Idadi ya watu Kenya yaongezeka na kufikia milioni 47.5 katika muongo mmoja

sensa
Maelezo ya picha, Mji wa nairobi ndio una idadi kubwa zaidi ya watu

Idadi ya watu nchini Kenya imeongeza hadi kufikia milioni 47.5 kwa mujibu wa chapisho la matokeo ya idadi ya watu maarufu sensa iliyotewa siku ya Jumatatu.

Hii ni sensa ya sita kufanyika tangu kupatikana kwa uhuru nchini humo. kwa mara ya kwanza watu wenye jinsia mbili walihesabiwa kama kundi maalum, watu hawa hawapo kwenye kundi la wanaume au wanawake.

Unaweza pia kusoma:

Matokeo hayo yalichapishwa na bodi ya takwimu ya Kenya, ilisema kuwa wanawake wapo millioni 24 na wanaume wanaume wakiwa 23.5 na zaidi ya watu wenye jinsia mbili 1500.

sensa

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Baadhi ya maofisa wa sensa, wakiwa wanajiandaa na zoezi la kuhesabu watu lilofanyika mwezi Agosti.

Mji wa Nairobi pekee ndio wenye watu wengi zaidi, ukiwa na watu milioni 4.4.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyata anasema kuwa idadi ya watu itasaidia sana katika kuandaa mikakati ya maendeleo.

Kenya ilianza zoezi la kuhesabu watu yaani sensa mwezi agasti. Serikali hutumia shughuli hii ili kujua jinsi ya kupanga na kukadiria matumizi ya raslimali na fedha lakini pia wanasiasa hutumia idadi ya watu na maeneo walioko kutathmini azma zao za kisiasa.

katika kipindi cha sensa ya mwaka huu, raia nchini Kenya walitumia mitandao ya kijamii kuelezea kutoridhishwa kwao na hatua ya kufunga maeneo ya burudani ili kufanikisha mpango wa kitaifa wa kuhesabu watu.

Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang alizua gumzo nchini humo baada ya kutangaza mabaa na kumbi za burudani kufungwa kwa ajili ya shughuli ya kuhesabu watu maarufu sensa.

Unaweza pia kusikiliza;

Maelezo ya video, Sensa Kenya: Kwa mara ya kwanza Afrika watu walio na jinsia mbili wasajiliwa