Uhifadhi wa mazingira: Tumefika wapi katika juhudi hizo?

Chanzo cha picha, Getty Images
Ukataji wa misitu, uchafuzi wa mazingira baharini na nchi kavu, uchafuzi wa maji na hali ya hewa ni baadhi ya mambo yanayotishia kuangamiza mazingira asilia duniani.
Hili ni onyo ambalo linatarajiwa kutolewa na zaidi ya wataalamu 500 kutoka mataifa 50 katika ripoti yao inayoungwamkono na Umoja wa Mataifa Jumatatu hii.
Ripoti hiyo itaangazia uharibifu unaokumba mazigira asilia duniani katika kipindi cha miaka 50 na jinsi maisha ya baadae ya mamia ya viumbe yatakavyo hatarini.
Ripoti hiyo pia inatarajiwa kutoa muongozo wa dharura wa hatua zitakzochukuliwa kuokoa mazingira
Kwa hivyo tunafahamu nini kuhusu mazingira na afya ya viumbe kadhaa vinavyoishi duniani?
1. Mazingira asilia inakabiliwa na tishio la kuangamia
Kutathmini orodha ya IUCN ya viumbe hai wanaokabiliwa na tishio la kuangamia ni hatua muhimu katika suala la uhifadhi mazingira.
Karibu viumbe hai 100,000 wamechunguzwa kufikia sasa kubaini ni wapi wanakabiliwa na tishio la kuangamia.
Kati ya hao zaidi ya robo moja wanakabiliwana tishio la kuangamia, miongoni mwa chura wa kipekee wanaopatikana Madagascar anayefahamika kama 'salamanders', na mimea kama vile conifers na orchids.


Uchunguzi haujakamilika lakini mpaka sasa hatuna idadi kamili ya viumbe hai vilivyopo duniani.
Inakadiriwa kuwa viumbe hai hivyo ni kati ya milioni mbili hadi trillioni moja, blakini wataalamu wengi wanasema ni karibu milioni 11 au chini ya hapo.

Wanasayansi wanamini kuwa dunia inakabiliwa na tishio la kuangamia - katika miaka kadhaa zijazo
"Sasa kuna ushahidi wa kutosha kuwa ulimwengu unapoteza viumbe hai kwa kiwango kikubwa," Prof Alexandre Antonelli, mkurugenzi wa sayansi katika bustani la Royal Botani, Kew, aliaimbia BBC.
Mwara ya mwisho hali kama hiyo ilishuhudiwa karibu miakamilioni 66, ilisababishwa na asteroid kugonga dunia, alisema kuwa sasa hivi hali hiyo inachangiwa na ''binadamu''
Viwango vya uharibifu sasa ni karibu mara 1,000 zaidi ya ilivyokua kabla wanadamu kuingilia kati na kuongeza uharibifu kwa zidi ya mara 10,000.

Chanzo cha picha, Getty Images
2. Miongoni mwa vitu vinachangia uharibifu wa mazingira ni mabadiliko ya hali ya hewa
Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni mabadiliko ya hali ya hewa bado ni tisho kubwa katika uhifadhi wa mazingira.
Vitu vingine vinavyochangia uharibifu huo ni kupotea kwa mazingira asilia kutokana na kilimo,ufugaji, uchongaji mbao, uwindaji, uvuvi, na shughuli za uchimbaji madini .


Wanyama kama vile pangolin wanakabiliwa na tishio la kuangamia kutokana na uwindaji haramu.
Ukataji wa miti kwa ajili ya kutengeneza mbao umechangia kupungua kwa idadi ya tumbili wakipekee nchini Myanmar.
Kuongezeka kwa shughuli ya kilimo pia kumetajwa kuwa sababu ya baadhi ya wanyama kama vile chui kutoweka.

"Serikali zimejikita zaidi katika suala la mabadiliko ya tabia nchi na kusahau kuangazia uharibifu wa mali asilia unaotokana na uharibifu wa ardhi, Mwenyekiti wa " IPBES', Prof Sir Bob Watson, aliambia BBC.
"Vyote vitatu ni muhimu kwa afya ya binadamu."
3. Wanyama na mimea wanaangamia kadri makaazi asilia inavyoharibiwa
Uharibifu kutokana na shuguli za binadamu umeathiri karibu watu bilioni 3.2 billion hali ambayo pia ina athari kwa mazingira dunia, kwa mujibu wa IPBES.
Hali ambayo imechangiwa zaidi na ukulima usiyokuwa na tija na uharibifu wa mazingira, mabadiliko ya hali ya hewa na katika baadhi ya sehemu, upanuzi wa makaazi katika maeneo ya mijini, ujenzi wa barabara na uchimbaji madini.
Uharibifu wa ardhi unatokana na ukataji wa misitu, huku kimataifa hali hiyo ikidhibitiwa kupitia upandaji wa miti.
Karibu hekari milioni 12 ya misitu duniani katika maeneo ya tropiki yaliangamia mwaka 2018, hii ikiwa ni karibu viwanja 30 vya mpira vinavyoharibiwa kila dakika kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni.

4. Uhifadhi wa makaazi asilia
Kwa mujibu wa IPBES, ni robo tu ya ardhi duniani ambayo haijaathiriwa na shughuli za binadamu.
Hali hii inatarajiwa kuimarika kwa kiwango kidogo ifikapo mwaka 2050.
"Suala la utumizi wa ni changamoto kubwa la uhifadhi wa mazingira tunalokabiliana nalo," Prof Mercedes Bustamante wa Chuo kikuu chaBrasilia aliiambia BBC.
Tangu mwaka 2001, Indonesia imepoteza mamilioni ya hekari ya misitu ya mvua lakini hali hiyo ilibadilika mwaka 2018 uharibifu huo ulipungua kwa 40%.
Hii ni kutokana na sheria kali zilizobuniwa na serikali kuhakikisha misitu inalindwa dhidi ya moto.


Katika maeneo ya kusini mashariki ya Asia misitu katika nyanda za chini ya visiwa vya Borneo na Sumatra, IPBES inakadiria kuwa aina tatu ya ndege na karibu robo ya wanyama wataangamia ikiwa uharibifu wa misitu utaendelea.
5. Baadhi ya misitu mikubwa duniani inaangamizwa
Eneo la Amazon linafahamika kwa kuwa na misitu ya tropiki ambayo ina mimea na wanyama wapya wanaogunduliwa
Rondônia, iliyopo magharibi mwa Amazon, ni moja ya sehemu zilzoharibiwa sana katika eneo la Amazon.
Miti inakatwa ili kufanya shughuli za kilimo, kutengeneza mbao, kufanya shughuli za kuchimvba madini au kulisha mifugo.
Kadri muda unavyosonga ndivyo misiti inavyoharibiwa na maeneo hayo kugeuzwa kuwa makaazi ya watu.













