Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wakazi wa Mogadishu waandamana kupinga ugaidi wa al-shabab
Mamia ya wakazi wa Mogadishu wamekusanyika pamoja katika maandamano dhidi ya Al-Shabaab baada ya mlipuko kutokea siku ya jumamosi.
Waandamanaji walikamatwa katika kituo cha polisi cha mafunzo ya polisi Kahiye huku kukiwa na ulinzi mkali katika mji wote wa Mogadishu.
Kiongozi wa mtaa alipanga maandamano hayo siku chache baada ya bomu kuuwa watu zaidi ya 80 na wengine kujeruiwa katika maeneo ya pembezoni mwa mji.
Siku ya jumamosi shambulio hilo lilitokea katikati ya maeneo ya watu ambao walikuwa wanafanya shughuli zao za kila siku.
Al-Shabaab ilidai kuhusika na shambulio hilo na kudai kuwa walikuwa wamewalenga wahandisi wa Uturuki ambao walikuwa wanatengeneza barabara ya Afgoye iliyopo Mogadishu.
Kwa mara ya kwanza kundi hilo la kigaidi liliomba radhi kwa kuuwa raia.
Ingawa serikali ya Somalia inailaumu shambulio lililofanywa katika taifa la jirani ambalo halikutajwa jina.
Wakazi wa eneo hilo ambao walishiriki maandamano hayo wameeleza huzuni zao kuhusu mashambulizi ambayo yamekuwa yakifanywa na kundi la kigaidi la al-Shabaab na kuitaka serikali kuzungumzia suala hilo.
Maandamano kama hayo dhidi ya wapiganaji wa al-Shabaab yalifanyika oktoba 2017 baada ya shambulio la bomu kuuwa watu zaidi ya 600 Mogadishu.
Baadhi ya waandamanaji wanasema:
"Nimemaliza chuo cha udaktarimiaka miwili iliyopita mjini Mogadishu, kwa sasa mimi ni daktari.Nimeacha shughuli zangu ili kuungana na wasomali wenzangu kuonyesha na kuelezea uchungu wetu na jinsi tunavyoteseka na mashambulizi yanayoangamiza watu wasio na hatia siku.
Kabla ya shambulizi hili, mwaka 2017 tulishuhudia watu 600 wasio na hatia wakiuwawa.
Tuko hapa kuonyesha mshikamano na serikali yetu kupambana na ugaidi."
"Nimekuja hapa kujumuika na wenzangu kuomboleza mauaji ya Wasomali. Tunaomba Mungu atuepushie janga hili ambalo linaendelea.
Mungu awahukumu wahusika wote wa mashambulizi haya ?
Hakuna utetezi katika mauaji ya namna hii. Kwa nini wanawauwa waislamu wenzao?
Tunawaombea waliokufa na kumuomba Mungu awaponye majeruhi. Kila mtu ajumuike nasi kupinga ugaidi."