Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Siku ya wanawake duniani 2020: Wanawake watoa wito wa usawa
Maandamano ya kuhamasisha suala la ubaguzi dhidi ya wanawake yamefanyika katika miji tofauti duniani kuadhimisha siku ya wanawake duniani.
Maandamano hayo yamehudhuriwa na idadi kubwa ya watu licha ya hofu ya mlipuko wa ugonjwa wa corona.
Watu kote duniani wamekuwa wakiadhimisha siku hii maalum ambayo imekuwa ikiadhimishwa Machi 8 kuwatambua wanawake kwa zaidi ya karne moja.
Ilianza kama vugu vugu la wafanyikazi lakini limekuwa na kutambuliwa na Umoja wa Mataifa kama hafla ya kila mwaka.
Wanawake katika mpaka wa Uturuki na Ugiriki waliandamana kushinikiza waruhusiwe kuvuka mpaka huo siku ya wakati wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake.
Kumekuwa na makabiliano makali kati ya wahamiaji na maafisa wa kulinda mpaka wa Ugiriki huku wahamiaji hao wakipambana kuingia Muungano wa Ulaya,EU
Wanawake wa Bangladesh walicheza mpira wa kikapu viungani mwa mji mkuu wa Dhaka, mechi ambayo ilipangwa kuadhimisha siku ya wanawake duniani.
Nchini Pakistan maandamano yalifanyika katika miji tofauti licha ya vitisho na ghasia zilizoibuka dhidi sheria mpya. Ambapo, wafuasi wa chama cha Kislam cha Jamaat-e-Islami waliandamana mjini Karachi.
Katika mji mkuu wa Kyrgyzstan, Bishkek polisi iliwazuilia wanaharakati kadhaa wa wanawake muda mfupi baada ya wanaume waliojifunika uso kuripotiwa kuwashambulia waandamanaji.
Wanaharakati wanasema haki ya wanawake inaendelea kukandamizwa nchini humo.
Huko Belarus wanawake walishiriki ''mbio za urembo''kuadhimisha siku hii. Hawa hapa baadhi yao wakijianda kwa mbio hizo.
Wanawake katika mji mkuu wa Uhispania Madrid walikusanyika katika ukumbi wa Sol Square na kujivinjari kwa kutumia sufuria na vikaangio kuadhimisha siku ya wanawake duniani shouted and bashed pots .
Soma zaidi kuhusiana na siku ya wanawake duniani:
Picha zote zinahaki miliki.