baina yake na mataifa yaliyoathirika sana kama Uchina na Marekani.

Pia vyombo vya habari vimeripoti wiki hii kuwa wasafiri watakaoingia nchini humo watalazimika kujiweka karantini kwa siku 14 ili kujichunguza kama wana dalili za virusi hivyo.

3. Vifaa vya kubaini Corona nchini Singapore

Kufanyiwa uchunguzi na kujitenga ndio hatua muhimu za kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa Covid 19.

Lakini Singapore ilichukua hatua zaidi: Ilitumia vifaa vya kutambua ugonjwa huo kubaini hasa uko wapi. Na hivyo ikafanikiwa kuudhibiti kutoka eneo la kitovu cha maambukizi.

Singapore ina mfumo imara na thabiti wa kufuatilia mawasiliano yanayowezesha ufuatiliaji wa waliotangamana na wagonjwa kwa urahisi kutoka mtu mmoja hadi mwingine ambapo watu na jamaa zao wa karibu wanaweza kutambuliwa na kutengwa kwa wakati unaofaa.

Kupitia njia hii, nchi hiyo ilifanikiwa kumaliza maambukizi katika maeneo ambayo ulikuwa umesambaa sana.

Mpaka sasa nchi hiyo imeripoti wagonjwa 926 na vifo 3.

Kuna programu nchini Singaore inayowatambua wale waliokaribiana na mgonjwa

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Kuna programu nchini Singaore inayowatambua wale waliokaribiana na mgonjwa

4. Watu wa Italia waliofanikiwa kudhibiti kusambaa kwa virusi baada ya kupata maambukizi

Si kila taarifa kutoka Italia juu ya virusi vya corona ni mbaya.

Mji unaovutia eneo la Veneto unaofahamika kama Vo Euganeo ulikuwa moja ya kitovu cha ugonjwa wa covid-19 nchini humo.

Eneo hilo likawa mbioni kukabiliana na jinamizi hili: Kituo cha kufanyiwa uchunguzi kikafunguliwa kwa wote wanaotaka kupimwa.

Kulingana na BBC Mundo, Profesa wa magonjwa ya maambukizi na virusi katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Padua, Andrea Crisanti, wakafanikiwa kupima kila mmoja katika mji huo.

Na kuanzia hapo wakaamua kuanza kufanya uchunguzi wa kufuatilia virusi hivi na kufikia yafuatayo: "Kisayansi walibaini kwamba kipindi cha kirusi kuhamia ni wiki mbili na kwamba mkakati wa kudhibiti maambukizi lazima utilie maanani idadi kubwa ya watu ambao wameshaanza kuonesha dalili."

Na kwa data hizi, wakafanikiwa kudhibiti mlipuko wa janga hili katika eneo husika.

Ni watu 63 pekee waliofariki Korea Kusini kutokana na ugonjwa wa coronavirus

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ni watu 63 pekee waliofariki Korea Kusini kutokana na ugonjwa wa coronavirus

5. Mkakati uliotumiwa na Korea Kusini kunusuru maisha ya wengi

Korea Kusini ilikuwa mfano duniani kwa sababu licha ya kwamba majirani zao ni China, chimbuko la ugonjwa wa Corona, idadi ya maambukizi na vifo ni ya chini.

Mpaka sasa nchi hiyo imeripoti wagonjwa 9,887 na vifo 165.

Kulingana na serikali ya Korea Kusini karibia watu 10,000 wanachunguzwa kila siku, na kufanya iwe rahisi kutenga wale wanaoonesha dalili, moja ya tatizo kubwa la usambazaji wa maambukizi.

Aidha, matukio mengine yaliyosaidia kudhibiti janga hili Korea Kusini ni utekelezaji wa hatua ya kujitenga bila kuzembea katika maeneo ya nchi hiyo. Ingawa baadhi ya hatua za kujitenga zimekosolewa kwa kuwa kali zaidi.

Wataalamu waliozungumza na BBC wamesema kwamba zilikuwa muhimu katika kuokoa maisha.