Balozi wa Marekani asema Putin ,Hitler na Stalin walishirikiana kuanzisha vita vya pili vya dunia

Chanzo cha picha, Getty Images
Mgogoro kati ya Urusi na mataifa ya Ulaya kuhusu kilichosababisha vita vya dunia vya pili umeendelea huku afisa mmoja mwandamizi wa Urusi akimshutumu balozi wa Marekani nchini Poland.
Spika wa bunge Vyacheslav Volodin alisema ujumbe wa twitter uliochapishwa na balozi Georgette Mosbacher ulikuwa ukiwatusi Warusi na Wamarekani. Siku ya Jumatatu alituma ujumbe wa twitter uliosema:
Kwa mpendwa Putin, Hitler na Stalin walishirikiana kuanzisha vita vya pili vya dunia. Lakini rais Putin anasema kwamba Poland na washirika wake wanapotosha historia.
Pia unaweza kusoma:
Wakati wa habari za marathon tarehe 19 Disemba, rais wa Urusi alisema kwamba ni makosa makubwa na haitakubalika kumlaumu kiongozi wa nazi Adolf Hitler na kiongozi wa Usovieti Joseph Stalin kwa kuzuka kwa vita hivyo.
Bwana Putin alisema kwamba alikuwa ameomba stakhabadhi za Sovieti ili kuweza kuandika kitabu kuhusu swala hilo la la uvamizi wa Nazi nchini Poland tarehe mosi Septemba na katika maoni yake ili kuweka kila kitu wazi .
Anahoji kwamba mataifa ya magharibi na Poland yaliunga mkono uchokozi wa Hitler kwa kumruhusu kunyakua Czechoslavakia mwaka 1938.
Uvamizi wa nazi nchini Poland ulijiri wiki moja baada ya waziri wa maswala ya kigeni wa Hitler Jachim von Ribbennstrop na waziri wa maswala ya kigeni wa Sovieti Vyacheslav Molotov kutia saini azimio la kusitisha uchokozi tarehe 23 mwezi Agosti 1939 ambalo liliishangaza dunia.
Kifungu cha siri katika makubaliano hayo kilinyakua mashariki mwa Ulaya ndani ya Nazi na ushawishi wa Usovieti na hivyobasi kuwaruhusu madikteta hao wawili - mmoja wao mfashisti na mwengine Mkommyunisti kunyakua na kuiharibu Poland.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ujumbe wa bi Mosbacher ulisema kwamba Poland ilikuwa mwathiriwa wa madikteta hao wawili.
Lakini bwana Volodin ambaye ni mwandani wa karibu wa Putin alisema kwamba idara ya maswala ya kigeni nchini Marekani inafaa kuhakikisha kuwa balozi kama bi Mosbacher alikuwa na habari za kutosha kuhusu historia ya taifa kabla ya yeye kutumwa kazi katika taifa hilo.
Bwana Putin amefufua ishara za kivita za Sovieti pamoja na picha za Stalin ambazo zinatumika sana Urusi kwa sasa.
Mwaka 2020, maadhimisho ya 75 ya washirika wake kuhusu ushindi dhidi ya Nazi ya Ujerumani yataadhimishwa.
Zaidi ya raia milioni 20 wa Usovieti walifariki katika kile Urusi inasema ni vita vya kizalendo baada ya Nazi kuvamia USSR 1941.
Babake Putin alihudumu katika kikosi cha Ujasusi cha Stalin na alijeruhiwa vibaya katika vita hivyo 1942.
Rais Putin alihoji kwamba Stalin alijaribu kubuni muungano dhidi ya Hitler na Uingereza, Ufaransa na Poland, lakini makubaliano ya Munich ya 1938, yaliimaliza Czechoslavakia lakini mpango huo ukaharibiwa.
''Stalin alilazimika kuweka makubaliano na Hitler , akihisi kusalitiwa na mataifa ya magharibi'', alihoji.
Lakini wanahistoria wa magharibi wanasema kwamba makubaliano ya Nazi-Sovieti yanayopinga uchokozi yanamaanisha kwamba Hitler hakufaa kuogopa vita na USSR iwapo angevamia Poland, hivyobasi kumuhakikishia alichotaka.
Zaidi ya hayo Stalin aliwapatia Nazi mashine za kivita na maliasili ambazo zilisaidia kuendeleza uchokozi wa Hitler dhidi ya mataifa ya magharibi mwa Ulaya.
Je mgogoro huo umeendelezwa vipi?
Jumatatu tarehe 30 mwezi Disemba: Mbali na ujumbe wa twitter wa balozi huyo wa Marekani, balozi wa Ujerumani wa Poland - Rolf Nikel pia aliingia katika mgogoro huo akituma ujumbe: Makubaliano ya "The Molotov-Ribbentrop Pact yalilenga kutayarisha uvamizi wa Nazi Ujerumani dhidi ya Poland. USSR pamoja na Ujerumani zilishiriki katika kuigawanya Poland.
Tarehe 29 Disemba: Waziri mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki alitoa taarifa akimshutumu rais wa Urusi bwana Putin kwa kutumia maswala ya vita vya pili vya dunia ili kuziba mapigo ya kimataifa ya Urusi ikiwemo swala la vikwazo la michezo , Bwana Morawiecki anasema rais Putin alidanganya mara kadhaa.
Tarehe 27 Disemba: Wizara ya maswala ya kigeni nchini Poland ilimtaka balozi wa Urusi nchini humo kufika mbele yake ikidai kwamba vita hivyo vilianza kufuatia muungano wa Nazi na USSR, na kwamba Poland ilipoteza zaidi ya raia milioni sita katika vita hivyo. Mapema bwana Putin aliishutumu Poland na mataifa ya magharibi kwa kumruhusu Hitler na kumtaja balozi wa Poland mjini Berlin 1930 kuwa nguruwe aliyewabagua Wayahudi.
Tarehe 19 Septemba: Makubaliano ya bunge la Ulaya yaliambia mataifa ya muungano wa Ulaya kuangazia upya uhalifu na uchokozi uliotekekelzwa na utawala wa kiimla na ule wa Nazi .
Ulielezea vita hivyo kama matokeo ya muungano wa Nazi na Usovieti wa 1932.













