Sensa Kenya: Kwa mara ya kwanza Afrika watu walio na jinsia mbili wasajiliwa

Maelezo ya video, Sensa Kenya: Kwa mara ya kwanza Afrika watu walio na jinsia mbili wasajiliwa

Kenya inaandikisha historia barani Afrika kwa kuwajumuisha huntha (watu wanaozaliwa na jinsia mbili) kwenye zoezi la kuhesabu Wakenya. James Karanja, ambaye alilelewa kama msichana hadi akiwa miaka 18, anaeleza masaibu yanayowakumba watu wanaozaliwa na hali kama yake.