Uvamizi wa Panama: Operesheni ya Marekani iliomng'oa madarakani Manuel Antonio Noriega

Uvamizi huo ulifanyika kupitia baharini, angani na ardhini. Maelfu ya wanajeshi walivamia Panama wakiwa na lengo la kumng'oa madarakani kiongozi wa taifa hilo na kumpeleka Miami ili kufunguliwa mashtaka.

Ilikuwa tarehe 20 mwezi Disemba 1989 na uhusiano wa karibu uliokuwepo kati ya jenerali Manuel Noriega na Marekani ulikuwa umezorota.

Katika hotuba yake kwa taifa , Rais George H W Bush alisema kwamba amewaagiza wanajeshi kuelekea Panama ili kulinda maisha ya raia wa Marekani na kumfungulia mashtaka Noriega.

Tangazo hilo lilijiri siku chache baada ya wanajeshi wa Panama kuwaua maafisa wa Marekani. Wakati huo, Noriega alikwa pia anakabiliwa na mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya nchini Marekani mbali na madai kwamba alikuwa amefanya udanganyifu katika uchaguzi mkuu wa 1989.

Operation Just Cause, kama ilivyojulikana ilishirikisha wanajeshi 20,000 wa Marekani ambao walivamia taifa hilo na kudhibti kambi muhimu za kijeshi.

Kirasmi wanajeshi 514 na raia waliuawa katika uvamizi huo lakini baadhi ya makundi yanasema kuwa idadi kamili inakaribia 1,000. Wanajeshi 23 wa Marekani waliuawa.

Uvamizi huo uliugeuza mji wa Panama kuwa eneo la vita.

Wafuasi wa Noriega walikamatwa wakati wa ghasia hizo.

Mtu huyu aliepatikana akiiba wakati wa uvamizi huo, alifungwa macho na kuzuiliwa na wanajeshi wa Marekani.

Raia wa Panama waliokuwa wakimpinga Noriega walisherehekea kung'atuliwa kwa kiongozi huyo.

Noriega alitafuta hifadhi katika ubalozi wa Vatican. Wanajeshi walisalia nje ya ubalozi huo katika kipindi cha Krisimasi na kucheza muziki wa sauti ya juu wa Rock ili kumshinikiza kutoka .

Nyimbo za Clash, Van Halen na U2 ni miongoni zilizochezwa.

Noriega alisalimu amri tarehe 3 mwezi Januari 1990 baada ya kuishi ndani ya ubalozi huo kwa takriban siku 11 .

Baadaye alikamatwa na kusafirishwa na kitengo cha kukabiliana na dawa za kulevya hadi Miami ili kufunguliwa mashtaka, kabla ya kupatikana na hatia ya ulanguzi wa mihadarati pamoja na ule wa kifedha.

Unaweza pia kusoma:

Noriega alihudumu kipindi chote cha maisha yake kizuizini - kwanza Marekani , baadaye Ufaransa na mwisho katika kifungo cha nyumbani nchini Panama.

Alifariki 2017, akiwa na umri wa miaka 83, kutokana na upasuaji wa kutoa uvimbe katika ubongo wake.

Picha zote zina hatimiliki.