Je wajua kamba Afrika ndiyo itakayoathirika pakubwa zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa?

Mtu akiwa amesimama katika mto ulio kauka kaskazini mwa Kenya

Chanzo cha picha, Getty Images

Afrika iko katika hatari kubwa ya kuathirika na mabadiliko ya hali ya hewa kulingana na mtaalam wa hali ya hewa Richard Washington.

Short presentational grey line

Afrika ndiyo itakayoathirika pakubwa zaidi.

Sababu nne kuu:

  • Kwanza ya ya Afrika inategemea pakubwa mfumo wa hali hewa; mamia ya mamilioni ya watu wanategemea mvua kukuza chakula
  • Pili, mfumo wa hali ya hewa wa Afrika inashuhudia mabadiliko makubwa ikilinganishwa na maeneo mengine yanaoishi viumbe na hivyo kutoweza kutabirika na kuongeza uwezekano wa kutokea kwa lolote.
  • Tatu, kiwango cha kubadiliko kwa hali ya hewa kiko juu huku Afrika ikishuhudia upungufu mkubwa wa mvua kuliko eneo jingine duniani hasa kaskazini mwa na kusini mwa Afrika. .
  • Na mwisho, uwezo wa kwendana na mabadiliko ya hali ya hewa uko chini huku umasikini ukipunguza kiwango cha machaguo yaliyopo na uongozi ukishindwa kuchukua hatua stahiki na kulipa suala la kukabiliana na hali ya hewa kipau mbele.

Je Afrika bado inachukuliwa uwezekano wa kutokea janga kama ndoto?

Mabadiliko ya mvua za msimu

Hali ya hewa ya Afrika inakumbwa na changamoto nyingi. Eneo la Sahara ndio jangwa kubwa zaidi lenye joto kuliko popote duniani.

Juni na Julai dhoruba kali yenye vumbi ilisambaa katika anga ya dunia ikiwa na chembe ndogo ndogo kabisa zenye kuathiri hali ya hewa kwa namna ambayo bado haijafahamika.

Pia unaweza kusoma kuhusu:

Dhoruba ya vumbi ikikaribia Khartoum Sudan mwaka 2007

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Madhara ya muda mrefu ya dhoruba ya vumbi kwa hali ya hewa bado hayajafahamika

Bado haijabainika ikiwa hali ya hewa ndio chanzo kikuu cha mfumo wa mvua za msimu magharibi mwa Afrika ambazo zinaleta mvua za miezi mitatu zenye kukatiza kiangazi cha miezi tisa katika jangwa la Sahel eneo la kusini.

Kwa miongo kadhaa kuanzia miaka ya 1960 hadi 1984, kiwango cha mvua kilipungua kwa asilimia 30 eneo la Sahel, na kusababisha baa la njaa na vifo kwa mamia ya maelfu ya watu huku wengine karibia milioni wakihama makazi yao.

Presentational grey line

Hakuna eneo jengine duniani ambalo limenakili kuwa na kiangazi cha muda mrefu kiasi hicho.

Hata hivyo inasemekana kwamba chanzo kikubwa cha hilo ni uchafuzi wa mazingira unaotokana na gesi za viwandani katika nchi za Magharibi ambako kulipoesha baadhi ya sehemu ya bahari na kuhitilafiana na mfumo wa mvua za msimu.

Na mvua zinazoshuhudiwa hivi sasa zinatabiriwa kuendelea katika karne yote ya 21, hasusan maeneo ya kati na mashariki mwa Sahel.

Wat wakiwa wamesimama kwenye vifusi vilivyofunga barabara kuu katika daraja moja baada ya mto Muruny kuvunja kingo zake magharibi mwa Poko, Kenya - November 2019

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Uwezo wa Afrika wa kuendena na mabadiliko ya hali ya hewa ni mdogo mno na hilo limesababisha maporomoko ya ardhi nchini Kenya

Lakini mabadiliko haya yanaonekana kutokea kulingana na sehemu itakayokuwa na kiwango cha juu cha joto katikati mwa Sahara.

Kusini mwa Afrika kinachojitokeza ukosefu wa mvua za msimu hali ambayo inatabiriwa kuwa mbaya zaidi katika miaka ijayo.

Kiwango cha joto eneo hilo kinabashiriwa kuongezeka kwa nyuzi tano au zaidi, hasa maeneo ya Namibia, Botswana na Zambia ambayo tayari yanashuhudia kiwango cha juu cha joto.

Fumbo la Afrika Mashariki

Wakati huo huo, Kenya na Tanzania, mvua ndefu za Machi na Mei zinaanza kuchelewa na kumalizaka mapema na kusababisha kupungua kwa mvua.

Map
Presentational white space

Hali hiyo imefanya iwe vigumu kubashiri kiwango cha mvua siku zijazo tatizo ambalo wanasayansi wamelipa jina la fumbo la hali ya hewa Afrika Mashariki.

Afrika ya kati, moja ya maeneo ambayo yanashuhudia dhoruba yenye ngurumo na kusababisha kiwango cha chini cha mvua kinachohitajika katika eneo hilo ambalo ni la pili duniani kuwa na misitu ya mvua.

Msitu wa mvua Jamhuri ya Kodemokraisa ya Kongo ukionekana kutoka juu ya anga

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hata upungufu mdogo tu wa mvua sikua zijazo kutahatarisha misitu ya mvua Afrika ya Kati

Upungufu wa mvua kidogo siku zijazo kutahatarisha misitu na kiwango kikubwa cha kaboni inachohifadhi.

