Ni namna gani watu wanaweza kupika mimea yenye sumu kuwa chakula salama?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwaka 1860, Robert Burke na William Wills walifahamika kwa kuongoza msafara wa kwanza barani ulaya ambao ulijulikana Australia yote.
Msafara huo haukwenda vizuri kutokana na uongozi mbaya na mipango isiyokuwa na utaratibu pamoja na mikosi.
Wakati wa kurudi, wasafiri hao walipata changamoto ya chakula na kutokuwa na maji ya kutosha .
Hali hiyo ya kukwama jangwani bila chakula iliwapelekea kutengeneza chakula ambacho walijua ni sumu lakini walikuwa hawana njia nyingine ya kuendelea kuishi.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Ngamia wote walikiwa wanakufa kwa sababu tulikuwa hatuna chakula cha kuwapa na tulikuwa tunajaribu tuweze kupona iwezekanavyo."
Wanakijiji wa eneo hilo la Yandruwandha walikuwa wanaishi licha ya hali ya eneo hilo.

Wenyeji waliwapa keki ambazo zimetengenezwa na unga wa mhogo .
Njaa za wasafiri hao Burke,Wills na King ziliwafanya kutokua na jinsi zaidi ya kula kwa sababu walikuwa wameishiwa nguvu.
King ndio msafiri pekee aliyetarajiwa atapona baada ya miezi kadhaa ambapo msaada ulifika kutoka ulaya
Chakula kilichowafanya kupona jangwani, kilifanya watu wafanye udadisi.

Chakula hicho hicho cha muhogo,mtu hawezi kusema kuwa ni sumu katika nchi nyingi za Afrika.
Wakulima barani Afrika wanalima zao hilo kwa ajili ya chakula na biashara.
Ingawa hata baadhi ya maeneo nchini Tanzania baadhi ya makabila huwa ni mwiko kwao kula mhogo kwa madai kuwa ni sumu.
Nchini Tanzania , wenyeji wa Kilimanjaro wa kabila la wachaga wamekuwa wakidai kuwa chakula hicho ni sumu na hivyo kuwa na utamaduni wa kutokula mihogo.
Lakini siku za hivi karibuni hali imeanza kubadilika pia.

"Ni sisi wachaga wa mjini hapa Dar es salaam ndio tunakula mihogo lakini asili yetu tangu enzi na enzi huwa hatuli mihogo kwetu kwa sababu tunaamini kuwa ni sumu." Mtanzania mmoja mwenye asili ya uchaga alieleza.
Mihogo ni chakula ambacho kina virutubisho vingi kwa afya ya binadamu kama vitamini na madini.Kuna mihogo ambayo ni mitamu na ambayo michungu.
Utofauti wa mhogo wenye sumu na usio kuwa na sumu utegemea eneo ambalo zao hilo umekuzwa.

Mihogo inaliwa kama chakula katika nchi zinazoendelea peke yake.
Tangu mwaka 1984 ,zao hilo limekuwa kwa kasi barani Afrika tofauti na mabara mengine.
Bei ya mihogo katika soko la kimataifa limekuwa kutokana na ongezeko la uhitaji na bidhaa ambazo zinaweza kutengenezwa kutokana na zao hilo.
Huku wengine wakiamini kuwa mihogo kuwa dawa vilevile.Mfano jijini Dar es salaam, mihogo imekuwa ikiuzwa mibichi barabarani.

Chanzo cha picha, Thorkild Tylleskar
Zaidi ya asilimia 50 ya mihogo inapatikana barani Afrika.
Nchi 39 za Afrika zinalima zao hili la kuanzia Madagascar Senegal na asilimia 70 ya maeneo ya Nigeria, DRC na Tanzania.
Nchi hizo zinazalisha mihogo kama chakula na wanajipatia kipato kwa kilimo cha miezi 12 mpaka 24.

Nchi nyingine za Afrika zinazolima mihogo kwa wingi ni Msumbiji ,Uganda,Ghana,Angola na Cameroon.
Kuna namna yake ya kuondoa sumu katika mizizi ya mihogo.
Mwaka 1981, mjini Nampula kutoka Swedish Hans Rosling alisema kuwa watu wengi walifika hospitalini kwa ajili ya matibabu kwa sababu walikuwa wamepooza.
Ilidaiwa kuwa ni ugonjwa wa polio ingawa dalili zake hazikuwahi kuandikwa katika kitabu lakini sababu za kuugua kwao kulitokana na mihogo.
Barani Afrika...mihogo ilianza kuliwa katika karne ya 17 mara baada ya watu kuelewa kanuni za ulimaji wake.













