Shambulio la Mexico la walanguzi wa dawa za kulevya lililorindima saa kadhaa

Relatives of victims look at burned vehicle

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Jamaa wa wahanga wa mashambulio wakiangalia gari la mpendwa wao lililokuwa na watu wanne lililoungua

Mvulana mwenye umri wa miaka 13-amenusurika na shambulio linaloshukiwa kuwa ni la wajumbe wa mtandao wa ulanguzi wa dawa za kulevya nchini Mexico dhidi ya msafara wa wafuasi wa dhehebu la Mormon la Marekani ambapo alifanikiwa kuwaficha ndugu zake sita vichakani kabla ya kutembea kilomita 23 sawa na maili 14 ili kuomba msaada, imeeleza familia yake.

Watoto tisa walinusurika na shambulio hilo la Jumatatu lililotokea kaskazini mwa Mexico ambapo wanawake watatu waliuwawa na watoto wengine sita.

Unaweza pia kusoma:

Watoto watano miongoni mwao wana majeraha ya risasi, vimeripoti vyombo vya habari vya Marekani.

Waathiriwa ni wajumbe wa familia ya LeBaron, yenye uhusiano na dhehebu la Mormon waliokuja na kuishi nchini Mexico miongo kadhaa iliyopita.

Waziri wa usalama wa Mexico, amesema kuwa huenda familia hiyo ililengwa kwa bahati mbaya kwa utambulisho uliokosewa . Hata hivyo watu wa familia hiyo wamesemakana kuwa wamekuwa wakiongea wazi kulaani mashambulio ya mitandao ya magenge , na awali walipokea vitisho

Jimbo la Sonora lililoko kaskazini mwa Mexico linapiganiwa na magenge mawili hasimu, huku jenge la La Línea, ambalo lina uhusiano na mtandao mkubwa wa Juárez cartel, na lile la "Los Chapos", ambalo ni sehemu ya mtandao wa Sinaloa yote yakiwa ni yawalanguzi wa madawa ya kulevya.

Watoto waliwezaje kutoroka?

Kikundi cha akinamama watatu na watoto wao 14 waliondoka katika msafara wa magari matatu kutoka eneo la Bavispe katika jimbo la Sonora Jumatatu asubuhi na walikuwa wakielekea katika jimbo jirani la Chihuahua.Wanawake hao walikuwa wakisafiri kwa pamoja "kwasababu za kiusalama", mmoja wa ndugu aliiambia televisheni ya CNN.

Christina Langford Johnson and baby Faith

Chanzo cha picha, Reuters/handout

Maelezo ya picha, BI Langford Johnson aliuawa lakini mtoto wake mchanga Faith alinusurika
Presentational white space

Walishambuliwa ghafla na watu wenye silahakatika eneo Bavispe. Baada ya mama yake na kaka zake wawili kupigwa risasi na kufa , Devin Langford, mwneye umri wa miaka 13, aliwafisha ndugu zake wengine sita vichakani na akawafunika na matawi ya miti. Halafu akatembea kwa saa sita hadi katika eneo la makazi ya watu la La Mora, alisema mmoja wa ndugu Kendra Lee Miller kupitia ujumbe wake alioutuma kwenye Facebook.

Mmoja wa dada zake na Devin mwenye umri wa miaka 9 kwa jina McKenzie, hatimae aliwaacha ndugu zake waliobaki watano na kutembea kwa saa nnekwenye giza baada ya Devin kutorejea . Baadae alipatikana alipotafutwa na waokozi.

Mtoto mchanga mwenye umri wa miezi saba, Faith Langford, pia alinusurika baada ya kiti chake cha watoto kuachwa chini kando ya gari na mama yake Christina Langford Johnson. Bi Langford Johnson alitoka nje ya gari huku akiwa amenyanyua mikono yake juu akiwaomba washumbuliaji kuacha kufyatua risasi lakini alipigwa risasi akaanguka chini, alisema mmoja wa watu walioshuhudia tukio hilo.

Baada ya mvulana Devin kufika La Mora, wakazi wake eneo hilo walijihami, waijiandaa kutoka kuelekea eneo la tukio la shambulio hilo la risasi. Lakini waliamua kusubiri maafisa wa usalama baada ya "kubaini kuwa kungekua na hatari ya kifo, kwasababu ufyatuaji wa risasi ulikuwa ukiendelea kwa saa kadhaa katika maeneo yote ya milima karibu na La Mora", alisema Miller.

Hatimae walimpata Faith ndani ya gari saa 11 baada ya shambulio

Map

Manusuira wa shambulio walisafirioshwa kwa ndege hadi katika mji wa Marekani wa Phoenix. Cody mwenye umri wa miaka minane alikuwa amepigwa risasi kwenye kidevu na mguuni mwake , Kylie, mwenye umri wa miaka 14, alikuwa amepigwa risasi kwenye mguu, Xander mwenye umri wa miaka 4 alipigwa risasi mgongoni na Brixton mwenye umri wa miezi 9 alipigwa risasi kifuani.

Waliokufa ni akina nani ?

Watano miongoni mwa waliouawa ni Maria Rhonita Miller aliyekuwa na umri wa miaka 30 na watoto wake mapacha Titus na Tiana waliokuwa na miezi 9 , Howard Jr aliyekuwa na umri wa miaka 12 na Krystal mwenye umri wa miaka 10./

Photo of Rhonita Miller and her family

Chanzo cha picha, CBS news

Maelezo ya picha, Maria Rhonita Miller na familia yake

Kilomita kadhaa nyuma yao magari mengine mawili yalishambuliwa. Dawna Langford, mwenye umri wa miaka 43, na watoto wake wavulana mwenye miaka 2 na 11 waliuawa pia . Bi Langford Johnson, mwenye umri wa miaka 31, aliuawa baada ya kutoka kwenye gari jingine

Katika ujumbe wake wa Twitter, rais Donald Trump aliwaelezea wahanga wa shambulio hilo kama kikundi cha "familia na marafiki wazuri" ambao "walijipata katika vita vya mitandao miwili ya masawa ya kulevya , waliokua wakifyatuliana risasi ".

Extra security forces have been sent to the area

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Vikosi vya ziada vya usalama vimepelekwa kwenye eneo la tukio

Rais Trump alijibu kwa kusema " yuko tayari" kutoa msaasa wa kukabiliana na tatizo la mitandao ya ghasia na "kufanya kazi hiyo haraka na kwa ufanisi ". Imeripotiwa kuwa maafisa wa FBI wametoa msaada kwa maafisa wa Mexico katika uchunguzi.