Kuna ufahamu mdogo sana kuhusu mfumo wa hali ya hewa kiasi kwamba kinafuatilia kwa karibu ulimwenguni. Inasemekana kwamba vipima mvua vilivyopo Uingereza eneo la Oxfordshire ni vingi mno kuliko hata bonge lote la Kongo.

Mfumo wa Afrika wa mabadiliko ya hali ya hewa unasemekana kuendeshwa pakubwa na mabonde matatu ya bahari duniani.

Kuanzia moja ya bahari yenye kiwango cha juu cha joto, vimbunga Idai na Kenneth vilitokea Machi na Aprili 2019 na kuharibu sehemu za Msumbiji, Zimbabwe na Malawi, huku kimbunga Kenneth kikielekea Tanzania jambo ambalo halikuwa la kawaida.

Matumaini kisayansi

Katika juhudi za pamoja wanasayansi wanashirikiana na kujitahdi kuhakikisha hali ya hewa inaweza kutabirika.

Eneo la karibu na Beira lililozama kwa maji baada ya kutokea kwa kimbunga Idai huko Msumbiji

Chanzo cha picha, AFP/UN

Maelezo ya picha, Zaidi ya watu 1,000 waliaga dunia baada ya kimbunga Idai kukumba Msumbiji na Zimbabwe

Utabiri wa mabadiliko ya hali ya hewa ni jambo gumu kama ilivyo kwa dunia yenyewe.

Hata hivyo, kupitia juhudi kama vile mradi wa Hatma ya Baadaye ya Afrika unaofadhiliwa na Uingereza, tajriba iliyopo na uelewa wa wanasayansi wa Afrika umepelekea ufahamu mzuri wa hali ya hewa Afrika.

Uelewa huu umejitokeza kupitia ubunifu wa wanasayansi.

Kila eneo Afrika linabadilika kwa namna tofauti lakini kile kinachofanana ni juhudi za pamoja katika upatikanaji wa mvua hata kipindi ambapo siku za baadaye zinatabiriwa kuwa kiangazi.

Mvua zinanyesha kwa kipindi kifupi tena zinakuja kwa wingi na kusababisha maafa pamoja na kushuhudiwa kwa vipindi virefu vya kiangazi.

Mbinu mpya zilizovumbuliwa katika mradi wa Uingereza, zimefufua matumaini na kuwa suluhu ya tatizo hili kwa bara zima la Afrika.

Fahamu dhoruba ya ngurumo

Matokeo yake ni kuongezeka maradufu kwa kiwango cha mvua pamoja na kipindi cha kiangazi.

Kikubwa katika mabadiliko ya mvua ni uwepo wa radi, ambayo inasemeka kuwa chanzo cha silimia 70 ya mvua zinazonyesha Afrika

Wilfried Pokam (wa pili kurshoto), aliongoza watafiti Cameroon, na ni miongoni mwa wasayansi wanaosaidia katika utafiti wa mabadiliko ya hali hewa Afrika.

Chanzo cha picha, RICHARD WASHINGTON

Maelezo ya picha, Wilfried Pokam (wa pili kurshoto), aliongoza watafiti Cameroon, na ni miongoni mwa wasayansi wanaosaidia katika utafiti wa mabadiliko ya hali hewa Afrika.

Mbinu za kawaida duniani za ufuatiliaji wa mabadiliko ya hali hewa zinawakilisha mifumo muhimu pekee lakini kwa mara ya kwanza mbinu mpya zina uwezo wa kuwakilisha mifumo ya radi.

Hizi ndio baadhi ya mbinu ambazo zimeanza kutumika kubaini hasa kile kinachochochea mabadiliko ya hali ya hewa.

Maabara moja yenye vifaa vya kisasa huko Cameroon, kwa mfano Wilfried Pokam na timu yake ya watafiti wamebaini uhusiano uliopo kati ya mfumo wa hali ya hewa wa Afrika ya Kati na Kusini mwa Afrika na kupata suluhisho ya kile ambacho kimekuwa tatizo kwa muda mrefu.

Serikali za Afrika zimeshindwa kutoa kipaumbele kwa mabadiliko ya hali ya hewa.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Serikali za Afrika zimeshindwa kutoa kipaumbele kwa mabadiliko ya hali ya hewa.

Matokeo kama hayo inakuwa vigumu kuaminika ikizingatiwa kwamba watafiti wanalazimika kupakuwa data kubwa kupitia simu zao za mkononi na kuchambua data hiyo usiku mzima.

Hata hivyo, wamefanikiwa kuweka mfumo wa kwanza wa mbinu ya utafiti Afrika ya Kati. Mfumo huo unapima upepo katika umbali wa karibu wa angahewa.

Kuna baadhi ya wanasayansi chipukizi wanaojiunga na nyanja hiyo ilikusaidia kutengeneza mazingira ya kwendana na mabadiliko ya hali ya hewa kabla uharibu wa hali ya hewa Afrika haujafikia kiwango cha kutoweza kudhibitiwa.

Jamii itatendewa haki tu iwapo ufumbuzi utapatikana.

Ukweli uliodhahiri ni kwamba Afrika itaathirika vibaya na mabadiliko ya hali ya hewa licha ya kwamba mchango wake katika uchafuzi wa mazingira ni kidogo sana.