Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Dikteta wa zamani wa Panama kufanyiwa upasuaji
Kiongozi wa zamani wa kiimla wa Panama Manuel Noriega ambaye amekuwa gerezani, ameruhusiwa kutumiwa kifungo wa nyumbani ndipo afanyiwe upasuaji kwenye ubongo wake, wakili wake amesema.
Noriega, 82, ambaye awali alikuwa rafiki mkuu wa Marekani, alitawala Panama kuanzia 1983 hadi 1989 alipotolewa kwa nguvu na majeshi ya Marekani.
Anahitaji kutolewa uvimbe kwenye ubongo.
Wakili wake Ezra Angel alifanikiwa kushawishi mahakama kwamba kiongozi huyo wa zamani anafaa kuruhusiwa kujiandaa na pia kupumzika nyumbani baada ya kufanyiwa upasuaji badala ya kukaa hospitali au gerezani.
Noriega alifungwa jela Panama kwa makosa ya mauaji, ulaji rushwa na uporaji wa mali ya umma.
Alihukumiwa akiwa hayupo kortini kwa makosa yaliyotekelezwa wakati wa utawala wake.
Alihamishwa kutoka Ufaransa kwenda Panama kutumikia kifungo chake mwaka 2011.
Atarejeshwa gerezani baada yake kupata nafuu.