Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Shambulio la kigaidi : Watu watatu wauwawa ndani ya basi Lamu Kenya
Watu watatu wameuwawa baada ya basi la Kenya kushambuliwa karibu na mpaka wa Somalia, maafisa wameeleza.
Watu wengine wawili wamejeruhiwa na sasa wanapata matibabu katika kliniki za jirani.
Maafisa wa usalama ambao wanajumuisha wanajeshi, askari polisi, wa askari wa wanyama pori wameanzisha dorria la kuwasaka magaidi hao.
Juhudi za kusaka kundi linalosadikiwa kuwa ni magaidi wa al-shabab, waliokimbia kuelekea msitu wa Boni bado zinaendelea.
Basi lilikuwa linasafiri kutoka Mombasa na lilishambuliwa lilipofika kaunti ya Lamu na wanaume waliolisimamisha na kulimiminia risasi.
Watu waliofanya shambulio hilo bado hawajafahamika lakini nchini Somalia, kundi la kigaidi la al-Shabab limekuwa likihusika na mashambulizi kadhaa nchini humo.
Maafisa wanasema kuwa usalama wameuimarisha ili kuhakikisha wanawakamata wahusika ambao wamekimbia.
Kenya ina jeshi nchini Somalia inalosaidia Umoja wa mataifa-UN kusaidiana na serikali kupambana na magaidi wa al-Shabab.
Nchhi hiyo imekuwa katika tahadhari kubwa wakati wa sikukuu za krismasi na mwaka mpya, baada ya taarifa za intelijensia kueleza kuwa al-Shabab wanaweza kufanya shambulizi.