Oscars, Brits na Baftas: Je tuzo kuu hujumuisha watu wa tabaka mbali mbali?

Je kumekuwa na uwakilishi wa kutosha wa watu tofauti katika tuzo za mwaka huu?

Kuanzia tuzo za Bafta mpaka za Brits, tuzo kuu zinazofanyika Januari na Februari zimeshutumiwa sana kwa kutokuwa na uwakilishi wa kutosha wa watu wa tabaka mbali mbali.

Lakini uwakilishi huo ungedhihirisha nini? Watu wengi wanaamini hakuna wanawake walioteuliwa pamoja na watu weusi, wenye asili ya Asia na hata wa kutoka makundi ya makabila ya wachache walioteuliwa.

Na kutokuwa na wateuliwa wengi kunamaanisha kuna washindi wachache.

Ni tuzo zipi zilizoshutumiwa zaidi?

Kwa ujumla tuzo zote zimeshutumiwa. Hii ni pamoja na tuzo ya Bafta ya Brits nchini Uingereza, na tuzo ya Oscar nchini Marekani.

Tuzo ya Bafta ilishutumuiwa kwa kukosa uwakilishi baada ya kukosa kuteuliwa watu wasiokuwa wazungu.

Hapakuwa na wanawake walioteuliwa katika kitengo cha muelekezaji bora kwa mwaka wa saba mtawalia sasa.

Katika tuzo ya mwaka huu ya Bafta, washindi kadhaa wa tuzo hiyo walitoa tamko katika hotuba walizotoa kuhusu kutoajumuishwa huko kwa watu wa tabaka mbali mbali na katika uteuzi na sekta nzima.

Wakati Dua Lipa aliponyanyua tuzo yake ya mshindi bora mwanamke Uingereza mwaka 2018 katika tuzo ya Brit alisema: " Tuz ohii iende kuchangia kushuhuiwa wanawake zaidi katika majukwaa haya, wanawake zaidi watakaoshinda tuzo na wanawake zaidi watakaoidhibiti dunia."

Mwaka mmoja baadaye katika tuzo za Brit 2019, idadi ya wanawake walioteuliwa iliongezeka kutoka wanne hadi kumi na wawili.

Lakini hali ilibadilika tena katika orodha ya wateuliwa 2020. Orodha ya wateuliwa wa mwisho katika kitengo cha albamu bora ilikuwa na majina ya wanaume watupu, huku mwanamke mmoja pekee - Mabel - akiteuliwa katika vitengo ambapo wanawake na wanaume wanaweza kuwania ushindi.

Wakati tuzo ya Brit iliposhutumiwa kwa hili katika siku za nyuma, waandalizi walijibu kwa kufanya mageuzi makubwa katika kamati yake ya upigaji kura.

Mwaka huu takriban nusu ya wanakamati hao walikuwa ni wanawake, na robo moja walikuwa ni weusi , wenye asili ya Asia na waliotoka makabila ya wachache. Kwa bahati mbaya, bado rodha ya wateuliwa haikufika kiwango cha uwakilishi uliotarajiwa na baadhi ya watu.

Inapokuja orodha ya wateuliwa ushindi wa tuzo ya Oscar hapa pia uwakilishi sawa ni tatizo.

Filamu kama 'Us', 'The Farewell' na 'Dolemite Is My Name' zote zimejumuisha waigizaji wa tabaka tofuati lakini hakuna muigizaji au filamu kati ya hizo ilioteuliwa.

Watafiti kutoka chuo kikuu cha Southern California wametazama fikamu 100 kuu katika box office na kugundua filamu nyingi kuu za 2019 ziliwajumuisha waigizaji wanawake na watu wanaotoka makabila ya wachache zaidi.

Wakosoaji walidhani muigizaji Lupita Nyong'o huenda angepata fursa kwa uigizaji wake kwenye filamu ya Us, lakini hakuteuliwa.

Mnamo 2019, kamati mpya inayotangaza tuzo hiyo ya Oscar iliidhinishwa na iliyokuwana idadi zaidi ya wanawake na watu wanaotoka makabila ya wachache.

Watu wanalizungumziaje?

Nyota mmoja mweusi aliyeteuliwa kushinda tuzi ya Oscar ni Muingereza Cynthia Erivo. Anasema ni hali ya 'tamu uchungu' kuwa mtu wa pekee wa rangi kuteuliwa.

Muigizaji Joaquin Phoenix alishinda tuzo ya muigizaji bora ya Bafta kwa uigizaji wake katika filamu ya Joker, alitamka kuhusu uwakilishi wa sawa katika hotuba yake ya kupokea tuzo.

Amemsema: "Nahisi kutatizika kwasababu waigiziaji wengi wenzangu wanaostahili hawakupata fura kama hii. Ninadhani tunatuma ujumbe wa wazi kwa watu wenye rangi kwamba hamukaribishwi hapa."

Mwanamfalme William pia alitoa hotuba katika tuzo ya Bafta na alisema: "Kwa mara nyingine tunajikuta tunazungumzia haja ya kuwajibika zaidi kukabiliana na uwakilishi sawa katika sekta hii.

"Hilo haliwezi kuwa sawa katika siku ya leo. Bafta lichukulieni suala hili kwa uzito, na kufuatilia uteuzi wa mwaka huu kuidhinisha ukaguzi kamili.. kuhakikisha fursa zipo wazi kwa kila mtu."

Nini kitakachofanyika sasa?

Sio mara ya kwanza kunazuka mzozo kuhusu uwakilishi wa sawa katika tuzo.

Mnamo 2015, kampeni ilioanzisha katika mitandao iliopewa jina #OscarsSoWhite iliidhinishwa, ilifuata ukosefu wa uwakilishi wa sawa katika tuzo ya 2015 ya Oscar.

Muelekeza filamu aliyejinyakulia sifa na tuzo Steve McQueen amesema tuzo kama za Bafta huenda zikawa hazina maana iwapo zitaendelea kushindwa kutambua vipaji.

Watu wengi wanashinikiza mageuzi yafanyike, na kwamba hatua zaidi zichukuliwe kuhusu tatizo hilo kwenye sekta hiyo, lakini suali ni je sherehe za tuzo zinazowadia zitalizingatia hilo?

Mwenyekiti wa kamati ya Bafta Marc Samuelson, amekiri kwamba uteuzi huo hazina uwakilishi sawa kama zinavyostahili kuwa.

Lakini ameshutumu sekta hiyo kwa jumla kwa tatizo linaloshuhudiwa, amesema: " Ni jambo la kukasirisha kuona kwamba sekta hii haisogei kwa kasi ambayo kikosi kizima cha Bafta ingependa isogee."