Mamilioni ya tani za mabaki ya chakula hutupwa kila mwaka duniani

Chanzo cha picha, Getty Images
Karibu tani bilioni 1.3 za chakula hutupwa kila mwaka, hali ambayo huchangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya tabia ya nchi.
Mabaki ya chakula '' ni moja kati ya matatizo makubwa yanayokabili binaadamu hii leo, limeeleza jarida la New York Chef Max La Manna.
Unaweza pia kusoma:
Yeye ni mwandishi wa makala za ''More Plants, Less Waste'' na hapa anaeleza ni namna gani unaweza kuleta mabadiliko

Chakula siku zote ni kiungo kikuu katika maisha yangu. Kuwa na baba mpishi, nilikua katika ulimwengu wa chakula.
Wazazi wangu wakati wote wlinifundisha kutokutupa chakula. Duniani karibu watu milioni tisa, tunakabiliwa na tatizo la ukosefu wa chakula na zaidi ya watu milioni 820 hawana chakula cha kutosha.

Chanzo cha picha, Andrew Burton
Mabaki ya chakula ni tatizo kubwa linalokumba binaadamu hivi leo- takribani theluthi moja ya chakula kinachozalishwa ulimwenguni hutupwa.
Kutupa chakula kunamaanisha kupoteza pesa, maji, nguvu, ardhi na gharama za usafirishaji.
Kutupa chakula pia kunaweza kuchangia mabadiliko ya tabia nchi. Chakula kilichotupwa ardhini huoza na kuzalisha gesi ya Methane.
Unaweza kufanya yafuatayo kuondokana na tabia hii
Fanya manunuzi kwa malengo

Chanzo cha picha, Getty Images
Watu wengi hununua zaidi ya wanachohitaji.
Nunua kwa malengo kwa kuorodhesha mahitaji na kununua kilicho kwenye orodha.
Maliza chakula chote ulichonunua kwenye manunuzi yako ya mwisho sokoni kabla ya kununua mahitaji mengine.
Hifadhi vizuri chakula

Chanzo cha picha, Getty Images
Kutotunza vizuri chakula kunasababisha vyakula kutupwa. Watu wengi hawana uhakika namna wanavyoweza kutunza matunda na mbogamboga, hivyo kufanya viive na hatimaye kuoza kabisa.
Kwa mfano, viazi, nyanya, matango na vitunguu havipaswi kuwekwa kwenye jokofu. hivi vinapaswa kuwekwa kwenye chumba chenye joto la kadiri.
mashina ya mboga na mizizi yanaweza kutumbukizwa kwenye maji.
Tunza chakula kinachobaki ( unaweza kukila hicho pia)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiporo cha chakula si kwa ajili ya nyakati za mapumziko ya sikukuu pekee.
Ikitokea umepika chakula kingi na kikabaki, tafuta wakati wa kukila na kingine chochote kilichokusanywa kwenye jokofu.
Ni namna nzuri ya kuepuka kutupa chakula, zaidi ya hayo inasaidia kuokoa muda na fedha.
Kuwa rafiki na jokofu lako

Chanzo cha picha, Getty Images
Kugandisha chakula kwenye jokofu ni njia rahisi ya kukitunza.
Kwa mfano, mbogamboga ambazo kidogo ni laini zinazoweza kutumika kwenye kachumbari zinaweza kuwekwa kwenye mifuko au mikebe na kutumika siku nyingine kama kuchanganya na juisi na viungo vingine.
Weka chakula chako kwenye mikebe

Chanzo cha picha, Getty Images
Fanya kuwa mbolea ukiweza

Chanzo cha picha, Getty Images
Kukifanya mbolea chakula kilichobaki ni njia nzuri ya kubadilisha mabaki ya chakula kuwa nishati ya mimea.
Pamoja na kuwa si kila mtu mwenye nafasi kubwa ya mfumo wa kusindika mabaki, kuna mfumo rahisi ambao unaweza kumfaa kila mmoja ambaye hana sehemu kubwa ya kutosha.
Kurundika nje kunafaa zaidi kwa watu wenye bustani kubwa.
Hatua ndogo, matokeo makubwa

Chanzo cha picha, Getty Images
Hitimisho ni kwamba tunaweza kupunguza kiasi cha takataka na kuna namna mbalimbali za kufanya hivyo. Na kwa kufikiria kuhusu chakula unachotupa kila siku, unaweza kusaidia kuleta mabadiliko kwa kukitunza na kutunza mazingira.
Hata mabadiliko kidogo kuhusu namna unavyonunua, kupika na kutumia chakula kunaweza kupunguza athari kwa mazingira.
Kwa jitihada za bila kutumia nguvu, unaweza kupunguza kukitupa, na kuokoa fedha, muda na kuokoa mazingira.












